Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  26 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 17
M.  Jumapili, 29 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Dhalimu Hasina ameanguka, lakini Washirika wake Waaminifu wa Kihindi bado wapo na wanaendelea kueneza Uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir

(Imetafsiriwa)

Dhalimu Hasina amepinduliwa, lakini wapambe wake na wafuasi watiifu wa India bado wana udhibiti. Mawakala hawa wa Hasina wanaopinga Uislamu wako dhidi ya ubwana wa watu na hivyo wanakula njama za kukitenganisha chama cha kweli cha kisiasa Hizb ut Tahrir na watu kwa kueneza uwongo na uzushi. Juhudi zao zinashindwa, kwa sababu Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha kimfumo na kifikra chenye msingi imara miongoni mwa watu katika ngazi zote. Umma unafahamu kwamba Hizb ut Tahrir ndicho chama pekee nchini Bangladesh kisicho na uoga na chenye kujitolea kufichua ukweli kuhusu mauaji ya kikatili ya Pilkhana ya 2009, ambayo yaliratibiwa na Hasina na India. Serikali ya muuaji ya Hasina ilishindwa kukabiliana na Hizb ut Tahrir kisiasa, na ikaweka marufuku isiyo halali na isiyo ya haki kwa shughuli zake kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo haikuwa na nambari ya memorandum, nambari ya SRO, na haikuwa na kifungu cha sheria, ili  kukandamiza kazi yake. sauti ya haki na ya kupinga. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir iliendelea na shughuli zake, hususan kupinga ukamataji, upotezaji, mauaji, kutimuliwa kwa maafisa wa jeshi na serikali ya Hasina na kuendeleza mapambano yake ya kisiasa yasiyolegeza msimamo dhidi ya Uislamu na dhidi ya watu. Katika muktadha kama huo, kwa kupuuza sheria, dhalimu Hasina mwaka 2013 kwa mara nyengine tena aliiorodhesha Hizb ut Tahrir chini ya Sheria ya Kupambana na Ugaidi kupitia agizo dhalimu la kiutendaji. Na wapambe waliojificha wa Hasina bado wako hai katika kutekeleza ajenda ya dola ya Kishirikina India kwa kueneza propaganda za uongo. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَاللّٰهُ يَشْهَدُ اِنَّ الْمُنٰفِقِيْنَ لَكٰذِبُوْنَ] “Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo.” [Surah Al-Munafiqun: 1].

Tunataka kusema kwa ufasaha kwamba lengo la Hizb ut Tahrir ni kuhuisha Umma wa Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Inataka kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kwa kuukomboa Umma wa Kiislamu kutoka mikononi mwa dola za kibeberu za Magharibi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَلْتَكُنْ مِّنْكُمْ اُمَّةٌ يَّدْعُوْنَ اِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُوْنَ بِالْمَعْرُوْفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ ۗ وَاُولٰۤىِٕكَ هُمُ الْمُفْلِحُوْنَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surah Aali-Imran:104]. Ni kupitia tu kusimamishwa Khilafah ambapo Bangladesh mpya itakuwa nchi inayoongoza kwa misingi ya haki. Kwa hakika munafahamu kwamba kusimamisha Khilafah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni suala la wakati tu. Khilafah ijayo itawahukumu vibaraka hawa pamoja na Hasina.

Tungependa pia kusisitiza kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Bangladesh Bw. M Mainul Islam kwamba unashikilia wadhifa wa uwajibikaji unaotaka kuzingatia ukweli halisi. Baada ya kumpindua dikteta Hasina, watu wa nchi yetu hakika hawatarajii uongo wa wazi kutoka kwa wadhifa wako kama vile maafisa wa kutekeleza sheria walivyofanya wakati wa utawala wa dhalimu Hasina. Wakati Hizb ut Tahrir ni chama kinachoungwa mkono na watu ambacho kinafurahia umaarufu mkubwa miongoni mwa matabaka yote ya jamii, inakuwaje hata ufikirie kukiita chama hicho kama cha ‘wanamgambo’! Ubandikaji huo wa uongo wa nguvu za kisiasa zinazounga mkono na Waislamu kama vile Hizb ut Tahrir ni ajenda ya kinyama ya Mshrikina India na mabeberu wa Magharibi kupambana na Uislamu wa kisiasa na kuchelewesha kuregea kwa Khilafah Rashida. Pia, kufikia sasa, lazima ujue kwamba Hizb ut Tahrir tayari iliwasilisha ombi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bangladesh mnamo Septemba 5, 2024 ya kuondoa marufuku isiyo halali iliyowekwa juu yake na serikali iliyopanduliwa ya Hasina, na wizara tayari imekubali ombi hilo kwa ukaguzi. Kwa hivyo, maoni yoyote kama haya ya kutowajibika kutoka kwa afisa wa ngazi ya juu zaidi wa polisi yatazuia uhakiki usioegemea upande wowote ya rufaa na uamuzi wa haki. Kwa hiyo, tunakuhimiza kusimama upande wa watu wa Bangladesh na Uislamu, na nguvu kama Hizb ut Tahrir ambayo daima itabaki kuwa watetezi wa watu. Sasa ndio wakati mwafaka wa kujionyesha kuwa mwaminifu, mtetezi wa watu, na mpenda Uislamu badala ya kuingia katika mtego wa njama za kupinga dola za India. Waangalie wakuu wa awali wa mashirika mbalimbali ya polisi nchini Bangladesh ambao walitembea kwenye vichochoro vya giza vya njama za India. Pia, kama Muislamu, ni wajibu wako pia kusaidia nchi hii kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Unapaswa kulinda wito wa Uislamu na kuwalinda wabebaji wito huu. Watu wa Bangladesh kamwe hawatakuvumilia ikiwa utakuwa msemaji yule yule wa India kama wakuu wa zamani wa polisi wa Hasina.

Hivyo basi, sisi, kwa niaba ya Hizb ut Tahrir, tunatoa wito kwa watu wote wenye ikhlasi na ushawishi mkubwa wa nchi hii kuwapinga watiifu wa Hasina wanaoungwa mkono na India kutoka katika misimamo yao na kufanya kazi bega kwa bega na Hizb ut Tahrir na kusimama nayo kuregesha Khilafah - suluhisho pekee la matatizo yote ya nchi hii.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu