Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  17 Jumada I 1446 Na: 03 / 1446 H
M.  Jumanne, 19 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waislamu nchini Denmark Kamwe Hawatajioanisha na Maadili ya Serikali ya Mauaji ya Halaiki

(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano ya kina na ya jukwaani na Jyllands-Posten mnamo Novemba 18, 2024, Waziri Mkuu Mette Frederiksen anafanya juhudi kubwa kutoa taswira kali ya idadi ya Waislamu wa nchi hiyo. Anatuhumu Quran kuwashajiisha Waislamu kufanya uhalifu, kuwapiga watoto wao, na kujihusisha na tabia ambayo inaleta ukosefu wa usalama katika maeneo ya umma. Hatari inayodaiwa kuletwa na Waislamu wanaoishi Denmark inalinganishwa na tishio la “Urusi na Putin.”

Katika mahojiano hayo, Waziri Mkuu anadai “uoanishwaji kwa msingi wa maadili” kutoka kwa Waislamu, akimaanisha kwamba lazima waache maadili yao ya Kiislamu. Maoni juu ya ushoga, Palestina, na kutumia Quran kama maregeleo yameainishwa kama maoni ambayo yanawafanya Waislamu kuwa maadui wa jamii.

Mahojiano haya yanajiri katika wakati ambapo hakuna juhudi zozote za serikali za kisiasa zilizofaulu kubadilisha idadi duni ya wapiga kura kihistoria. Jaribio lililofeli la Waziri Mkuu la kutoa taswira ya huruma zaidi limefanya kidogo kubadilisha mtazamo wa umma juu yake kama mwanasiasa mwenye taaluma ya ukosoaji na upigaji hesabu. Kwa kutapatapa, sasa anaamua kucheza “karata ya Uislamu” kwa matumaini ya kupata pointi duni za kisiasa.

Tuhma zake za udanganyifu dhidi ya Quran kama chanzo cha uhalifu na unyanyasaji dhidi ya watoto ni kauli za kuchukiza zaidi kuwahi kutolewa na Waziri Mkuu wa Denmark. Kwa njia ya hila, ananasibisha maadili ya Kiislamu na uhalifu, ghasia, na ukosefu wa ajira, licha ya kujua vyema kwamba uhalifu wa magenge miongoni mwa vijana wa Kiislamu unasukumwa na kuvutiwa na utamaduni wa Kimagharibi. Kitambulisho cha Kiislamu, kwa hakika, ndio kipengee chenye ufanisi zaidi katika kuwavuta vijana kutoka katika muondoko huu duni wa maisha wa Kimagharibi.

Waziri Mkuu anafahamu kabisa kwamba ukosefu wa usalama na vurugu havihusiani na Waislamu wanaojifunga na Uislamu. Viwango vya uhalifu wa vijana ni vya chini kihistoria na vinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka. Hii ni hasa kutokana na kukiri kwa Mette Frederiksen mwenyewe katika mahojiano: vizazi vichanga vya Waislamu vinashikamana Uislamu kwa uthabiti zaidi kuliko vile vilivyotangulia.

Taswira anayojaribu kuwaonyesha Waislamu kama vimelea vya kijamii inapingwa na tafiti nyingi za kiuchumi, ambazo zinaonyesha kwamba kiwango cha juu cha ajira cha “wahamiaji wasio wa Magharibi” kimekuwa msingi wa ukuaji wa uchumi unaoendelea wa Denmark katika miaka ya hivi karibuni.

Tishio la kweli kwa jamii ya Denmark halitokani na jamii ya Waislamu bali kutokana na ukaidi wa Waziri Mkuu, ambao umedhihirika wazi katika kuunga mkono mauaji ya halaiki huko Gaza. Waislamu hawatakubali kamwe maadili yake ya mauaji ya halaiki, kwa vile hayawavutii wao wala kwa yeyote aliye na hata chembe ya ubinadamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu