Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  10 Jumada I 1441 Na: 1441 / 06
M.  Jumapili, 05 Januari 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Uokovu wa Taifa kutoka kwa Majanga yake na Kuhifadhi Hadhi yake kunaweza kupatikana tu kwa kufuata Njia ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Miezi mitatu imepita tangu kuanza kwa harakati maalumu nchini Iraq, ambayo imeongezeka kwa masafa na ukali ili kujumuisha sekta kubwa za watu, zilizowasilishwa katika utalaamu mbalimbali katika jamii kama vile madaktari, wahandisi, wanafunzi wa vyuo vikuu, wanasheria, wafanyibiashara, na wamiliki wa shahada za kisayansi pamoja na majeshi yasiyoajiriwa, na pia watu wa makabila kadhaa katika majimbo ya kati na kusini, na takriban watu wote – isipokuwa wachache - wamehusishwa katika maandamano haya kuunga mkono uasi baada ya kushindwa kuvumilia dhulma kubwa na ukweli wakuhuzunisha unaotokana na sera za mfululizo wa serikali zilizowekwa na kafiri tangu mwaka wa 2003.

Licha ya usumbufu kamili wa maisha katika vituo kadhaa vya nchi, vikundi vinavyotawala bado vinachukua nafasi zao kwa njia za kudanganya na kutoa maoni kwa raia kuwa wanabadilisha uhalisia wa ufisadi kama njia yaa kukaa na kushikilia udhibiti wa madaraska kwa kubadilisha baadhi ya nyuso za kiza! Pamoja na utekaji nyara unaoendelea wa wanaharakati na kufilisika kwa mwili unaotekelezwa na vikosi vya Irani, uhalifu huu hauwaongezei waandamanaji isipokuwa kuthubutu zaidi katika nafasi zao zilezile kuhusu kukataliwa kwa chama tawala kwa ujumla.

Nchi imekuwa bila ya kiongozi anayesimamia mambo ya watu wake; serikali imejiuzulu, “na Rais wake” Rais Barham Saleh yuko kati ya moto wa mapinduzi ya vijana, na kati ya shinikizo la vyama fisadi ambavyo vinailaumu katiba kuwa ndio sababu ya hali mbaya iliyoko, kwa hivyo imeshindwa hadi sasa kuweka mrithi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Abdel-Mahdi, licha ya tarehe za mwisho zilizokosekana za katiba zilizowafanya wao kukejeliwa kwa kila muangalizi!

Kwa upande wa hali hii isiyowezekana, Amerika imekuwa kitovu cha matatizo kwa wafanyikazi wake nchini Iraq, kukasirishwa na kutofaulu kwao kuidhibiti barabara yenye hasira, na ilikuwa tu baada ya ukweli kwamba – baada ya kimya kirefu juu ya vyama vya Irani na mikono yake iliyorefuka nchini – ilimtoa kafara mmoja wa mbwa wake wakali, Qassem Soleimani, ambaye alinyonya damu ya watu wengi wasio na hatia nchini Iraqi, Syria, Lebanon na Yemen. Amerika ilifanya hivyo kulipiza kisasi kwa jeraha (kujivunia kwake) kama taifa lenye nguvu na ushawishi mkubwa baada ya kuvamia ubalozi wake huko Baghdad kutoka kwa wanamgambo ambao iliwasimamia kwa upande mmoja, na jaribio la kutembea na raia wanaoikataa na wateja wake kwa upande mwingine, na tatu kwa kujitayarisha kwa kupangilia hali nchini Iraq baadaye kwa kulazimisha wakala mpya ambaye picha yake bado haijachomwa kwa kumpa utawala, ili aweze kuitoa nchi katika majanga yake iliyonayo hivi sasa.

Enyi vijana wa mapinduzi:

Kama tunavyoangazia ukweli wa mateso yenu na kuwasilisha ukweli wa wazi mbele yenu, sisi kwa hakika na kwa dhati tunawashauri na kuwaonya nyinyi dhidi ya matokeo ya kufuata mfumo wa Kafiri katika siasa na usimamizi wao wa mambo ya watu kupitia udanganyifu wa demokrasia ya kafiri na usekula mbovu, ambao unaweza kuwarudisha nyinyi nyuma ya ndoto zake za urongo kuwaondoa nyinyi mbali na njia ya uokovu ambayo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka aliwataka nyinyi mulete sheria ya Uislamu safi na kweli juu ya usumbufu wa madhehebu mabaya na ubaguzi wa rangi, kwa hivyo rudini kwenye Uislamu kwani chini yake ni uadilifu, usalama na maisha mazuri.

(وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُصِيبَهُمْ بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ * أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu* Je, wao wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah: 49- 50]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu