Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  10 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 14
M.  Jumapili, 16 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pongezi kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd
(Imetafsiriwa)

Kwa mnasaba wa Idd al-Adha, tunatoa pongezi na baraka tele kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla, na hasa kwa wafanyikazi wenye ikhlasi kutoka miongoni mwa wabebaji Dawah kwa ajili ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, wa kwanza miongoni mwao, Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amhifadhi na ampe ushindi kupitia mikono yake). Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu airegeshe Idd hii kwa Umma wa Kiislamu kwa usalama, amani, na Uislamu, na aifanye kuwa ni Idd yenye baraka iliyojaa kheri, neema, ushindi, na tamkini.

Enyi Waislamu: Tunamhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu mwanzo na mwisho kwa neema zake zilizo dhahiri na zilizofichika. Tunamuomba atukubalie amali zetu njema na zenu. Huku tukifurahia siku hii na kusikia sauti za Waislamu zikivuma kwa "Labbaik Allahumma Labbaik" katika kuitikia wito wa Mola wao wa kutekeleza faradhi ya Hija, maumivu ni makali. Ulimwengu mzima unashuhudia mauaji yanayofanywa na Mayahudi na washirika wao kutoka kwa makafiri wa Magharibi dhidi ya watu wetu katika Gaza yenye ujasiri, uhalifu usio wa kibinadamu ambao unaaibisha ubinadamu. Maumivu yetu yanazidi tunaposhuhudia jinai hii kwa macho yetu wenyewe, huku majeshi ya Umma wa Kiislamu yakibaki bila kuchukua hatua yoyote, yakiwa hayana mwelekeo wa kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa. Vilio vya wafiwa na machozi ya watoto haviwasumbui, na majeshi haya bado hayajibu kwa sauti ya juu kabisa “Labbaik Allahumma Labbaik” katika kuitikia mwito wa Mola wao wa jihad na kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa. Je, udhaifu na udhalilifu umefikia kiwango hiki?

Hata hivyo, enyi Umma wa Kiislamu, jueni kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, kwamba ushindi wa Mwenyezi Mungu uko karibu, na kwamba pamoja na dhiki huja wepesi. Ummah huu una rutuba, na tunaona kwa macho yetu kile kikundi kidogo, chenye imani chenye rasilimali chache kinavyofanya dhidi ya adui aliyejihami kisawasawa na usaidizi wa wazi wa Magharibi. Uvamizi huu umedumu kwa zaidi ya miezi minane, na kuudhihirishia ulimwengu uoga wa kweli wa Mayahudi na kwamba umbile lao ni dhaifu kuliko utandu wa buibui.

Enyi Umma wa Kiislamu na Watu Wenye Nguvu: Hii ni siku yenu, na huu ndio wakati wa uamuzi wa kutangaza muko kambi gani – kambi ya imani, ambapo mnaitikia amri ya Mola wenu Mlezi:

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia,” [Al-Anfal:72] Au kambi ya unafiki, ambayo Mwenyezi Mungu anasema kuihusu:

[وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا]

“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Al-Ahzab:67]?!

Jueni kwa yakini kwamba adui yenu asingesubutu kufanya kitendo hiki kiovu lau mungekuwa na mamlaka na dola. Kwa hivyo, enyi Umma wa Kiislamu, kunjeni mikono ya mashati yenu na muharakishe kufanya kazi na wale wanaojitahidi kusimamisha Khilafah na Dini, ngome ya Ummah, na taji la faradhi za Rab Al-Alamin.

Kwa kumalizia, tunaupongeza Ummah wa Kiislamu kwa Idd al-Adha iliyobarikiwa na kusema: Muwe karibu na Mwenyezi Mungu kila mwaka... Ummah wa Kiislamu uwe kwenye kheri kila mwaka.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu