Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  1 Safar 1446 Na: 01 / 1446 H
M.  Jumanne, 06 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwanachama Mwengine wa Hizb ut Tahrir Atiwa hatiani kwa Kutoa Wito wa Ukombozi wa Palestina: Historia Itakumbuka Neno la Kweli na Wahalifu wa Kweli

(Imetafsiriwa)

Siku 303 baada ya mauaji ya halaiki ya Wazayuni yanayoungwa mkono na Denmark dhidi ya raia wa Gaza, hukumu nyengine imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Copenhagen dhidi ya mwanachama wa Hizb ut Tahrir kwa kutoa wito wa ukombozi wa kijeshi wa Palestina. Ilianzisha hukumu ya kifungo cha miezi 9 jela bila masharti kwa Sam Mohabbat kueleza yaliyo dhahiri katika maandamano ya mnamo 10 Oktoba 2023: kwamba uvamizi wa Wazayuni mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 ulikabiliwa na pigo la kudhalilisha ambalo lilifichua udhaifu wake kwa ulimwengu na kuharibu simulizi ya kutoshindwa kwake. Kwamba silaha muhimu zaidi katika safu ya uvamizi huu wa kinyama, wa kijeshi ulisagwa sagwa siku hiyo ya kihistoria - kuzuiwa.

Tangu wakati huo, kwa ukatili mpya, Wazayuni wamejaribu kwa kutapatapa kuregesha kile ambacho mara moja kiliteketezwa, na katika mchakato huo walidhihirisha ukosefu wao kamili na wa Magharibi wa ubinadamu wao wenyewe. Hata hivyo, hii imeutia nguvu tu ujumbe kwamba uvamizi wa Kizayuni unaishi kwa wakati ulioazimwa na haujawahi kuwa na uhalali wowote. Ulianzishwa kwa vita vya kikabila, mauaji ya halaiki, mateso na wizi wa ardhi kwa msaada na ushajiisho wa dola za Magharibi, ikiwemo Denmark. Leo hii unaendelea na kazi yake kwa kutumia mbinu zilezile, na dola ya Denmark inaendelea na usaidizi wake wa kuchukiza na usafirishaji wa silaha kwa ajili ya mauaji ya halaiki.

Hukumu hii inapaswa kuonekana jinsi ilivyo. Tume ya kisiasa inafanya kazi kutoka kwa serikali inayotapatapa, iliyokumbwa na migogoro ambayo, mithili ya uvamizi wa mauaji ya halaiki ambao inauunga mkono kwa dhati, inaonyesha tu uozo wake kabisa. Waziri Mkuu asiye na historia na asiyestahili kihistoria, Mette Frederiksen, alitangaza mnamo 9 Novemba 2023, kwamba “amefadhaishwa” na maandamano mengi yanayounga mkono Wapalestina, na kumtuma Waziri wake wa Sheria mjini kwa muda wa wiki moja tu kujibu mashtaka ya kisiasa katika “Maelezo ya jinsi polisi na upande wa mashtaka wanavyotumia ulinzi wa sheria ya jinai dhidi ya uchochezi na kuunga mkono ugaidi”.

Unafiki wa kipuuzi unadhihirika wazi wakati pindi wanasiasa wa serikali, viongozi wa maoni na waandishi wa habari kwa zaidi ya siku 300 wameonyesha uungaji mkono wao kwa uvamizi, mauaji makubwa ya watoto na njaa ya pamoja kwa zaidi ya siku 300. Rasmi Denmark inaunga mkono uhalifu huu dhidi ya yote ambayo hayawezi kukiukwa na pengine inawazia kwa utovu wa kanuni zake kwamba majaribio yake ya vitisho kwa kufunguliwa mashtaka na adhabu yatapunguza kasi ya wito wa ukombozi wa Palestina.

Hizb ut Tahrir / Denmark inampongeza mwanachama wetu, Sam Mohabbat, kwa msimamo wake mtukufu. Ana hatia ya kulingania suluhisho la pekee kwa Palestina - kuondolewa kwa “Israel” na ukombozi kamili wa Palestina na majeshi ya Kiislamu ya nchi zinazoizunguka kwenda vitani, vita vya heshima na vya haki vya ukombozi kutoka kwa uvamizi wa kijeshi na ugaidi wa dola unaoungwa mkono na Denmark.

Hukumu 40,000 za mahakama ya kisiasa hazitatunyamazisha au kutikisa azma yetu hata kidogo!

Palestina itakombolewa na historia itakumbuka neno la kweli pamoja na wahalifu wa kweli.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu