Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza

Kwa kuamini Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu na watu wa Jordan kwa jumla na kwa mashababu wa Hizb ut Tahrir hasa, mmoja wa mashababu wake waaminifu, wenye subira na matumaini, ndugu mwanachuoni mkubwa:

Dkt. Abdul Halim Muhammad Al-Ramahi (Abu Imad)

Soma zaidi...

Tatizo la Kiuchumi nchini Jordan Kimsingi ni Tatizo la Kisiasa, na halitatatuliwa isipokuwa kupitia Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu kwa kuregea Dola ya Khilafah

Haikutarajiwa kamwe kwamba Baraza la Wawakilishi, lenye kiwango cha 75% ya waliohudhuria, lingeidhinisha sheria jumla ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023, licha ya ukosoaji mkali wa mswada huo wakati wa vikao vya mijadala ya siku 3 kutokana na nakisi ya kifedha, riba kubwa (riba) ya deni la umma, na kukosekana mipango, miradi na mikakati inayokuza ukuaji wa uchumi.

Soma zaidi...

Inatosha Udhalilifu, Shutma, na Uombaji kwa Umbile la Kiyahudi na Wafuasi wake Waovu! Majeshi ya Umma Na Yalimalize Umbile hili Katili ndani ya Saa Moja!

Kabla ya watawala wa Misri na Jordan kuhitimisha makubaliano ya udhalilishaji na fedheha pamoja na umbile la Kiyahudi na kutambua uwepo wake katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na iliyo na Misikiti wa tatu kwa utukufu baada ya misikiti miwili Mitukufu, Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa

Soma zaidi...

Mkataba wa Maelewano (MoU) wa Umeme kwa Maji ni Mwezeshaji Waziwazi wa umbile la Kiyahudi Kwa Gharama ya Watu wa Jordan na Ummah na Dhidi ya Chaguo lake la Kuikomboa Palestina

Mnamo tarehe 8/11/2022, juu ya kadhia za ziada za Mkutano wa Kilele wa Tabianchi huko Sharm El-Sheikh, Jordan, Imarati na umbile la Kiyahudi zilitia saini mkataba wa maelewano (MoU) ili kuendeleza upembuzi yakinifu na "kushiriki katika kutengeneza ala muhimu katika zilizopangwa kwa wakati kwa ajili ya mkutano wa COP28” utakaofanyika Imarati mnamo Novemba 2023, kuanzisha miradi miwili tofauti, inayotegemeana na kuhusiana; kwa lengo la kuasisi kiwanda cha kusafisha maji katika Bahari ya Mediterania kwa badali ya kuanzishwa kwa kiwanda cha kuazalisha umeme safi nchini Jordan.

Soma zaidi...

Mkataba wa Maelewano na Usaidizi wa Kifedha kwa Jordan Udhibiti Hatari wa Kikoloni wa Marekani

Mnamo siku ya Ijumaa tarehe 16/9/2022, Naibu Waziri Mkuu wa Jordan na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni Ayman Safadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken walitia saini, jijini Washington, mkataba mpya wa maelewano kuhusu uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuhusu misaada ya kifedha ambayo Amerika inakusudia kutoa kwa Jordan kwa miaka saba ijayo, ukihakikisha kujitolea kwa Amerika kwa usalama na utulivu wa Ufalme huu.

Soma zaidi...

“Blackberry Wakati wa Uvamizi Haina Maana!” Utayari wa Dola ya Khilafah katika Kukabiliana na Maafa na Ajali

Kuporomoka kwa jengo la makaazi katika eneo la Al-Weibdeh katikati mwa mji mkuu, Amman, siku ya Jumanne, kumesababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine 10, katika hali isiyokwisha, huku msako wa kuwatafuta manusura ukiendelea kwenye vifusi. Kuna habari ambazo hazijathibitishwa juu ya uwepo wa zaidi ya watu 10 chini ya vifusi, ambao kati yao wako hai, na Manispaa ya Amman imeondoa watu kwenye majengo 4 karibu na jengo lililoporomoka.

Soma zaidi...

Rasimu ya Sheria ya Haki za Mtoto katika Baraza la Wawakilishi la Jordan ni Aina ya Vita Dhidi ya Uislamu na Lazima Ikataliwe

Haibishaniwi kwamba Sheria ya Haki za Mtoto iliyoagizwa kutoka UNICEF, moja ya mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa, ni sheria ambayo haina uhusiano wowote na haki za watoto katika Uislamu,na ni aina ya vita dhidi ya Uislamu kama mifano yake iliyotangulia ya sheria za haki za binadamu na CEDAW inayo husiana na wanawake, ambapo Magharibi inajaribu kuanzisha maadili ya urasilimali uliooza, ambayo ni kinyume na...

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu