Afisi ya Habari
Denmark
H. 21 Rabi' II 1446 | Na: 02 / 1446 H |
M. Alhamisi, 24 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maimamu Hawana Wajibu wowote wa kutoa Ufafanuzi kwa Mawaziri Wanaounga Ugaidi
(Imetafsiriwa)
Mnamo Oktoba 23, 2024, Jyllands-Posten ilichapisha makala yenye kichwa “Maimamu lazima watoe jibu: Uchunguzi unawahimiza mawaziri kuwaita viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Denmark kwa ajili ya ‘mazungumzo mazito’.” Pamoja na Waziri wa Ushirikiano na Waziri wa Makanisa wakipiga pamoja picha zisizopungua nne, tulifahamishwa kwamba wanapanga kufanya majadiliano mazito juu ya maadili, chuki dhidi ya Mayahudi, na msimamo wa Waislamu kuhusu kadhia ya Palestina katika mkutano na maimamu na wawakilishi wa Waislamu mnamo Oktoba 24, 2024.
Ni jambo chanya kwamba wawakilishi wa Waislamu walighairi ushiriki wao katika mkutano huo na kukataa “kuitwa” na mawaziri ambao wametangaza wazi nia yao ya kuwaingiza Waislamu katika maadili yale yale ambayo yamewawezesha kuunga mkono ugaidi wa dola ya Kizayuni na kwa muda wa mwaka mmoja wa mauaji ya halaiki huko Gaza. Hakuna msingi wa mazungumzo ya maana au sawa kati ya wawakilishi wa jamii ya Kiislamu na mawaziri wasio na haya, ambao kile kinachoitwa maadili yamezikwa kina cha chini katika majivu ya mauaji ya halaiki.
Waislamu na wasiokuwa Waislamu vile vile, wale walio na adabu na ubinadamu wa kimsingi, wameonyesha wazi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwamba wanakataa kukubali kimya kimya jinai zisizoelezeka za Wazayuni ambazo serikali ya Denmark imefanya kila kitu ili kuzifinika. Huku wakiunga mkono kwa moyo wote ugaidi wa kimpangilio wa watu halali wa Palestina, wanalenga, wakiwa na kadi ya ugaidi mkononi, hasa sauti za Waislamu zinazotaka ukombozi wa Palestina. Kwa upande mwingine, wanashikilia kadi ya chuki dhidi ya Mayahudi, ambayo, haswa kwa kifurushi kipya cha kisheria juu ya suala hilo, imefichuliwa kuwa ni pazia nyembamba, inayotumika kuhalalisha upinzani dhidi ya uvamizi wa mauaji ya halaiki wa Kizayuni.
Huku kiburi kikitiririka kutoka katika kila tundu la miili yao, mawaziri hawa wanataka kuhubiri akhlaki na maadili kwa umma wa Kiislamu.
Jambo moja, hata hivyo, wako sahihi kulihusu: ujumbe wazi unahitajika:
- Mfumo wa maadili unaowakilishwa na serikali ya Denmark umeshindwa kabisa katika mauaji ya halaiki yanayoendelea. Waislamu hawana sababu yoyote ya kujiunga nayo. Dybvad na Dahlin (mawaziri wanaohusika) wanaweza kuchukia wanavyotaka. Kwani baada ya yote, wao si wa mwanzo linapokuja suala la chuki dhidi ya Uislamu.
- Waislamu hawawezi kuwajibishwa kwa chuki kubwa iliyokita mizizi ya Kiyahudi barani Ulaya ambayo ilisababisha jinai ambazo sasa zinatumiwa kisiasa kwa mauaji ya halaiki na mauaji ya kikabila yanayotekelezwa na Mayahudi wa Kizayuni wenye asili ya Ulaya kimsingi dhidi ya wahanga wa Kiislamu huko Palestina.
- Ukombozi kamili wa Palestina yote kupitia kukomeshwa kwa uvamizi wa kikatili wa kijeshi unaoitwa “Israel” ni wajibu wa Kiislamu na hitaji la kibinadamu, ambalo linapaswa kutangazwa kwa sauti kubwa na bila shaka, hasa katika mimbari za misikiti.
- Kuna sababu moja tu ya msingi kwa wawakilishi wa Waislamu kukutana na wanasiasa wanaopiga vita maadili ya Kiislamu, kuzuia haki zetu, na kuunga mkono ugaidi wa dola na mauaji ya halaiki ya watoto na wanawake – kufichua uovu na unafiki wao na kukataa kabisa kusujudu hata kidogo kwa madai na vitisho vyao, bila kujali matokeo.
Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Denmark |
Address & Website Tel: |