Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  26 Sha'aban 1442 Na: 1442 / 19
M.  Alhamisi, 08 Aprili 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali nchini Jordan Inakabiliwa na Migogoro Mfululizo, Yenye Kukaba Koo
(Imetafsiriwa)

Katika siku za hivi karibuni, watu walifuatwa na msururu wa matukio yaliyoanza Jumamosi 4/3/2021, yakidai kwamba usalama na utulivu wa serikali umefichuliwa kwa njama, ambayo ilisababisha kampeni ya ukamataji na kutolewa kwa taarifa zilizoambatana na kuibuka kwa uvujaji na kisha watu wa katikati. Mnamo Jumatano 7/4/2021, mkuu wa serikali, Mfalme Abdullah II, alitoa ujumbe wa maandishi uliochapishwa kwenye vyombo vya habari;  unaosema, "Fitina imefikia mwisho, na kwamba tunataka baba yetu, awe salama na thabiti."

Sio siri kwa wale ambao wafuatilia kwa uangalifu na kwa umakini matukio ambayo serikali nchini Jordan imekuwa ikikabiliwa nayo - tangu kuzaliwa kwake mikononi mwa Waingereza – kutokana na mfululizo wa migogoro inayotokea yenye kukaba koo, na huu hautakuwa ni mgogoro wake wa mwisho, kwa sababu kile ambacho serikali hii inateseka nacho ni kuwepo migogoro uwepo, utawala, siasa, uchumi ... nk, Ni matokeo ya kimaumbile ya kukataa kwake hukmu za Uislamu katika kuendesha maisha ya watu binafsi, jamii na dola, na kujisalimisha kwake kwa ushawishi wa mkoloni kafiri ambaye alizigawanya nchi za Uislamu na kuimega Jordan kutokana na asili yake ya kimaumbile, Ash-Sham.

Kukabiliana na mgogoro huu, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir / Wilayat ya Jordan, tungependa kufafanua mambo yafuatayo:

Kwanza: Serikali nchini Jordan inazidi kuzorota katika mgogoro wa utawala wake na imeporomoka bila shaka. Ufisadi katika utawala na ucheleweshaji ndani ya dola unatokana na fikra ambao mfumo huu unasimama juu, ambayo ni kutenganisha dini na maisha, na katika utawala ambao ulitegemea Uingereza na baada ya hapo kwenda Amerika, ambazo ni nchi mbili za kikoloni ambazo zinavutana juu ya machumo katika nchi yetu, serikali inayotawala kiasili hali yake imesimama juu ya utekelezaji na uhakikishaji wa maslahi ya Magharibi, ambayo huipa msaada wa kuendelea kutawala, na serikali hii hajakufanya na kamwe haitafanya kazi kwa maslahi ya Umma na watu wake kwa sababu haitegemei Umma katika uwepo na uhalali wake, na ndio msaada wa kimaumbile kwa mtawala yeyote.

Serikali inayotawala katika nchi yetu unaunyang'anya Umma mamlaka yake, na watu wenye nguvu hujaaliya mamlaka mikononi mwa mtawala, ambaye naye hutarajia kuhifadhiwa kiti chake na Magharibi kikoloni, iwe ni Ulaya au Amerika, na mapambano juu ya sheria za mchezo wenyewe hazibadilishi hali ya Umma kwa chochote, haswa ndani ya familia inayotawala na kwa msingi wa kumtumikia kafiri. Ukweli zaidi wa hili ni kwamba hali hiyo ilifikia mwamba kwa karne moja kupitia mfanyakazi anayesubiri maaagizo ya ubalozi wa Uingereza na michezo yake.

Pili: Ni makosa kwa msimamo kuzidiwa na mazungumzo juu ya kubadilisha sura ya mtawala au mwelekeo wake, na kubakia hai kwa kanuni, sheria na katiba kwani zimetungwa na wanadamu, au kutaka mageuzi ya baadhi tu ya nidhamu na kanuni, kwani hivi huchukuliwa kuwa viraka tu ambavyo haviwezi kuleta athari yoyote. Hakika mageuzi na mwamko huja kupitia njia ya fikra ya kisiasa ambayo inasimama juu yake hukmu, kwa maana nyengine, ni kuujenga utawala juu ya Aqeeda ya kiakili ambayo sheria na kanuni zinatokana kwayo, na mwamko hauwezi kutokea duniani isipokuwa juu ya msingi huu, na mtu yeyote haweza kuleta mwamko na kuufikia isipokuwa kwa kutembea katika njia hii.

Na serikali tawala hapa inatafuta maslahi yake, ambayo kubakia madarakani na kuihudumia Magharibi kafiri bila kujali sura ya mtawala, kwa hivyo njia hiyo ni njia ya mababa na mababu, na njia yao haikuwa ila ya khiyana, usaliti, kujisalimisha na kusalimisha uwezo wa nchi kwa Magharibi, kupora utajiri wake na kukiuka ardhi zake.

Tatu: Inasikitisha kwamba wale wanaoitisha harakati mitaani kuna wale wanaoidhani vizuri Amerika, Uingereza au wengineo, na wanafikiria kuwa nchi hizi zitawaacha watu wa Jordan kutibu migogoro yao tiba ya kimsingi au kuutibu mzozo wa kisiasa tiba ya mafanikio, kwa hivyo lazima iwe wazi katika akili za watu wa Jordan, kuwa nchi hizi hazitarajiwi kutoka kwao mema, kwani wao ndio msingi wa ndwele na kujifunga nazo ni kifo kibaya. Badala yake, wataunda vizuizi na shida anuwai za kuzuia mizozo ya nchi yetu kutatuliwa, na watafanya kazi ya kueneza na kukuuza fikra ambazo zinasababisha machafuko na ghasia na kuongeza kina cha mwanya kati ya watu wa Jordan.

Nne: Mageuzi ambayo Umma lazima uyatafute na kujitahidi kuyafikia bila ya uchovu au kuchoshwa ni mageuzi ya serikali kutoka mizizi yake, mageuzi kamili ya kimapinduzi ili nidhamu za sasa zilizotungwa na wanadamu zisibakie athari, na hii ni pamoja na kubadilisha katiba, sheria na mifumo yote ya maisha, na kuchukua nafasi ya mfumo ulioanzishwa na Mtume (saw) mjini Madina, mfumo wa Uislamu, ili imani ya Kiislamu iwe ndio msingi ambao katiba, sheria na kanuni zote zinatokana nao; Na hiyo ni kwa kumchagua khalifa wa Umma wote wa Kiislamu umpe ahadi ya utiifu (bay'ah) ili auhukumu kwa Kitabu na Sunnah kwa mkabala wa utiifu kwake kwa mepesi na mazito, khalifa ambaye maelezo ya Mtume yanapatikana kwake, pindi (saw) aliposema:

«خِيَارُ أَئِمَّتِكُمُ الَّذِينَ تُحِبُّونَهُمْ وَيُحِبُّونَكُمْ وَيُصَلُّونَ عَلَيْكُمْ وَتُصَلُّونَ عَلَيْهِمْ»

“Viongozi wenu wema ni wale ambao mnawapenda na wanakupendeni, na wakuombeeni kwa Mwenyezi Mungu nanyi mnawaombeeni kwa Mwenyezi Mungu.” Khalifa ambaye atakuwa ngao ya kinga kwa Umma, sio mwenye kuzipora kheri zake, na mwenye kuukandamiza. Mtume (saw) amesema:

«وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na kujihami kwake.” [Imepokewa na Al-Bukhari].

Enyi watu wetu katika ardhi ya Hashd na Rabat (Mkusanyiko na Kituo):

Hakika inasikitisha kwamba nchi yetu ni uwanja wa mapambano yanayohusiana na balozi za kigeni, ambao hutekeleza ajenda zao, hula njama dhidi ya nchi na waja, wana uadui na Uislamu na nidhamu zake, na hawajali juhudi zozote za kuwadhalilisha watu wao na kupora rasilimali zao, na nyinyi mnao uwezo wa kuwabadilisha, na mabadiliko hayatakuwa ya kweli isipokuwa serikali zote za batili za kibinadamu zitakapoondolewa na mitindo anuwai ya serikali kukataliwa, pamoja kuanzia ufalme, ufalme wa kikatiba na jamhuri, na nyuzi za balozi ambazo zilizovisogeza vinyago kwenye jukwaa kukatwa, na hili haliwezi kufanywa ila kwa kupitisha kutabanni Uislamu mtukufu, kuwa na utambuzi nao, na kufanya kazi kuuleta madarakani chini ya uongozi wa Hizb ut-Tahrir. Na hilo litakuwa kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itauweka Uislamu katika upande wa utabikishaji, kuwang'oa vibaraka, kuwashinda wale wanaopanga njama, kuhifadhi utajiri wa nchi na kuling'oa umbile la Kiyahudi, basi kuweni pamoja na wale wanaofanya kazi kwa ajili yake.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu