Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 8 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 082 |
M. Ijumaa, 07 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Trump Aitishia Gaza kwa Uvamizi wa Moja kwa Moja na Kuwafukuza Watu Wake
(Imetafsiriwa)
Jioni ya Jumanne, 4 Februari 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza katika mkutano wake na Waziri Mkuu wa Kiyahudi kwamba "Wapalestina hawana chaguo zaidi ya kuondoka Ukanda wa Gaza. Nataka kuona Jordan na Misri zikipokea Wapalestina kutoka Gaza. Hakuna badali kwa wakaazi wa Gaza isipokuwa kuondoka." Aliongeza, "Jordan na Misri tayari zimekataa kuwapokea wakaazi kutoka Gaza, lakini baadhi ya watu wanakataa mambo isipokuwa hatimaye kukubaliana nayo."
Katika mkutano na waandishi wa habari, Trump alisema: "Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza, na tutausimamia vilevile. Ikibidi, tutafanya hivyo, tutakinyakua kipande hicho cha ardhi, tutakiimarisha, na kuunda maelfu na maelfu ya nafasi za kazi. Litakuwa ni jambo ambalo Mashariki ya Kati nzima inaweza kujivunia." Alipoulizwa ni nani angeishi huko, alisema inaweza kuwa makaazi kwa "watu wa ulimwengu," akitabiri kuwa ingegeuka kuwa "Riviera ya Mashariki ya Kati."
Trump anaonekana kuamini kuwa yeye ndiye Farauni wa zama hizi, akishikilia funguo za sayari nzima. Tangu siku yake ya kwanza madarakani, amekuwa akitoa ahadi za kijasiri na vitisho kila mahali, kuanzia Panama na Greenland hadi nchi jirani za Canada na Mexico, hadi kwa wapinzani kama China na Urusi, na hata kwa washirika wake barani Ulaya. Wote wamekabiliana na kiburi chake, na orodha inaendelea kukua. Anafanya kana kwamba ulimwengu ni mali yake binafsi: ima kunyenyekea kwake au kukabiliana na ghadhabu yake na vikwazo vikali, hasa vya kiuchumi.
Sasa, anaichukulia kadhia ya Palestina kama moja tu ya mikataba yake ya kibiashara, akitishia kuikalia kimabavu Gaza na kuiteka ili kujenga mji wake wa kitalii juu ya magofu yake na mafuvu ya watu wake. Kinaya ni, anazungumza juu ya uharibifu na hali isiyoweza kuishika ya Gaza kana kwamba ni matokeo ya majanga ya kimaumbile, mithili ya tetemeko la ardhi au volkano, badala ya matokeo ya uvamizi wa nchi yake na umbile la Kiyahudi katika kipindi cha miezi 15 iliyopita. Hata anadokeza nia yake ya kufanya maisha mjini Gaza yasiwezekane ili kuwalazimisha watu wake kuhama. Mjumbe wake wa Mashariki ya Kati na Waziri wa Mambo ya Nje pia wameeleza kwamba itachukua miongo kadhaa kuijenga upya Gaza ili kuifanya iweze kuishika tena. Mjumbe Steve Witkoff alisema, "Ni upuuzi kufikiria Gaza inaweza kuishika na Wapalestina ndani ya miaka mitano baada ya vita vya uharibifu kati ya 'Israel' na Hamas."
Mchakato wa kukaza kitanzi tayari umeanza. Tangu usitishaji mapigano uanze kutekelezwa, wameliruhusu umbile la Kiyahudi kuchelewesha kuingia kwa misaada ya kibinadamu, mahema, na nyumba za kuhama hama, pamoja na uhaba wa maji, chakula, na hali mbaya ya afya, na kufanya maisha mjini Gaza kuwa magumu sana, ikiwa sio kutowezekani.
Uadui wa Trump na Marekani dhidi ya Waislamu, hasa Wapalestina, si jambo geni wala si siri kwa mtu mwenye macho ya kuona. Iwapo umbile la Kiyahudi linaikalia kimabavu Gaza kwa usaidizi wa Marekani au Marekani inafanya hivyo moja kwa moja, wote wawili ni maadui wakorofi ambao kamwe hawatakubaliwa na watu wa Palestina au Umma wa Kiislamu. Waislamu hawatakubali maamuzi ya kiburi ya Trump. Ndoto na mipango yake itasambaratika dhidi ya uthabiti wa Umma wa Kiislamu na uthabiti wa watu wa Palestina. Ukweli kwamba Wapalestina wameshikilia ardhi yao iliyobarikiwa na kusimama kidete kwa miaka 77 dhidi ya umbile la Kiyahudi na dola zote za kikoloni zilizo nyuma yake unathibitisha kwamba Umma wa Kiislamu sio kama watawala wake walioridhika. Ushirikiano na utiifu Trump anaouna kutoka kwa viongozi vibaraka hautawahi kuakisiwa kwa Umma au watu wa Palestina.
Enyi Waislamu: Lau mungekuwa na Khalifa anayewatawala kwa njia ya Utume, Trump na mfano wake wangefikiri mara elfu moja kabla ya kusubutu kusema neno dhidi yenu au Uislamu. Kwa hiyo, lazima mujikusanye kwa haraka pambizoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi ili kusimamisha Khilafah leo. Katika historia yenu yote, ni majeshi ya Khilafah ndiyo yaliyonyamazisha matamanio ya walafi.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |