Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  2 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 / 25
M.  Jumanne, 06 Julai 2021

Tanzia ya Wabebaji Ulinganizi Wawili

﴿مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

Hizb ut Tahrir Wilaya ya Jordan yawaomboleza wawili miongoni mwa mashababu wake wema, wabebaji ulinganizi:

Sheikh Adeeb Ahmad Rais Al-Shishani (Abu Ahmad Al-Shishani)

Na Ustadh Muhammad Khitab Masad Al-Umari (Abu Iyad Al-Umari)

Ambao waliondoka kwenda katika rehma ya Mwenyezi Mungu (swt) siku ya Jumatatu 5/7/2021 M, baada ya miaka mirefu ya mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa dhidi ya tawala za twaghuti, wakiwa wameivaa haki na ari ya kubeba ulinganizi wa kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Sheikh Abu Ahmad Al-Shishani, na Ustadh Abu Iyad Al-Umari, Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu wote wawili, walibeba da'wah ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu katika safu za Hizb ut Tahrir, na walikutana na mateso na kifungo walichokuwa wamevumilia, na walibaki imara juu ya haki, wakipokea bishara njema ya nusra, wakidumu katika kuamrisha mema na kukataza maovu, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja na hali wao wawili walikuwa hivyo, na roho zao zikatoka kwenda kwa Muumba wake.

Twamuomba Mwenyezi Mungu awafunike kwa ukubwa wa rehema zake na awaingize katika Pepo Yake pana na awalipe kwa niaba yetu na kwa niaba ya Uislamu na Waislamu na malipo bora zaidi.

Ni cha Mwenyezi Mungu kile alichotoa na ni cha Mwenyezi Mungu kile alichochukua, na hatusemi isipokuwa tu yale yanayomridhi Mola wetu.

﴿إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴾.

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea." [Al-Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilaya Jordan

- Kalima katika Mazishi ya Ustadh Adeeb Al-Shishani (Abu Ahmad) -

- Kalima katika Mazishi ya Ustadh Ahmad Khitab Al-Umari (Abu Iyad) -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu