Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 5 Jumada I 1446 | Na: H 1446 / 045 |
M. Alhamisi, 07 Novemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wito wa Kushiriki katika Chaguzi za Kimagharibi ni Wito wa Kujioanisha ndani ya Mujtamaa za Kikafiri za Kimagharibi, na Kuzuia Ulinganizi wa Ujumbe wa Uislamu kwa Ulimwengu Mzima
(Imetafsiriwa)
Katika kila uchaguzi unaofanyika katika nchi za Magharibi, iwe ni uchaguzi wa urais au ubunge, wanaharakati wengi katika jamii za Kiislamu katika nchi za Magharibi hupaza sauti zao wakitaka kushiriki katika chaguzi za ndani katika nchi hizo. Wanaharakati hao wakiwemo masheikh na maafisa wa vituo vya Kiislamu wanafanya kile kinachofanana na kampeni za uchaguzi wakiitaka jamii kukipigia kura chama au mgombea fulani. Hawatoi wito wa kuacha kupiga kura, hata kama wagombea hawapendi “masheikh” hawa, wakisisitiza ulazima wa kushiriki katika uchaguzi, na kupiga kura, hata kama mpiga kura Muislamu hatajaza chochote katika karatasi yake ya kupigia kura. “Masheikh” hawa wanasema kwamba mujarrad tu wa kushiriki katika uchaguzi ni wajibu wa kidini na “kitaifa,” kama wanavyodai. Hii inatufanya tuamini kwamba walengwa wa wito huu ni Waislamu wenyewe, sio kura zao, na kiwango cha ushawishi wao. Wamefikia hatua ya kudai kuwa jamii za Kiislamu, hata kama idadi yao ni ndogo, huweka uwiano katika kuamua matokeo ya uchaguzi, wakati mwingine. Kama mengi yalivyoelezwa katika ripoti ya udanganyifu iliyochapishwa na Al Jazeera ya Kiarabu wakati wa uchaguzi wa Marekani, chini ya kichwa “Waislamu huamua matokeo ya uchaguzi katika majimbo saba.” Ingawa ripoti hiyo inasema kwamba “Waislamu nchini Marekani ni watu wachache kwa kulinganishwa na watu milioni 3.5 hadi 4, kati ya watu milioni 336,” iliongeza kwamba “ushawishi wao katika uchaguzi wa urais unatarajiwa kuwa mkubwa, hasa katika majimbo yenye maamuzi ya Pennsylvania, Michigan, Arizona, Nevada, Georgia, Carolina Kaskazini, na Wisconsin, ambayo ni majimbo ambayo uungaji mkono wa vyama viwili vikuu, Republican na Democratic, uko karibu sana.”
Kwanza: Waislamu wanashangazwa na wito wa namna hii katika nchi za Magharibi zinazotawala kinyume na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), na zina uadui na Uislamu na Waislamu, ndani na nje ya nchi. Hatuoni hata mfano (shubha) wa dalili ya Kisharia kwa fatwa hizi, ambazo zinagongana na misingi (usul) ya fiqh ya Kiislamu. Miongoni mwa kanuni hizo za msingi ni kwamba uchaguzi ni mkataba wa uwakilishi (wakala) kati ya mpiga kura na mteule. Basi vipi “masheikh” hawa wanaweza kumruhusu Muislamu kumkabidhi kafiri kutawala kinyume na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) akitawala tu kwa maslahi ya nchi yake pekee?! Wanawezaje kuruhusu hili ilhali hukmu ya kafir inalingana na katiba, sheria, na sera za nchi yake, ambazo daima zinaugharimu Umma wa Kiislamu na maslahi yake popote pale walipo?! Ajabu zaidi ni kwamba ukiwakumbusha juu ya dhana hii, wanaipuuza na kuhalalisha madai yao kwa kusema, “Tunachagua la hafifu katika maovu mawili,” au kama alivyosema mmoja wao, kwamba watu wana khiari kati ya “Abu Jahl na mbeba kuni,” huku akitoa wito kwa mgombea wa tatu asiyejulikana ambaye hana nafasi katika uchaguzi. La ajabu pia ni kwamba “masheikh” hawa wanapotumia kile wanachofikiria kuwa ni hukmu ya Shariah, kanuni ya “hafifu ya maovu mawili,” wanapuuza kwamba baadhi ya maulamaa, walioitabanni kanuni (qaida) hii, waliweka masharti kwamba Muislamu lazima alazimishwe kwa nguvu katika moja ya maovu mawili. Haijuzu kwake kuchagua baina ya maovu mawili hali ya kuwa amestarehe, kumaanisha kuwa hajatenzwa nguvu au kulazimishwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, hatuoni hoja ya Kishariah ya kutoa wito wa ushiriki katika chaguzi za Kimagharibi, hata ndani ya kutabanni kwao qaida hii. Tunatoa wito kwa Waislamu wote wanaoishi Magharibi, wakiongozwa na “masheikh” na maafisa wa vituo vya Kiislamu, kumcha Mwenyezi Mungu (swt). Tunatoa wito kwao kutowapa uwakilishi wale wanaowatawala kwa ukafiri, na kuwa mawakala katika kutekeleza miradi ya Magharibi ya kupanga njama dhidi ya Waislamu, na kuwaua kote duniani. Tunatoa wito kwao kutosikiliza fatwa zinazopingana na sheria ya Kiislamu ya Mwenyezi Mungu (swt). Tunawaomba wasitegemee ulimwengu na starehe za maisha, na wasitishwe na sera ya kindoto ya karoti na fimbo. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا]
“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [Surah An-Nisaa 4:60].
Pili: Kushiriki katika chaguzi za Kimagharibi ni kuukubali mfumo wa kisekula wa kikafiri. Ni wajibu wa Kishariah kwa Waislamu waishio Magharibi kuwalingania Wamagharibi kwenye Uislamu mpana, kuubeba kama ujumbe wa rehma kwa wanadamu wote, na kufanya Dawah kwa Uislamu wote, na sio sehemu yake tu, ya ibada za mtu binafsi pekee. Dawah kwa Uislamu lazima iwe ni Dawah kwa mfumo kamili wa maisha, utawala, uchumi, na nyanja zote za maisha. Hii ndiyo maana ya Dawah kwa Uislamu, hasa kwa vile nchi za Magharibi zinaishi katika hali ya kuporomoka kwa hadhara. Nchi za Magharibi zinahitaji sana badali ya kihadhara ambayo itawaokoa Wamagharibi kutokana na ufisadi wa hadhara ya kisekula ambayo imewafanya watu wa Magharibi kuwa duni. Hadhara ya Magharibi imekuwa laana ndani ya nchi, na laana kwa watu wa dunia, ukiwemo Umma wa Kiislamu. Yaani, Dawah kwa Uislamu lazima iwe ni Dawah kwa Uislamu mtukufu kuchukua nafasi ya hadhara ya Magharibi, pamoja na mfumo wake unaoegemezwa kwenye dhulma za usekula. Hili kimsingi lawahitaji Waislamu wa nchi za Magharibi kutangaza kutouamini kwao mfumo wa kisekula, na kuuwasilisha Uislamu kama hadhara badali kwa jamii ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hilo kwa wagombea wa nyadhifa za kisiasa, na wasimchague yeyote kati yao, hata awadanganye na awahadae watu kiasi gani kuwa atawatumikia wao na maslahi yao! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لاَ يَسْمَعُ بِي أحد من هذه الأمة لا يَهُودِيٌّ، وَلاَ نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كانَ مِنْ أَصْحَابِ النار»
“Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake, hakuna yeyote atakayesikia uwepo wangu katika Umma huu, sio Myahudi wala Mnaswara, kisha akafa na hali hakuamini yale niliyotumilizwa nayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.” [Ahmad]
Tatu: Muungano wa jamii za Waislamu wanaoishi ng’ambo katika nchi za Magharibi, chini ya mwavuli wa Kiislamu, na kubeba kwao Uislamu kama ujumbe wa mwongozo na rehma, ndiko kunakowafanya kuchangia vyema katika jamii za Magharibi. Kuulingania Uislamu ni ujumbe wa mbinguni kwa nchi za Magharibi, hasa kwa watu wanaokandamizwa na mabepari wachache, wanaowatawala kwa manufaa ya kifedha, kama wamiliki wa makampuni makubwa ya mabara tofauti tofauti. Kuwafikishia ujumbe huo kwao ni wajibu wa Shariah, na kutoshiriki katika mfumo wao wa maisha, jambo ambalo limewafanya kuwa wadhalilifu na kuwaletea Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Muungano wa Waislamu pia unawalinda dhidi ya njama zozote zinazofanywa na wale wanaokula njama dhidi yao na Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,
«عليكَ بالجماعةِ فإنَّما يأكلُ الذئبُ منَ الغنمِ القاصيةَ»
“Shikamaneni na mkusanyiko (Jama’a), kwani hakika mbwa mwitu humla tu kondoo aliye peke yake.” [Imepokewa na Ahmad]. Kwa hivyo wakati Waislamu milioni kumi nchini Amerika, kwa mfano, wana mwakilishi wao, na kutoka kwao, uwakilishi huu unawafanya kuwa nguvu ambayo haiwezi kupuuzwa. Kisha, haki zao haziwezi kupuuzwa, haswa ikiwa matakwa yao ni halali Kisharia na ya haki. Hii ni kama vile kudai haki zao za kisheria kama raia, iwe wanashiriki katika uchaguzi au la. Hili pia ni kama vile takwa lao la kutolipatia umbile la Kiyahudi silaha wanazotumia kuwaua ndugu zetu mjini Gaza.
Nne: Tunawalingania Waislamu wa nchi za Magharibi kuwa mabalozi wa kweli wa Uislamu na Waislamu. Hebu wasifu wa Maswahaba waliohamia Habasha, akiwemo Ja’far ibn Abi Talib (ra) na uwe chanzo cha msukumo kwao. Wasijioanishe na kujiyeyusha ndani ya mujtamaa za Kimagharibi, wakitekeleza njia za kisiasa za Kimagharibi zinazowanyima sifa ya kubeba Dawah ambayo ni ya watu wote. Tunawaomba wapambanuliwe na wachangie kwa njia chanya katika jamii hizo, kwa kufanya kazi kwa bidii kuwatoa watu katika ibada ya viongozi wa pesa, na kuingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa makundi. Hii ni kupitia Dawah kwa Uislamu kama imani na mfumo mpana wa maisha kwa nyanja zote za maisha. Kwa njia hii watazisafisha dhamiri zao kwa watu wa nchi wanayoishi miongoni mwao, hivyo hawatawajibishwa Siku ya Kiyama kwa kushindwa kwao kuwafikishia Ujumbe. Kwa namna hii watamridhisha Mola wao Mlezi kwa kubeba Ujumbe Wake, kwa namna inayompendeza. Kwa njia hii watajilinda wao wenyewe na vizazi vijavyo kutokana na kuyumba katika maisha ya ukafiri na njia zake. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[ادْعُ إِلَى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ]
“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.” [Surah An-Nahl 16:125].
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |