Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  10 Rajab 1445 Na: 1445 / 07
M.  Jumatatu, 22 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Inalipa Gharama ya Kutetea Masuala ya Ummah na Kutoa Wito kwa Majeshi yake Kuwanusuru Watu wa Gaza
(Imetafsiriwa)

Mnamo Ijumaa, Januari 19, 2024, Uingereza ilipiga marufuku rasmi Hizb ut Tahrir, ikiituhumu kwa chuki dhidi ya Mayahudi na kuunga mkono shambulizi la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, dhidi ya umbile la Kiyahudi. Iliiongeza Hizb kwenye orodha yake ya mashirika yaliyoainishwa kama mashirika ya kigaidi.

Tuhma hii ni uongo na udanganyifu. Msimamo wa Hizb ut Tahrir wa kuunga mkono Waislamu wanaokabiliwa na jinai mbaya zaidi za kibinadamu huko Gaza hauna uhusiano wowote na chuki dhidi ya Mayahudi. Vile vile, uungaji mkono wake kwa Waislamu wa Rohingya na Uighur huko Myanmar na Turkestan Mashariki, ambao wamekabiliwa na mauaji ya halaiki, hauhusiani na chuki dhidi ya Ubuddha.

Baada ya takriban miaka arubaini ya kuwepo Uingereza, James Cleverly, Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya Rishi Sunak, anaamua leo kwamba ni shirika la kigaidi! Ni vyema kutambua kwamba Uingereza, kama ilivyo kwa ulimwengu wote, inatambua kwamba Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa chenye kanuni za Kiislamu. Kazi yake ya kisiasa haikubali vitendo vya vurugu, kwa kuzingatia hukmu za Sharia katika suala hili.

Ukweli ni kwamba ulinganizi wa Hizb ut Tahrir wa kuyataka majeshi ya Kiislamu yawanusuru ndugu zao wanaodhulumiwa huko Gaza umetikisa misingi ya utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wa Magharibi. Wanatambua kikamilifu kwamba tukio kama hilo linaashiria mwisho wa umbile la Kiyahudi na mwisho wa utawala wa Magharibi juu ya ardhi za Kiislamu.

Enyi Waislamu, hii ndiyo Magharibi ambayo imepasua vichwa vyetu kwa madai yake ya demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu. Kauli mbiu zote hizi huyayuka linapokuja suala la Uislamu na Waislamu. Neno la haki huwakera na kusumbua akili zao. Barakoa wanazojaribu kueneza katika nchi za Kiislamu zimeanguka, na kufichua uhalisia wao wa kihalifu na ushirikiano wao na mhalifu ambaye hutoa hasira yake kwa watu walio madhaifu, wakiwemo wanawake, watoto, na wazee, kutoka kwa watu wenye ujasiri wa Gaza.

Hebu Uingereza na ulimwengu mzima naujue kwamba Hizb ut Tahrir haitazuiliwa kutokana na wajibu wake, unaofanywa kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu, kwa upigaji marufuku, kuharamisha, au uorodheshaji wa magaidi. Hili litaongeza tu kujiamini kwake kwamba iko kwenye njia iliyo sawa na njia iliyonyooka.

Enyi Umma wa Kiislamu na watu wenye nguvu na ustahimilivu, je, haujafika wakati kwenu kutambua hofu na uoga wa adui yenu wa kurudi kwenu katika Dini yenu na njia ya Mwenyezi Mungu wenu? Je, haujafika wakati wa nyinyi kuwa makini katika kufanya kazi ya kuhuisha maisha kamili ya Kiislamu pamoja na wafanyikazi wenye ikhlasi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume? Munawaona Wazayuni na Wamagharibi waliokufuru wametoa meno yao, na chuki yao inadhihirika. Wamekusanyika, wakiweka kando tofauti zao, na wanapambana na lile lililokuwa jinamizi kwao. Tunawalingania, enyi Waislamu, kuweni wenye kumnusuru Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa watangulizi wenu, muwatoe watu katika giza kuwapeleka kwenye nuru, kutoka katika ibada za wanadamu hadi kwenye kumwabudu Mola wa wanadamu. Kuweni na imani na ahadi ya Mwenyezi Mungu na nusra yake kwa waumini katika ushindi wa hapa duniani na furaha ya kesho Akhera.

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur:55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu