Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Jumada I 1446 Na: H 1446 / 044
M.  Jumatatu, 04 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utawala wa Sisi Hautaweza Kuficha Usaidizi wake kwa Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Vyombo vingi vya habari vimefichua kuwa Misri iliiruhusu meli ya MV Kathrin, ambayo imebeba vilipuzi na silaha iliyokuwa ikielekea katika umbile la Kiyahudi, kutia nanga na kupakua katika bandari ya Alexandria, jambo ambalo lilisababisha shirika la Amnesty International kusema kuwa “Misri haipaswi kusaidia au kuwezesha uhamishaji haramu wa shehena ya vilipuzi kuelekea ‘Israel’.” Nataša Posel, mkuu wa tawi la Amnesty International nchini Slovenia, alikuwa ameonya hapo awali, akisema: “Shehena hatari inayoaminika kuwa ndani ya MV Kathrin lazima isifikie ‘Israel’ kwani kuna hatari ya wazi kwamba itachangia uanzishaji wa uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Palestina.”

Katika jaribio lililofeli la kukataa kutoa msaada wa kijeshi, serikali ya Misri ilitoa taarifa rasmi ikikana kutoa msaada wowote wa kijeshi kwa umbile hilo. Taarifa hiyo ni ya uwongo wazi na haiwezi kuaminiwa, kwani kutia nanga kwa meli yenyewe ni ushahidi wa ushirikiano na usaidizi.

Meli hiyo ilisafiri na shehena yake kutoka bandari ya Vietnam ya Hai Phong mnamo Julai 21. Mnamo tarehe 24 Agosti, mamlaka ya Namibia ilibatilisha kibali cha awali cha meli kuingia bandari kuu ya Namibia, ikitoa taarifa kutoka kwa waendesha meli hiyo kwamba vilipuzi vilivyokuwa ndani ya meli hiyo vilikuwa vya umbile la Kiyahudi. Mnamo arehe 31 Agosti, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Francesca Albanese, alisema kuwa meli ya MV Kathrin ilikuwa na makontena nane ya vilipuzi (vilivyoripotiwa kuwa viungo muhimu vya mabomu ya angani na roketi) vinavyotumiwa na umbile la Kiyahudi dhidi ya Wapalestina. Albanese alitoa wito kwa dola zengine kuzuia meli hiyo kutia nanga katika bandari zao.

Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Ulaya hapo awali kiliripoti kuwa meli hiyo imezuiwa kutia nanga katika bandari kadhaa za Afrika na Mediterania, zikiwemo Angola, Slovenia, Montenegro na Malta. Mamlaka za Ureno zilikuwa zimeitaka meli hiyo kubadilisha bendera yake kutoka ya Ureno hadi Ujerumani kabla ya kuendelea na safari yake. Katika maelezo ya ziada, kituo hicho kilionyesha katika ombi lake kwamba shehena hii ya vilipuzi inaweza kutumika katika utengenezaji wa risasi katika vita vinavyoendelea huko Gaza, ambavyo vinaweza kusababisha kutekelezwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kwa mujibu wa ripoti, shehena hiyo inaelekea kwenye kampuni ya Elbit Systems, mojawapo ya makampuni makubwa katika umbile la Kiyahudi katika sekta ya kusambaza vifaa vya kijeshi.

Ushahidi huu unaonyesha uongo wa mamlaka za Misri ambazo zinadai kuwa shehena hiyo ilikusudiwa kwa ajili ya Wizara ya Uzalishaji wa Kijeshi ya Misri.

Kwa hiyo, kuruhusu tu meli hiyo kutia nanga bila kujali sababu, bila shaka inaashiria kuwa Misri inashirikiana na umbile la Kiyahudi na kuiunga mkono katika kuwaangamiza watu wa Gaza. Hivyo, inashiriki moja kwa moja katika mauaji ya watoto na wanawake na ubomoaji wa nyumba. Jinai ambazo historia ya kisasa haijashuhudia chochote mithili yake.

Utawala wa Misri haukutilia maanani maonyo na tahadhari za nchi nyingi zinazoizuia meli hiyo kutia nanga katika bandari zao, na ukairuhusu kwa ufidhuli na kiburi, hivyo kukaidi hisia za Waislamu, hasira za Ummah, na hata hasira za watu wengi waheshimiwa duniani ambao wana uchungu kwa kile wanachoona juu ya jinai za mauaji ya halaiki na vita vya kikatili nchini Palestina. Kwa kufanya hivyo, inathibitisha mara kwa mara njama na uungaji mkono wake kwa umbile hilo poraji, na kujitenga kwake na Ummah usiokubali khiyana hizi na usiokubali udhalilishaji na unyonge huu.

Kwa upande mwingine, Mamlaka ya Mkondo wa Suez ilithibitisha katika taarifa rasmi “kujitolea kwake kuruhusu manuari kuvuka mkondo huo pasi na ubaguzi kwa msingi wa utaifa wa meli hiyo, kwa mujibu wa Mkataba wa Konstantinopoli, ambao unasisitiza uhuru wa urambazaji.” Kwa kufanya hivyo, inajaribu kujiondolea hatia kutokana na kuruhusu manuari zinazounga mkono moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja umbile la Kiyahudi kuvuka, na ikiwa inahalalisha jambo hilo kwa msingi wa makubaliano ya kimataifa, pia inafanya kazi kwa namna ambayo inagongana na wajibu wake chini ya makubaliano mengine ya kimataifa, yaani Mikataba ya Geneva, ambayo inaweka masharti ya kukataza uhamishaji wa zana za kijeshi zinazohusika na uhalifu dhidi ya raia, na kufanya kazi kuzuia uhamishaji wote kama huo.

Sio tu utawala nchini Misri unaochangia kuunga mkono umbile la Kiyahudi katika vita vyake dhidi ya watoto na wanawake wasio na ulinzi wa Palestina. Badala yake, nchi zinazozunguka na zilizo nje ya eneo linaloizunguka Palestina zinaendelea kutoa msaada wa kibiashara kwa siri na dhahiri, kama ilivyo kwa ukanda wa ardhi unaovuka nchi za Kiarabu unaoanzia Ghuba ya Uarabuni hadi Palestina inayokaliwa kwa mabavu ili kupitisha chakula na vifaa vya viwandani kwa umbile la Kiyahudi, pamoja na biashara inayonawiri kati yake na Uturuki.

Enyi wana wa Ummah mtukufu wa Kiislamu, mnaopuma kwa wema: Msijiwekee kikomo kwa wito wa kususia bidhaa za umbile la Kiyahudi au kampuni zinazoliunga mkono, bali lazima mufanye kazi kwa nguvu zenu zote kukata kila mkono unaolisaidia umbile hili la kihalifu na kulipatia msaada katika jinai zake. Zaidi ya yote, ni lazima mushirikiane na Hizb ut Tahrir kuwapindua watawala hawa vibaraka na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo itawang'oa Mayahudi na umbile lao kutoka katika ardhi iliyobarikiwa na kuitakasa kutokana nao.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu