Jumanne, 22 Safar 1446 | 2024/08/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  15 Safar 1446 Na: H 1446 / 013
M.  Jumanne, 20 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Damu za Waislamu zinamwagika huku watawala wao wakishuhudia na hakuna suluhu!
(Imetafsiriwa)

Umbile la Kiyahudi linaendeleza uvamizi wake dhidi ya watu wa Palestina na linaendelea na jinai zake mbele ya masikio na macho ya walimwengu, bila kuzuiwa na azimio au hukumu yoyote ya Umoja wa Mataifa kutoka Mahakama ya Kimataifa. Idadi ya mashahidi waliohesabiwa imezidi 40,000, na pengine idadi sawia bado wamenaswa chini ya vifusi. Idadi ya waliojeruhiwa inakaribia 100,000, huku wale waliosalia wakiwa hai wanateseka sana kutokana na njaa. Matukio ya kila siku ya mateso, kuhama, uharibifu, njaa, magonjwa, kuchomwa moto, na kuhangaishwa ni karibu kupita maelezo.

Vita hivi sasa vimeingia mwezi wake wa kumi, bila dalili za uvamizi huu wa kikatili kuisha au mauaji haya ya kila siku ya watoto wasio na hatia, wanawake na wazee kukoma. Umbile hilo linahalalisha mauaji yake kila wakati kwa uwongo wa wazi na udanganyifu. Imedhihirika kwa kila mtazamaji kwamba umbile hili nyakuzi halizuiwi na mazungumzo, wala kwa maneno ya kulaani, wala vitisho havifanyi kazi dhidi yake. Tangu kuundwa kwake na Waingereza wahalifu na kusaidiwa na washirika, umbile hili, kama ilivyoelezwa na Mwenyezi katika Qur'an Tukufu, ni taifa la udanganyifu ambalo halitimizi makubaliano au kuheshimu amana yoyote. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[أَوَكُلَّمَا عَاهَدُواْ عَهْداً نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم بَلْ أَكْثَرُهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ]

“Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.” [Surat Al-Baqara:100]. Na Yeye (swt) amesema:

[الَّذِينَ عَاهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِي كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لاَ يَتَّقُونَ]

“Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara, wala hawamchi Mungu.” [Surat Al-Anfal:56].

Hili limedhihirika kwa wote na halihitaji uthibitisho. Kila mtu mwenye akili timamu, na hata watoto wa Waislamu, wanaelewa na kutambua hili.

Ushirikiano wa watawala wa nchi za Waislamu unajulikana sana, iwe ni nchi jirani kama Jordan, Syria, Lebanon, Misri na Saudi Arabia, au nchi nyingine za Kiislamu. Kimya chao, kinaodhihirisha uoga na utiifu wao, imefichua hali yao ya kweli. Wengine wanatamani hata vita viishe kwa kushindwa Mujahidina, ushindi kwa Mayahudi, na funzo kwa wengine ili asije yeyote akasubutu tena kufikiria Jihad. Wanataka kila mtu akubali masuluhisho yaliyowekwa juu yao na dola za Magharibi, iwe ni suluhisho la dola mbili, kuhamishwa kwenda nchi jirani kama nchi badali, fidia, au masuluhisho mengine ya kisiasa yenye lengo la kulihifadhi umbile hilo kilema na kuendelea kuwadhoofisha Waislamu huku wakidumisha migawanyiko ulioundwa na mipaka ya Sykes-Picot.

Hapa tunauliza, hasa kwa kuzingatia taharuki iliyopo katika eneo hili baada ya umbile hilo kutekeleza mfululizo wa mauaji ya kisiasa katika miji mikuu ya nchi za Kiislamu, Damascus, Beirut na Tehran, ambayo yaligharimu maisha ya watu mashuhuri. Mayahudi hawangesubutu kufanya hivyo kwa ushupavu kama huo kama si ulaji njama na ushirikiano na vibaraka na majasusi katika nchi hizo. Tunashangaa kuhusu majibu yanayotarajiwa, hasa baada ya viongozi wa nchi hizi kupaza sauti zao kwa vitisho na maonyo!

Iran na chama chake nchini Lebanon hapo awali zilitishia kwamba jibu litakuwa kali na la kuzuia, na kumfanya adui kujutia hatua yake, kufuatia shambulizi la umbile la Kiyahudi kwenye ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus, na kuua Wairani saba akiwemo kamanda wa Kikosi cha Quds. Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi. Vile vile, baada ya kuuawa Sheikh Al-Arouri na wenzake katika viunga vya kusini mwa Beirut, Iran na chama chake nchini Lebanon iliapa jibu kali na la kuzuia. Walakini, jibu lilikuwa dhaifu na la kuchekesha! Mkuu wa Majeshi ya Iran, Sardar Bagheri, alisema kuwa Iran ilituma ujumbe kwa Marekani kupitia ubalozi wa Uswisi, na kuonya kwamba ikiwa Marekani itashirikiana na umbile la Kiyahudi katika hatua zake za baadaye, kambi za Marekani “hazitakuwa salama” na zitakuwa hatarini! Wakati huo, ushirikiano wa Marekani katika majibu ulikuwa wazi, kwani ilizuia droni kwenye anga ya Jordan kutoka kwa besi za Amerika huko, na hivyo kuzuia majibu. Hakuna kombora au ndege isiyo na rubani iliyofika kwenye chombo, na kuiacha salama na salama. Rais Joe Biden hata alimwambia Waziri Mkuu wa chombo hicho, Benjamin Netanyahu, wakati wa simu, “Unapaswa kuzingatia usiku wa leo ushindi kwa sababu tathmini ya sasa ya Marekani ni kwamba mashambulizi ya Iran hayakufanikiwa kwa kiasi kikubwa na yalionyesha uwezo wa juu wa kijeshi wa Israeli.” Kambi za Wamarekani, ambazo ni umbali mfupi tu kutoka Iran nchini Qatar, Iraq, au Jordan, zimesalia salama, na hakuna vitisho vyovyote vilivyotekelezwa!

Mullah wameitawala Iran kwa zaidi ya miaka 45, mara kwa mara wakiitaja Amerika kama adui mkubwa na kutishia kufuta muundo wa Kiyahudi. Walakini, ushirikiano wao na Marekani nchini Afghanistan, Iraq, na baadaye Yemen umefichua uaminifu wao kwa Marekani, na kufichua kama mshirika wake na chombo cha kutishia Ghuba na kuzidisha migawanyiko ya kidini kati ya Waislamu.

Je, ni mara ngapi tumesikia kutoka kwa Bw. Hassan Nasrallah kwamba chama kinamiliki wanajeshi na vifaa vinavyoweza kulifuta umbile hilo kwenye ramani ikitaka au ikiwa umbile hilo litaanzisha vita dhidi ya Lebanon? Licha ya vitisho vyake, ndege zinaendelea kuruka juu ya Beirut, zikionya na kutishia, zikiwaua viongozi wa ngazi za juu wa chama mmoja baada ya mwengine katika mashambulizi yaliyowalenga, kama ilivyotokea kwa mauaji ya Fuad Shukr! Msimamo huu dhaifu na vitisho vitupu ndivyo vimelipa ujasiri umbile la Kiyahudi wa kuendelea na mauaji yake, hata kumuua Ismail Haniyeh huku akiwa mwenyeji wa Iran katikati ya Tehran. Sasa, zaidi ya wiki tatu zimepita, na wengine wangali bado wanasubiri majibu madhubuti, wakitazamia shambulizi kubwa kutoka kwa pande za upinzani ili kuliondoa umbile hilo na kulipiza kisasi uchokozi wa moja kwa moja dhidi ya Iran na chama chake nchini Lebanon!

Ukweli Ambao Lazima Ueleweke ili Kuelewa Matukio ya Sasa:

- Mfumo wa kimataifa leo ni wa kikoloni, unaoongozwa na Marekani. Taasisi na mashirika yote ya kimataifa ima yanadhibitiwa au kusukumwa na mfumo huu wa kikoloni, ambao unafanya njama za kuwadhoofisha Waislamu na kuzuia mwamko na umoja wao.

- Watawala hawa wanakula njama na kushirikiana kuzima moto wa Jihad, kulinda maslahi ya Magharibi, na kuyaweka sawa na maslahi yao binafsi ili kulinda viti vyao vya enzi na madaraka. Maamuzi yao yanawiana na utashi wa mfumo wa kikoloni, na wanafanya kazi kudumisha ushawishi na udhibiti wake.

- Watawala wote hawa hawajali maslahi ya Waislamu na wanahofia kwamba vita vinaweza kuendelea au kudumu zaidi, na hivyo kufanya iwe vigumu kudhibiti hisia za wanachama wanyoofu wa Umma, wanaochemka kwa hasira na tayari kulipiza kisasi dhidi yao na kulipindua umbile hilo.

- Imedhihirika kuwa umbile hilo ni dhaifu na kwamba Ummah hakika una uwezo wa kuling'oa chini ya uongozi wa kweli. Watawala wanatambua kwamba vuguvugu hili litaanza kwa kuwaondoa wao, kwani wao ndio kikwazo cha ukombozi kutoka kwa dhulma, udhalimu, uchokozi na uvamizi.

- Vitisho na maonyo hayabadili hali hiyo; zinafichua tu udhaifu na kulipa umbile hilo mkono wa juu, wakiliruhusu kuendelea na uchokozi wake, wakihakikisha kwamba hakuna mtu yeyote atakayelipiza kisasi dhidi ya uchokozi wake au kulipiza kisasi kwa makosa na kiburi chake.

- Kugeukia kile kinachoitwa uhalali wa kimataifa na sheria ya kimataifa ni upuuzi tu, uhadaifu na udanganyifu wa watu, ambao hauna faida yoyote. Ushahidi wa hili ni mwingi mno kuweza kuhesabiwa.

Na baada ya hayo: Ni kiasi gani cha damu kitamwagika, na ni watu wangapi watapoteza maisha kabla ya watawala hawa kuhamisha majeshi yao kuwanusuru wanyonge?! Jibu la hili lipo katika maneno ya Mwenyezi Mungu, Al-Hakeem, katika Wahyi Wake Uliokatikiwa:

[وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَكِن كَرِهَ اللهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ]

“Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa!” [Surat At-Tawba:46].

Huu ndio msimamo wa watawala wote wa ardhi za Waislamu, hususan zile nchi zinazomiliki kikweli nguvu za kisiasa na kijeshi, kama vile Uturuki, Iran, Pakistan na Misri. Badala ya kuweka kizuizi kwa umbile hilo, wanalipatia chakula na kufungua milango kwa ajili ya unafuu wake, kama vile Jordan na Dola za Ghuba. Kwa hivyo, haishangazi kuona kukatishwa tamaa na usaliti kutoka kwa vyombo hivi dhaifu, kukimbilia mazungumzo kwa matumaini kwamba ahadi za Marekani na umbile hilo za usitishaji vita na kuruhusu chakula na misaada ya kibinadamu kuingia Gaza zitatimizwa.

Wanaonekana kuridhika na kudumisha hali ilivyo, wakiamini kwamba mapigano ya kutosha yametokea. Ni kana kwamba wanajaribu kuwahadaa watu kudhani kwamba wamepata ushindi kwa vitisho, na kwamba hasara ya kiuchumi inayolipata umbile hilo kutokana na vitisho pekee inatosha kulidhoofisha au kulishinda. Huu ni udanganyifu mtupu wa kisiasa na tusi kwa akili za watu.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu