Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  13 Rabi' I 1442 Na: 1442 / 05
M.  Jumamosi, 31 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

Ndugu Jihad Abdulqadeem Zalloum

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً﴿

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Jordan inaomboleza kwa Umma jumla wa Kiislamu, Ndugu Jihad Abdulqadeem  Zalloum, mmoja wa mashababu wa Hizb ut-Tahrir, na mtoto wa Amiri wetu na Sheikh aliyetangulia, marehemu Abdulqadeem  Zalloum, aliyefariki siku hii ya Jumamosi tarehe kumi na nne ya Rabi al-Awwal 1442 H sawia na 31/10/2020 M Jijini Amman.

Marehemu Jihad (Abu Al-Amin) alikuwa mbebaji wa ulinganizi kwa haki ya kutoa maisha yake na umri wake katika da'wah hii, japo hatumtakasi mtu yeyote kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo alikuwa mrithi bora wa mtangulizi bora.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Aliye juu, Muweza, amfinike kwa upana wa rehema yake, na apanua mlango wake, akirimu mashukio yake, na amuingize Peponi ya Firdausi Kuu pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, wema na hao ni marafiki wazuri, na atupe sisi na jamaa zake subira, uvumilivu na faraja njema.

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

 "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea." [Al- Baqara: 156]

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Jordan

- Kalima katika mazishi ya Ustadh Jihad Abdulqadeem Zalloum, Mwenyezi Mungu amrehemu -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu