Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  1 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 18
M.  Ijumaa, 04 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Mpito Imeweka Mfano wa Aibu kwa Kumkamata Imtiaz Salim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh

(Imetafsiriwa)

Katika majira ya mapema Oktoba 4, 2024, serikali ya mpito, kwa desturi ya serikali ya kidikteta ya Hasina aliyeondolewa madarakani, ilimkamata Imtiaz Salim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh. Kwa mujibu wao, kosa lake ni kwamba alishiriki katika shughuli za kisiasa za Hizb ut Tahrir. Kama unavyoona, Imtiaz Salim alikuwa amewasilisha maombi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutaka kuondoa marufuku isiyo halali iliyowekwa na serikali dhalimu ya Hasina dhidi ya Hizb ut Tahrir na baada ya hapo akafanya mkutano na waandishi wa habari na timu ya wanasheria kuhusu kuwasilisha ombi hilo. Je, ni jinai kwake kupinga amri zisizo za dhulma za serikali dhalimu ya Hasina juu ya chama cha kisiasa chenye ikhlasi na ukweli cha Hizb ut Tahrir? Je, ni uhalifu kwamba yeye kwa niaba ya Hizb ut Tahrir alidai kuregeshwa haki za kisiasa zilizochukuliwa na serikali dhalimu ya Hasina? Sisi, Hizb ut Tahrir tunadai kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa Imtiaz Selim.

Tayari munafahamu kwa nini serikali ya Hasina iliweka marufuku haramu kwa Hizb ut Tahrir. Mnamo 2009, wakati mauaji ya kikatili huko Pilkhana yalipotokea katika njama ya Hasina na India, chama pekee nchini Bangladesh kilichofichua jambo hili kwa taifa kwa kujitolea na ujasiri kilikuwa Hizb ut Tahrir. Serikali ya mauaji ya Hasina ilishindwa kukabiliana na Hizb ut Tahrir kisiasa, na iliweka vikwazo visivyo halali na visivyo haki kwa shughuli zake kupitia taarifa kwa vyombo vya habari - bila nambari ya memo, bila nambari ya SRO na bila kutajwa kwa sheria - kukandamiza sauti yake ya haki na ya kupinga. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir iliendelea na shughuli zake, hasa kupinga kukamatwa, kupotezwa, mauaji, kufutwa kazi kwa maafisa wa jeshi na serikali ya Hasina na kuendeleza mapambano yake ya kisiasa yasiyolegeza msimamo dhidi ya serikali ya Hasina dhidi ya Uislamu, dhidi ya shughuli za Nchi na Watu. Katika muktadha kama hiyo, dhalimu Hasina mnamo mwaka 2013 kwa mara nyengine tena alipuuza sheria na utaratibu wowote, kwa kutekeleza amri ya kiutendaji kwa nguvu aliiorodhesha Hizb ut Tahrir chini ya Sheria maarufu ya Kupambana na Ugaidi.

Mara tu baada ya kuanguka kwa serikali ya Hasina, taarifa na habari mbalimbali za uzushi, za uongo na uchochezi dhidi ya Uislamu na Hizb ut Tahrir zilikuwa zikienezwa na serikali ya  India na vyombo vyao vya habari. Tunauliza, je, serikali ya mpito ina utiifu wao kwa dola za Magharibi na India? Je, wanajaribu kuthibitisha nini kwa kumkamata Imtiaz Salim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh? Sisi, Hizb ut Tahrir tunatoa wito kwa serikali ya mpito kuacha utegemezi kwa Wakoloni makafiri wa Magharibi na mshirika wao wa kieneo India kama vile kibaraka Hasina, na kuregea kwenye hisia na matarajio ya watu. Unapaswa kutambua kwamba wanafunzi, ambao kwa damu yao uliingia madarakani, wanakosoa vikali sera yako ya kuunga mkono Indi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ]

“Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Aal-i-Imran: 28].

Tunataka kusisitiza kwa maneno yaliyo wazi kwamba Hizb ut Tahrir ni chama chenye ukweli na cha kimfumo cha kisiasa ambacho lengo lake ni kuhuisha Umma wa Kiislamu na kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, na kuukomboa Umma wa Kiislamu kutoka katika makucha ya Dola za Wakoloni wa Magharibi na washirika wao wa kieneo. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنْ الْمُنْكَرِ وَأُوْلَئِكَ هُمْ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surah Aal-i-Imran: 104]. Ni kwa kusimamishwa Khilafah kwa njia ya Utume pekee, Bangladesh mpya itakuwa Dola adilifu na inayoongoza. Kwa hiyo, sisi, kwa niaba ya Hizb ut Tahrir, tunatoa wito kwa watu wote wenye ikhlasi na ushawishi wa nchi hii, kufanya kazi bega kwa bega na Hizb ut Tahrir na kusimama pamoja nasi kuiregesha Khilafah kwa njia ya Utume.

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“…kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza” (Hadith: Musnad Ahmad)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu