Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 10 Rabi' II 1446 | Na: H 1446 / 19 |
M. Jumapili, 13 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Haishangazi hata kidogo kwamba Serikali ya Modi, kwa kuhofia kutokea kulikokaribia kwa Khilafah ingepiga marufuku Hizb ut Tahrir - Chama cha Kweli cha Kisiasa na Kisicho na Vurugu
(Imetafsiriwa)
Kwa kuhofia kuibuka Khilafah inayoongozwa na Hizb ut Tahrir, Wizara ya Mambo ya Ndani ya India (MHA) mnamo Alhamisi iliyopita (Oktoba 10, 2024) ilipiga marufuku Hizb ut Tahrir, ikieleza kwamba “inataka kusimamisha dola ya Kiislamu ya kimataifa na Khilafah, ikiwemo India, kupitia jihad na shughuli za kigaidi”. Kwa sababu wanajua kwamba kuna hitaji kubwa la kuanzishwa dola ya Khilafah katika eneo hili chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir, na kwamba majenerali wa Kiislamu chini ya Khilafah inayokaribia wataikomboa tena India kupitia jihad, kama vile kamanda shujaa wa Khilafah Umawiyya, Muhammad bin Qasim akiwa na umri wa miaka 17, alimshinda Mfalme Dahir dhalimu mwaka 712. Na bishara ya RasulAllah (saw) itatimia, katika hadith iliyopokewa na Abu Huraira (ra), Mtume (saw) amesema, «لَيَغْزُوَنَّ الْهِنْدَ لَكُمْ جَيْشٌ، يَفْتَحُ اللهُ عَلَيْهِمْ حَتَّى يَأْتُوا بِمُلُّوكِهِمْ مُلَّكِهِمْ مُلَّكِهِمْ مُلُّوَ ِمْ ِمْ فِي فِرُ اللهُ ذُنُوبَهُمْ» “Hakika jeshi lenu litaivamia India na Mwenyezi Mungu atawapa ushindi wake mpaka wawatie wafalme wao minyororo na Mwenyezi Mungu atawasamehe dhambi zao” (Imepokewa na Na’iim bin Hammaad katika al-Fitan). Kwa hivyo, haishangazi hata kidogo kwamba utawala huu wa kioga wa Hindutva ungepiga marufuku Hizb ut Tahrir. Kwa kukitaja chama cha kisiasa kisicho na vurugu na cha kifikra cha Hizb ut Tahrir kuwa ni magaidi, wamewahadaa watu wao wenyewe na kufichua kufilisika kwao katika kukabiliana na Hizb ut Tahrir kifikra na kisiasa.
Enyi Watu, mnafahamu kwamba mwamko wa vijana chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ni jambo lisilofikirika, na kushuhudia haya, India kupitia vibaraka wake na baadhi ya vyombo vya habari nchini Bangladesh, imekuwa changamfu katika kueneza taarifa potofu dhidi ya chama hiki cha kisiasa kisicho na vurugu na cha kifikra, na kujihusisha katika jaribio lisilofeli la kupinga matakwa ya Khilafah kutoka ngazi zote za watu. Lakini India inapaswa kukumbuka kwamba kibaraka wake mwaminiwa, serikali ya dhalimu Hasina iliyoanguka, ilishindwa kuzuia sauti ya Hizb ut Tahrir licha ya ukandamizaji mkubwa katika miaka 15 iliyopita ya utawala wake. Kama mnavyojua, wakati mauaji ya kikatili ya Pilkhana yalipotokea mwaka wa 2009 katika njama za Hasina na India, chama pekee nchini Bangladesh, Hizb ut Tahrir, kililifichua jambo hili kwa taifa hili kwa kujitolea na kwa ujasiri. Na kwa hivyo njama ya India ya kudhoofisha jeshi la nchi hii lilipigwa chini. Na kisha serikali ya muuaji Hasina iliyoanguka ikaipiga marufuku Hizb ut Tahrir kwa amri ya India. Baada ya kufeli katika juhudi zote, India kwa kutapatapa sasa imechukua jukumu yenyewe dhidi ya Hizb ut Tahrir.
Enyi Watu, kupigwa marufuku kwa Hizb ut Tahrir na dola adui India ni cheti kwamba ni chama cha wakweli na uamuzi huu wa kizembe wakati huu unaashiria kwamba Khilafah iko karibu mno. Kwa hiyo, kuweni waanzilishi katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Mara tu baada ya kusimamisha Dola ya Khilafah, itafungua mashtaka ya mauaji ya Pilkhana, kufuta mikataba yote na India na kutangaza India kuwa nchi adui na kufunga balozi zake. Zaidi ya yote, Khilafah ingeiregesha India chini ya utawala wake ili kutimiza bishara njema ya RasulAllah (saw), na kukomesha utawala wa India na utulivu wa kieneo utaregeshwa.
[فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الأَمْرُ مِنْ قَبْلُ وَمِنْ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum: 4-5]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |