Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  9 Jumada I 1446 Na: H 1446 / 046
M.  Jumatatu, 11 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ushirikiano wa Mamlaka za Uholanzi pamoja na Watu Ovyo wa Mayahudi Umesalia Kuvama ndani ya Kumbukumbu ya Umma...
(Imetafsiriwa)

Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti vitendo vya kundi la wachochezi wa Kiyahudi wakati na baada ya mechi ya kandanda, kujihusisha na uchokozi dhidi ya Waislamu kuhusiana na kadhia kuu ya Umma wa Kiislamu, kadhia ya Palestina. Vitendo hivi viliibua hisia za kimaumbile kutoka kwa Waislamu wa mataifa mbalimbali na kutoka kwa raia waheshimiwa wa Uholanzi wenyewe. Hata hivyo, kinachodhihirika ni kimya cha mamlaka za Uholanzi kuhusiana na chokochoko za wachochezi hao, ikifuatiwa na vyombo vyao vya usalama kukabiliana na waandamanaji wanaopinga chokochoko hizi na kuwakamata wengi wao!

Katika muktadha wa majibu, misimamo fulani ya fedheha inafaa kutajwa. Tukianza na kauli ya Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, ambaye alilaani kile alichokitaja kuwa “mashambulizi dhidi ya Mayahudi.” Vile vile, Balozi wa Marekani katika umbile la Kiyahudi alishutumu kile alichokitaja kama “mashambulizi ya kutisha” dhidi ya Mayahudi, akipuuza kiurahisi kwamba ni wao walioanzisha uchochezi na vitendo vya ghasia. Jambo la kuchukiza vile vile ni matamshi ya Mjumbe Maalum wa Marekani wa Ufuatiliaji na Kupambana na Chuki dhidi ya Mayahudi, ambaye alionyesha kushtushwa na kile alichoeleza kuwa mashambulizi yaliyotokea Amsterdam. Rais wa Tume ya Muungano wa Ulaya pia alionyesha kukasirishwa na kile alichokiita “mashambulizi ya kuchukiza” yaliyolenga Mayahudi jijini Amsterdam. Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya, alisisitiza ahadi yake ya kupambana na chuki dhidi ya Mayahudi, kama alivyodai. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alitaja matukio hayo kutoka Amsterdam kuwa “ya kutisha na ya aibu sana kwa Ulaya.” Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwa upande wake, alitumia fursa hiyo kukumbuka nyakati za giza zaidi katika historia, akimaanisha kile alichokiita ghasia dhidi ya mashabiki wa soka wa Kiyahudi.

Haya yote—kwa tukio lolote au pasi kwa tukio—yanathibitisha uadui wao dhidi ya Uislamu na Waislamu, bila ya haki wanaunga mkono wahalifu wavamizi ambao wameteka ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wakipuuza kwa urahisi—au wakipuuza kwa makusudi—uhalifu wa Mayahudi nchini Palestina na kwengineko, uhalifu unaotendwa dhidi ya watoto, wanawake na wazee. Umbile lao katili iliundwa juu ya mafuvu ya Waislamu, kuanzia Nakba ya 1948 na kuendelea na ukatili wao wa hivi karibuni huko Gaza, Lebanon, Syria, Iraq, Yemen na Iran.

Ingawa tunapongeza misimamo ya watu wengi waheshimika na walio huru barani Ulaya ambao wamesimama dhidi ya uhalifu wa hivi karibuni wa umbile la Kiyahudi huko Gaza na chokochoko za wachochezi wa Kiyahudi, ujumbe wetu unaelekezwa kwa serikali na mamlaka barani Ulaya na kwengineko - haswa zile ambazo ziliunga mkono misukosuko ya uchafu wa Kiyahudi, zikiegemea upande wa umbile la Kiyahudi katika unyakuzi wake wa ardhi za Waislamu, na zilichangia kuundwa kwa umbile hilo. Kwa yale mataifa yote ambayo yamesaidia mauaji na jinai zake, tunasema: ukatili wote huu umebakia kuvama ndani ya kumbukumbu ya Umma wa Kiislamu na hautasahaulika kamwe. Mataifa haya hayatakuwa na hadhi wala mapatano na Ummah wakati Khilafah ijayo, itakaposimamishwa hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka uwepo.

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu'ara:227].

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu