Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 17 Safar 1446 | Na: H 1446 / 014 |
M. Alhamisi, 22 Agosti 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina Sio Karata ya Uchaguzi kwa Ruwabidha Mzembe
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 19/8/2024, Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitoa wito kwa Misri kufungua mipaka na Ukanda wa Gaza kwa jeshi la Algeria, ili kuwanusuru wakaazi wa Ukanda wa Gaza, na kusema: “Naapa kwamba haraka iwezekanavyo tutapeleka vitengo huko na kujenga upya kile kilichoharibiwa,” na akasema: “Jeshi la Algeria liko tayari kwenda Gaza na sisi tuko tayari, tunasubiri tu Misri itufungulie mipaka yake.” Katika taarifa iliyochapishwa kwenye kituo cha Televisheni cha Bilad kwenye YouTube, Tebboune, ambaye anagombea katika uchaguzi ujao wa rais mnamo Septemba 7, alisema: “Wallahi kama wangetufungulia mipaka, tungepeleka jeshi huko. Tungepeleka mabasi huko na kujenga hospitali tatu ndani ya siku 20. Tungetuma madaktari na kujenga upya kile ambacho Wazayuni waliharibu. Gaza sio kadhia ya Wapalestina, bali ni kadhia yetu sote,” na akafafanua kwamba jeshi la nchi yake liko tayari kusonga mara tu mipaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza inapofunguliwa.
Baada ya miezi kumi ya watawala wa Waislamu na majeshi yao kuwakatisha tamaa watu wa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na Gaza, hatukuwa na matumaini kwamba uhai ungefufuka ndani ya watawala hawa, ili uungwana wa Al-Mu'tasim utokee ndani yao na wangesimama kwa ajili ya wanawake wa Gaza na watu wake. Imethibiti kwa kila aliye mbali, wale wanaoshirikiana mipaka ya Gaza na Palestina na walio mbali nayo, kwamba watawala hawa Ruwaibidha (wajinga) wa Waislamu wanakula njama na Mayahudi dhidi ya ardhi ya Isra na Mi'raj na watu wake. Hatutarajii jema lolote kutoka kwao, bali maovu yote. Kauli za Tebboune zilikuja kuthibitisha hili. Ingawa ana hakika kwamba kadhia ya ardhi iliyobarikiwa ya Palestina ni kadhia ya kijeshi, sio ya kisiasa, kadhia ya majeshi, sio viti vya enzi, anapotosha kwa ubaya wote. Katika sehemu ya hotuba yake kuhusu kile kinachotokea Gaza, na msisitizo wake kwa jeshi kuchukua mahali pake, alilitaja kama shirika la matibabu ya kibinadamu! Kana kwamba dori ya majeshi wakati wa vita, uharibifu, mauaji ya Waislamu na kuvunjwa heshima ni kujenga hospitali, kutengeneza barabara, na kuzindua bustani na mbuga! Tebboune pia anajua kwa hakika kwamba nchini Misri, nchi ya Kinana, kuna Firauni ambaye anatangaza wazi uadui wake kwa Uislamu, Waislamu na watu wa Gaza na kula njama na Mayahudi dhidi yao. Anajua vizuri kwamba Farauni wa Misri hatafungua mipaka. Anawezaje wakati yeye ndiye anayelinda mipaka kwa kuogopea Muislamu au mwanajeshi yeyote kutoka ardhi ya Kinana (Misri) kusonga mbele ya askari wa Algeria, Tunisia na kizazi cha Omar Al-Mukhtar nchini Libya, na sio kwa kuogopa harakati ya Tebboune na mfano wake kutoka kwa wanafiki?! Kwa hiyo, Tebboune anahakikishiwa katika madai yake kwamba Farauni wa Misri hatafungua mipaka na ataishi na matarajio yake mabaya zaidi ndani yake. Mwenyezi Mungu awapige vita wote wawili.
Si tu kwamba jeshi la Misri (Kinana) lina uwezo wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ndani ya muda wa saa moja tu, bali pia jeshi la Algeria linaloshika nafasi ya pili katika nchi za Kiarabu baada ya jeshi la Misri, linaloshika nafasi ya tisa kwa kiidadi duniani, na ya kumi na tano ulimwenguni katika suala la uwezo wa mapigano na vifaa, kwani viungo vyake vilivyo tayari na vilivyotayarishwa kwa mapigano vinakadiriwa kuwa askari 603,000. Pia lina uwezo wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa kutoka katika makucha ya Mayahudi na kukinajisi kwao Kibla cha kwanza kati ya Viblah viwili na ya tatu ya Haramain. Kikwazo kinachowakabili majeshi si udhaifu au unyonge, bali ni usaliti wa watawala wa Waislamu na kuwaangusha kwao Waislamu wa Gaza, baada ya kutoa ahadi wenyewe kwamba hawatatulia mpaka wawape nguvu Mayahudi katika Ardhi iliyobarikiwa na wainuke pakubwa. Ili kufanikisha hili, wanakwamilia viti vyao vya enzi, na wanajitahidi sana kuchakachua chaguzi ambazo zitawafanya wafanikiwe kwenye viti vya enzi (vya madaraka), wakitumia kadhia tukufu zaidi kama karata ya uchaguzi ili kufikia malengo machafu zaidi!
Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi katika Majeshi ya Misri, Jordan, Pakistan na Algeria!
Mwenyezi Mungu amekujaribuni kwa kukufanyeni ni boma la Ummah, ukuta wake wa ulinzi na nguvu zake za kushambulia. Kwa nini mumetulia tuli bila kuwanusuru watu wenu huko Gaza huku mukiwaona Mayahudi wachache wakiwashambulia bila uoga wala wasiwasi?! Hata kama hali ingekuwa mbaya na mukavamia nyumba zao, hawangebaki mbele yenu hata kwa saa moja. Mliwaona mnamo Oktoba 7, 2023, wakati kikundi cha waumini kilipovamia nyumba zao na vifaa vyao vya kawaida, na wakakimbia mbele yao kama ndege wadogo, bila kuangalia nyuma kwa hofu ya kile walichokiona juu ya ushujaa wa ndugu zenu. Kwa hivyo, vipi kama wangekabiliana na jeshi kama la Misri (Kinana), au jeshi la Algeria, ardhi ya mujahidina na mashahidi milioni moja?! Je mnafikiri wangesimama kwenye Bahasha ya Gaza, au wangeendelea na safari ya kuelekea Al Quds ili kusafisha aibu ya usaliti wake katika miaka yote iliyopita?!
Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi katika Majeshi ya Ummah!
Mnajua kwa yakini ya kwamba mustakbali ni wa Dini hii, na mnajua kwamba Mwenyezi Mungu anawanusuru wanaomnusuru Yeye, na anawabadilisha wale wanaopuuza kuinusuru Dini yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]
“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Muhammad: 38].
Kwa nini hamchukui hatua ya kufikia utukufu huu mkubwa, na kumnusuru Mola wenu Mlezi na kuwa Answar wapya wa Dini hii, kama walivyokuwa watetezi (Answar) wa Aws na Khazraj?! Amueni, zigeuzeni meza watawala wenu, na muipe Nusrah (msaada) yenu Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itawakomboa mateka na Masra (Msikiti wa Al Aqsa) na kulipiza kisasi cha damu ya mashahidi, sio tu mashahidi wa Gaza waliouawa mikononi mwa Mayahudi, bali pia wale waliouawa huko nyuma nchini Algeria mikononi mwa Wazungu na Wafaransa. Tokeni kwa baraka za Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anapotaka kuwanusuru waja wake na vipenzi vyake, hupeleka kheri hii kwa wanaostahiki, basi kuweni kaumu yake na watu wake.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |