Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  26 Rabi' II 1442 Na: 1447/02
M.  Ijumaa, 11 Disemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan
kwenda kwa vitivo vya Sharia na Waandaaji wa Kongamano la "Uhalisia wa Maji Nchini Jordan"

(Imetafsiriwa)

Chini ya uangalizi wa Waziri wa Wakfu na Masuala ya Matukufu ya Kiislamu, Dkt Muhammad Al-Khalayleh, vitivo vya Sharia katika vyuo vikuu vya Jordan, kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ), watafanya kongamano la kwanza kwa wanafunzi wa vitivo vya Sharia katika vyuo vikuu vya Jordan chini ya anwani: "Uhalisia wa maji nchini Jordan ... Changamoto na Masuluhisho kutoka kwa Mtazamo wa Kiisilamu." Ambalo litafanyika kwa kutumia programu ya Zoom mnamo Jumamosi tarehe 12/12/2020.

Kwa wakuu na madaktari wa vitivo vya Sharia ... na kwa waandaaji kongamano hili ... na kwa wataalam wa sayansi ya sheria:

Nyinyi mna karibia kufanya kongamano hili, ambalo litawakusanya wanafunzi wote wa vitivo vya Sharia nchini Jordan, kuzungumzia shida ya maji na masuluhisho yake kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu.Tunaweka mikononi mwenu vidokezo kadhaa ambavyo haviwezi kurukwa au kupuuzwa inapo zungumziwa shida ya maji nchini Jordan.

Na kabla ya hapo, tunashangazwa na ongezeko la shida ya maji kwa kushirikiana na shirika la Ujerumani na taasisi za kimataifa. Kwa kuwa tunazungumza juu ya kutatua shida kutokana na mtazamo wa Kiislamu, inahusu nini mashirika ya kimataifa kwa masuluhisho ya shida za Waislamu?! Je! Haitoshi kwamba mnatafuta kutatua suala la Palestina kwa msingi wa kanuni ya kimataifa, ambayo kwa kweli ni kuifuta kadhia hiyo, badala ya kuiangalia kwa mtazamo wa kisheria?!

Tukirurudi katika nukta muhimu zaidi, tunasema:

Kwanza: Hakika Uislamu umeyaorodhesha maji kuwa ni miongoni mwa mali ya umma ambayo Mtunzi wa Sheria (Shari') ameujaalia umiliki wake kwa jamii ya Waislamu, na akawajaalia washirikiane baina yao, na akawataza watu binafsi kumiliki. Mtume (saw) amesema:

»النَّاسُ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي الْكَلَأِ، وَالْمَاءِ، وَالنَّار«

"Watu ni washirika katika vitu vitatu: katika malisho, maji, na moto." Kwa hivyo, ni haramu kuyabinafsisha na kuyauzia kampuni maalum. Kama ilivyo nchini Jordan.

Pili: Shida ya maji nchini Jordan kimsingi ni shida ya kisiasa inayohusiana na kuasisiwa kwa Jordan kama umbile, mfumo wake wa serikali, na uhusiano wa watawala wake na Mayahudi. Jordan haitimizi wajibu wake wa kutoa maji muhimu na yanayofaa kwa watu wake, sio kwa sababu ya ukosefu wa maji nchini Jordan, bali kwa sababu imekuwa ikiunganisha maisha ya watu na maji kwa matakwa ya makafiri na Mayahudi na maslahi yao, kupitia makubaliano na mikataba, kuanzia miradi ya Kiingereza, kupitia mradi wa Kiamerika wa Johnston, na kuishia na makubaliano ya Wadi Araba pamoja na umbile la Kiyahudi; ambayo yaliwawezesha Mayahudi kupata mwanya wa kuvifikia vyanzo vya maji ya juu na chini ya ardhi ya Jordan.

Tatu: Umbile la Kiyahudi limechukua - na lingali linachukua - idadi kubwa ya maji ya Jordan, ima kupitia kuikalia kwake, makubaliano, au kwa wizi.

Ama kuikalia kwake, wakati Mayahudi walipovamia Golan, walipata udhibiti kamili wa vyanzo vya maji na vijito vya Mto Jordan (Hasbani, Baniyas, na Al-Dan), na walidhibiti zaidi ya nusu ya urefu wa Mto Yarmouk.

Ama kuhusu makubaliano hayo, hakuna ushahidi wowote uliomo katika makubaliano ya Wadi Araba na kiambatisho cha maji, kwa mfano ilikuja katika Kifungu cha 6 cha kiambatisho cha makubaliano ya maji: (Pande hizo mbili zinakubaliana juu ya mgawanyo sawa kwa kila mmoja wao, katika maji ya mto Jordan na Yarmouk na kutoka kwa maji ya chini ya ardhi ya Wadi Araba).

Ama kuhusu wizi, ilielezwa katika ripoti moja ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mnamo 1992 M, (kwamba Israeli inavuta maji mengi hadi kwenye kituo cha kitaifa cha usafirishaji maji kuliko ilivyokubaliwa na zaidi ya maelezo ambayo kwayo kilianzishwa, na inaielekeza mito yenye chumvi na isiyofaa hadi sehemu ya kusini ya mto – yaani Mto Jordan - ili isichafue maji ya Tiberia).

Nne: Waislamu wametambua umuhimu wa maji kama jambo muhimu katika kujenga dola na jamii tangu kuanzishwa kwa dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina. Kutoka kwa Uthman bin Affan, (ra): Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokuja Madina, kulikuwa na kisima kimoja pekee kilichokuwa kikitumika, kisima cha Rumah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:

«مَنْ يَشْتَرِيهَا مِنْ خَالِصِ مَالِهِ فَيَكُونُ دَلْوُهُ فِيهَا كَدِلَاءِ الْمُسْلِمِينَ، وَلَهُ خَيْرٌ مِنْهَا فِي الْجَنَّةِ...»

Yeyote atakaye kinunua kwa pesa zake mwenyewe ndoo yake itakuwa ndani yake kama ndoo za Waislamu (yaani, kipeane kisima kwa Waislamu na ushirikiane nao katika matumizi) na atakuwa na kheri zaidi ya hicho Peponi.” Ama nchini Jordan, wamelipa uwezo umbile nyakuzi wa maji ya Waislamu nchini Palestina na Jordan, na hata wamewazuia Waislamu kutokana na kutumia maji yao ili watawala watimize makubaliano yao na Mayahudi.

Tano: Suluhisho la suala la maji nchini Jordan lazima liwe suluhisho msingi ambalo lazima liwe katika kiwango cha eneo na Umma, sio kwa kiwango cha mitaa au jimbo. Utajiri wa maji katika eneo hili ni mali ya umma huu na washirika wake wote wanapaswa kufaidika nayo, kama alivyosema Mtume (saw):

«مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ كمَثَلِ الْجَسَدِ الوَاحِد؛ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

"Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuoneana huruma kwao, na kuoneana upole kwao ni kama mfano wa mwili mmoja; pindi kiungo kimoja kinaposhtakia maumivu, mwili mzima unaitikia kwa kukosa usingizina homa". Basi mwili huu mmoja unapaswa kuungana pamoja ndani ya umbile moja la kisiasa ili kuliondoa umbile la dola ya Kiyahudi. Na kwa hivyo, shida ya maji itatuliwa kimsingi nchini Jordan na eneo zima.

* Kwa kumalizia: Tunatoa angalizo kwenu kwa kijitabu kilichotolewa na Hizb ut-Tahrir mnamo 1999 chini ya kichwa: (Shida ya Maji Mchini Jordan, Suluhisho Lake ni Nini?), Ambapo ndani yake shida hii imeelezewa pamoja na suluhisho lake, na kufafanuliwa uhalisia wa maji, hifadhi yake na usambazaji wake nchini Jordan, na kulinganisha kile ilicho nacho Jordan kuhusiana na hifadhi, kile watu wanachohitaji, na kile kinachoporwa, yote haya yakiwa na nambari na takwimu zilizoandikwa.

Kwa kutamatisha, tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

]وَإِذْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ]

Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha.” [Aal-i Imran: 187].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu