Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  14 Jumada I 1446 Na: H 1446 / 048
M.  Jumamosi, 16 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala wa Iran ni Uhalisia tu wa Sauti na Maonyesho ya Fataki Hawana Uhusiano Wowote na Ushindi au Ukombozi
(Imetafsiriwa)

Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Meja Jenerali Hossein Salami, alithibitisha katika ufunguzi wa mazoezi ya mapambano ya usalama ya “Nasrallah” kwamba “umbile la Kizayuni linakosea ikiwa linadhani kuwa Hizbullah itatoka nje ya uwanja kwa kuwauwa viongozi wake,” na kubainisha kuwa “chama hicho ni vuguvugu kubwa ambalo haliwezi kuzimwa wala kumalizwa.” Akalitisha umbile la Kiyahudi kwa kusema: “Leo tuna nyinyi machoni mwetu, na tutapigana mpaka mwisho, na hatutakuruhusuni kudhibiti hatma ya Waislamu, na tutalipiza kisasi, nanyi mtapata pigo chungu, na lazima musubiri.”

Kwa hivyo, viongozi wa Iran hawaoni aibu kukariri misemo ya vitisho kwa umbile nyakuzi, halifu la Kiyahudi, bila ya kuona hatua yoyote ya kweli au harakati halisi kutoka kwao kwa kiwango cha uhalifu na hali hiyo.

Imedhihirika kwa kila mwenye macho na utambuzi kwamba wao ni waongo na wadanganyifu, kwani waliwaacha Mayahudi kuangamiza Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi ukawa ni mrundo wa vifusi, katika vita vya kikatili vilivyogharimu maisha ya mashahidi zaidi ya 146,000 na majeruhi, wengi wao watoto na wanawake, na zaidi ya elfu 10 wamepotea, na hawakuwa na uungwana wa kuwanusuru, lakini waliwaacha wakabiliane na Mayahudi, Amerika, Uingereza, Ujerumani na nchi nyingine za kikoloni na zenye kiburi kwa vifua wazi.

Kisha umbile la Kiyahudi likaanza uvamizi wake wa kikatili dhidi ya Lebanon na Dahieh, kusini mwa Beirut, ngome ya chama cha Iran nchini Lebanon, na kuwauwa viongozi wake wa daraja la kwanza na la pili. Kwa hivyo, Iran iliiacha ili kukabiliana na jeshi la Kiyahudi, jeshi lake la anga, mabomu yake ya moto yenye kupenya, na makombora yake hatari ya kuongozwa. Haikuwanusuru, bali iliwaacha wakabiliane na hatma yao peke yao, katika tukio lililojaa udhalilifu na kufeli.

Sasa, viongozi wa Iran wanaendelea na hotuba zao kali na vitisho vitupu, kana kwamba ni jambo tu la maneno, na hata wanapotishia, mvuke na ngurumo, vitendo vyao vinaishia kwenye maonyesho ambayo yanabeba ujumbe ambao hautamuumiza adui au kukomesha uvamizi.

Palestina na Lebanon zina haki kubwa juu ya Iran, kwani Palestina ina haki ya kukusanywa majeshi kwa ajili yake na ndege zao, makombora, droni na vifaru; ili kupigana na umbile la Kiyahudi katika vita vya kweli ambavyo vitaling'oa, na si pigo kali ambalo linaweza kuliumiza lakini litalibakisha na sio kuliondoa, kana kwamba tuko kwenye uwanja wa mieleka katika mechi ya michezo huo!

Ama Lebanon, ina haki ya kukusanywa majeshi ili kuinusuru, kuushinda Uvamizi na kulipiza kisasi cha damu ya mashahidi wake na waliojeruhiwa, sio sherehe na hotuba, au hata kwa msaada wa kijeshi wa tahadhari kutoka nyuma ya pazia.

Kila mtu aliye huru na mwenye heshima katika majeshi ya Waislamu ni lazima ajiunge na msafara wa wafanyikazi waaminifu ili kuwaondoa watawala kutoka kwenye viti vyao vya utawala na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kuuunganisha Ummah na kuandamana na majeshi yake kuelekea Palestina na Lebanon ili kuzitakasa kutoka na Mayahudi. Vyenginevyo, Ummah wetu utaendelea kupata maumivu, mauaji na maangamivu.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu