Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  7 Shawwal 1445 Na: 1445 / 10
M.  Jumanne, 16 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaliko wa Washington kwa Waziri Mkuu wa Iraq ... Maagizo Badala ya Mazungumzo
(Imetafsiriwa)

Rais wa Marekani, Joe Biden, alitoa mwaliko kwa Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani, Kuzuru Washington. Mwaliko huo ulikubaliwa, na alingoza ujumbe uliokutana na maafisa kadhaa mnamo Jumatatu, Aprili 15, 2024, akiwemo Rais Joe Biden na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin.

Katika mkutano wake na al-Sudani, Rais wa Marekani alianza kwa kueleza uungaji mkono wa Marekani kwa umbile la Kiyahudi na umuhimu wa usalama wake. Majibu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Iraq yalikuwa ya kusitasita na hafifu, kwani alisema, “... maoni yetu huenda yakawa tofauti kuhusu yale yanayoendelea huko katika eneo hilo, lakini tunakubaliana pasi na shaka na sheria ya kimataifa, sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na jukumu la kulinda sheria ya vita. na tunakataa uchokozi wowote dhidi ya raia, haswa wanawake na watoto. Na tunashajiisha kujitolea sio kutoheshimu desturi za kimataifa na uhusiano wa kidiplomasia”.

Ukweli ni kwamba mkutano huu haukuwa kwa ajili ya kujadili masuala kati ya serikali hizo mbili; badala yake, ulikuwa mwaliko kwa bwana kuamuru masharti yake kwa mtumishi wake. Marekani ni nchi inayokalia kwa mabavu iliyoivamia Iraq, ikaangusha utawala wake, ikavunja jeshi lake, ikaanzisha utawala wake wenyewe, ikalazimisha katiba yake, na kuleta vibaraka wake kulinda mfumo wake. Usanii wote na udanganyifu wa vyombo vya habari kuionyesha Iraq kama umbo huru ni uongo na udanganyifu unaothibitishwa na uhalisia wa kisiasa wa nchi hii.

Kwa hivyo, mwaliko na ziara hii ulilenga kuimarisha avamizi chini ya visingizio vya kuvutia. Wakati serikali ya Iraq inazungumza kuhusu kukomesha uwepo wa muungano wa kijeshi nchini humo, Austin alisema katika Pentagon, "Mataifa haya mawili yanakubaliana juu ya haja ya mpito kuelekea uhusiano wa kudumu wa usalama wa pande mbili." hili lilisisitizwa katika tweets za balozi wa Marekani jijini Baghdad, akisisitiza ushirika wa kimkakati wa kina na wa kudumu kati ya Washington na Baghdad katika ngazi zote, ikiwemo nyanja za utamaduni na afya.

Enyi Ummah wa Kheri, na Enyi Umma Bora: huu ndio uhalisia wa wale ambao wamejitwika mamlaka juu yenu; wao ni watumwa duni wanaotafuta kibali cha mabwana zao kwa gharama ya watu, usalama wao, na mali zao. Hii ndiyo hali yenu ya sasa baada ya dola yenu kupinduliwa, na ubwana wenu kutoweka. Katika zama hizo (chini ya Khilafah), watawala wa Waislamu walikuwa hawaondoki nchini isipokuwa kama wakombozi au mahujaji wanaoelekea kwenye Nyumba Tukufu. Hata hivyo, watawala wenu leo hawaondoki isipokuwa kama walaji njama au wezi wanaokimbia. Basi amkeni kutoka katika usingizi wenu, na muitikie amri ya Mwenyezi Mungu kwa kutabikisha Shariah yake na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na mpeni bay'ah Imam mwadilifu anayetiiwa na kupigana nyuma yake. Hapo ndipo mtapata heshima hapa duniani na kufaulu kesho Akhera.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu