Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 9 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 083 |
M. Jumamosi, 08 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Majeshi ya Waislamu: Nani Atawakomesha Wapumbavu Hawa Wawili?!
(Imetafsiriwa)
Jana usiku, chaneli za satelaiti zilitangaza sherehe za mapokezi ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, pamoja na mkutano wa waandishi wa habari uliotangulia mazungumzo yao. Trump alionekana kama mcheshi akilenga kufurahisha watazamaji wanaomtazama, kwa kauli zake za kizembe kuhusu Ukanda wa Gaza, na nia yake ya kuwaondoa watu wake na kuweka udhibiti wa Amerika juu yake.
Hatutazungumza juu ya aibu iliyowapata watu wa Amerika kutokana na kauli za rais wao wa kinyago, na kuwafanya kuwa kicheko mbele ya ulimwengu wote, wala juu ya athari za viongozi wa ulimwengu na mawaziri wao wa mambo ya nje kupinga kauli hizi za kipuuzi, na kuzielezea kuwa ni kinyume na sheria za kimataifa, wala kwa kauli iliyotolewa na shirika la Amnesty International iliyoelezea matamshi ya Trump kuwa ya kipuuzi!
Bali, kinachotuhusu na kutuvutia zaidi hapa, na ambacho tutazungumzia, ni ummah wa Kiislamu uliolengwa unaokusudiwa na kauli hizi za kizembe. Je, upingaji wa dhahiri kutoka kwa watawala wake unatosha? Je, kushikamana kwao na sheria za kimataifa na kutozivunja kunatosha kusimama dhidi ya wapumbavu hawa wawili?!
Mwitikio wa kweli wa Umma wa Kiislamu katika muda wote wa historia umewekwa katika misimamo ya Mtume Muhammad (saw), na matendo ya watu watukufu kutoka miongoni mwa makhalifa na viongozi wa Ummah; kama vile msimamo wa Mtume (saw) kwa Banu Qaynuqa walipomshambulia mwanamke mmoja wa Kiislamu na kumuua Muislamu. Mtume (saw) alijibu kwa kulikusanya jeshi dhidi yao, kuwazingira, na hatimaye kuwafukuza kutoka mjini hadi Adhri'at. Vivyo hivyo ndivyo misimamo ya Harun al-Rashid, ambaye alimhutubia adui wa Ummah kama 'mtoto wa kafiri', akimaanisha kwamba jibu lilikuwa ni hatua ya kijeshi na jeshi ambalo mwazo wake uko kwa adui na mwisho wake uko kwa Khalifah, na kupelekea adui kunyenyekea na kurudi kwenye kulipa kodi. Msimamo mwingine ulikuwa ule wa Al-Mu’tasim, ambaye alipopokea ombi la msaada kutoka kwa mwanamke mmoja wa Kiislamu, hakutulia mpaka alipomlipizia kisasi na kuiteka Amuriyya. Na msimamo wa Salahuddin, ambaye aliunganisha Umma na majeshi yake na akaikomboa Palestina kutoka kwa Wapiganaji wa Msalaba, na msimamo wa Sultan Abdul Hamid II, aliyeihifadhi, pamoja na watu wengine watukufu wa Umma huu, Mwenyezi Mungu awarehemu wote.
Yaliyoikumba Gaza na watu wake kuhusiana na maangamizi na mauaji yamesababishwa na mashini ya jeshi la Kiyahudi ya Marekani, pamoja na hifadhi, ulinzi na usaidizi wa Marekani. Uharibifu na mauaji haya yasingetokea lau majeshi ya Waislamu yangejikusanya ili kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kukata uwepo wa Marekani kutoka katika ardhi zetu.
Enyi majeshi ya Waislamu:
Je, damu haijachemka katika mishipa yenu munapotazama uharibifu na mauaji huko Gaza, na kisha baadaye katika Ukingo wa Magharibi?!
Je! roho ya yule anayelingania haki haijakusisimsheni?! Je, hamjajawa na kiburi, mlipomwona mpumbavu Trump akimkaribisha mhalifu wa kivita Netanyahu kama shujaa, na mkasikia matamshi yake yanayouchokoza umma wenu ilhali nyinyi ni majeshi yake, nusra yake, na ngao yake ya ulinzi?!
Je, haujafika wakati wa nyinyi kuwang’oa watawala hawa vikaragosi, kuziondoa tawala zao za usaliti, kusimamisha utawala wa Uislamu, na kutetea heshima na adhama ya umma wenu? Wako wapi wanaume miongoni mwenu ambao hawalali chini ya dhulma, hawanyamazi mbele ya batili, na hawakubali kudhalilishwa katika dini yao na umma wao, katika ardhi zao na matukufu yao? Hii ni fursa yenu, kwa hivyo musiipoteze. Hii ni Hizb ut Tahrir, ambayo ina miliki ruwaza wazi ya kisiasa iliyoegemezwa juu ya Sharia, ikikulinganieni kuinusuru katika kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili Umma uinuke kama mtu mmoja dhidi ya hao madhalimu wawili na kuondosha minong’ono ya Shetani.
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |