Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  12 Shawwal 1445 Na: 1445 / 15
M.  Jumapili, 21 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Jordan Haina tena Mahali pa Kuficha Utetezi Wake wa Umbile la Kiyahudi

Kuweka Matendo katika Mizani ya Uislamu Inaongoza Dira Yako kwenye Suluhisho la Shariah
(Imetafsiriwa)

Habari na taarifa mara kwa mara katika vyombo vya habari rasmi na majukwaa ya mitandao ya kijamii, chaneli za satelaiti zilikuwa zimejaa mahojiano ya ndani na kimataifa kutoa maoni juu ya matukio yaliyofanyika katika kanda hii tangu vita vya Gaza. Zilikuwa zinakinzana na za uwongo hivi kwamba walishangaza watu kufuatia kadhia za Ummah na nchi zao. Maoni yalitofautiana na kuzidi kutofautiana katika utafutaji wake wa hatua sahihi na kuweka dira kuelekea njia ya ukweli ya Sharia, kutoka na msimamo ambao utawaokoa kutoka kwa udhalilishaji wa maadui na njama za watawala, na kurudisha fahari na hadhi ya Ummah ambayo inastahili kama ilivyokuwa mstari wa mbele katika mataifa. Hii ni kwa sababu tu Waislamu walipitisha viwango vingi katika uamuzi wao wa matukio, na hivyo kutofautisha katika mtazamo wao juu ya suluhisho na hatua za kivitendo kutoka kwa shida zao na ugumu ambao wanaishi, kutoka kwa utawala wa maadui wa makafiri na udhibiti wake juu ya uwezo wake, na uwezeshaji wa watu wa chini kabisa, Mayahudi, kudhibiti nguvu kubwa za Ummah. Umbali wa watu kutoka kwa sheria na viwango vya Uislamu, na kufuata kwao uzalendo na utaifa kwa msingi ambao nchi yao iligawanywa, ndio sababu ya moja kwa moja ya kutawanyika kwa mawazo yao na kupooza kwa nguvu zao na mwelekeo wa kisiasa katika kutafuta suluhisho bora, na kwa hivyo wakapoteza njia yao ya wokovu.

Leo, hakuna utawala au serikali inayotawala na Uislamu au kutekeleza hukmu za Sharia; ambayo wengi wa watu wao wanaiamini na ambao hisia zao zimeungana pambizoni mwa imani yake, na kutamani kuzitekeleza hukmu za Uislamu katika dola moja ya Kiislamu. Haya ndio maoni ya Waislamu wengi ulimwenguni, lakini wanakengeuka kutokana na njia ya Sharia inayoongoza kwenye lengo kuu kama lilivyoainishwa na Uislamu!

Kwa hivyo, ufahamu wa kisiasa na njia ya Kiislamu ya mabadiliko ni miongoni mwa mahitaji ambayo yameunganisha Ummah katika juhudi zake kuelekea ukombozi kutoka kwa wale ambao wanayafunga minyororo mamlaka yake na dola kubwa, haswa itikadi ya kisiasa ya Uislamu, kwa hivyo wanaamua kumuangamiza mtu yeyote anayesimama dhidi ya mradi wake mkubwa wa kuregesha dola yake tukufu, dola ya Khilafah, iwe ni dola za kikoloni za kikafiri au serikali vibaraka ambazo zimekuwa zikiunyonga Ummah kwa zaidi ya karne.

Miongoni mwa misingi na maregeleo yanayohusiana na Vita vya Gaza baada ya shambulizi la Oktoba 7, 2023, na kuingia nusu kwa Iran katika mandhari ya matukio na athari za baada yaye, ni:

- Hakuna serikali yoyote katika nchi za Kiislamu zilizoingia madarakani kupitia njia halali ya Sharia, lakini badala yake zilinyakua mamlaka ya Ummah na mamlaka ya watu wake, kwa hivyo hazipaswi kutiiwa. Zote haziufanyi Uislamu kuwa kigezo cha sera zao za ndani au za nje, lakini badala yake zinasimama upande wa maadui wa Ummah, mkoloni kafiri Magharibi, katika utiifu wake kwake na kuiwezesha kudhibiti nchi za Waislamu.

- Iran imekuwa katika mzunguko wa Marekani na imeweza kufikia maslahi yake katika kanda hii tangu ilipoanza kutawala, kama ilivyotokea nchini Afghanistan na Iraq kwa kutambuliwa kwa viongozi wao, na michezo ya kisiasa ambayo inafanyika katika nchi za kanda hii. Dori yake ya jinai nchini Syria bado inaendelea kumhami dhalimu wa Ash-Sham kwa kuitumikia Marekani, kwa badali ya kufikia baadhi ya maslahi ya Iran katika ujanja wa kijeshi na kisiasa kwa miongo kadhaa. Droni za Iran na makombora 'dhidi ya umbile la Kiyahudi chini ya macho ya Marekani na udhibiti wake wa wimbo kati ya umbile la Kiyahudi na Iran ni moja tu yao, haikunyosha hata kidole kuwanusuru watu wa Gaza.

- Serikali nchini Jordan ni serikali kibaraka, inayofanya kazi kwa lengo la uwepo wake ili kulilinda na kulipa tamkini umbile la Kiyahudi. Itabakia madarakani maadamu bado inahitajika. Transjord ilianzishwa kama chombo kwa ajili ya misheni hii, watu wa Jordan hawapendezwi na uwepo wake, ni pale iko tu pale kuunganisha umbile la Kiyahudi kijeshi na kiusalama, na inaruhusu ardhi yake kulengwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, na kambi za Ujerumani, ambazo kwazo inazindua utekelezaji misheni kulinda maslahi yao. Ukweli kwamba serikali nchini Jordan ilizikabili droni na makombora ya Iran yaliyoelekezwa kwa umbile la Kiyahudi inaonyesha dori ya serikali na urefu wa usaliti kwa umma katika kulihami na kulilinda umbile la Kiyahudi, ambalo kila mwenye macho na ufahamu hawezi kukataa.

- Kwa mnasaba huu, majukwaa ya mitandao ya kijamii yalijazwa na makala, mahojiano, na habari za kimataifa ambazo zinaonyesha vitendo vya serikali, kama vile makala ya David Hearst katika Jicho la Mashariki ya Kati, na mahojiano ya George Galloway na Scott Ritter. Katika utangulizi uliotangazwa na serikali ya Jordan hadharani chini ya kisingizio cha kuwalinda raia wake na anga zake, ambazo hapo zamani zilikuwa lengo wazi kwa vikosi vyote vya maadui wa Magharibi, wakiongozwa na Marekani na umbile la Kiyahudi, kama ilivyoelezwa katika Jarida la Arab Post katika uchunguzi maalum kuhusu uwepo wa ndege mbili za Kiyahudi zinazozunguka anga za Jordan wakati wa majibu ya umbile la Kiyahudi nchini Iran alfajiri Ijumaa iliyopita, kutoka kaskazini na kusini.

- Vitendo vya serikali za Kiarabu, haswa zile zinazozunguka Palestina na zile za karibu nayo, hazina afadhali katika kufeli kwao na utiifu kwa kafiri Magharibi katika msaada wao kwa umbile la Kiyahudi, iwe kupitia uhalalishaji mahusiano au kuzingirwa kwa watu wa Gaza, na wakati huo huo kulipa umbile la Kiyahudi ukanda wa biashara kutoka Imirati hadi kwenda Saudi Arabia kupitia Jordan, ili kuliokoa kutokana na kuzingirwa kwa Bahari Nyekundu.

- Katika wakati ambapo sababu ya kushindwa kwake mara kwa mara imekuwa wazi kwa Ummah, ambayo ni mifumo yake ya utawala, hairuhusiwi kwa mtu yeyote au watu wa kanda hii kujipanga upande wa serikali hizi kwa msingi wa uzalendo wa kitaifa katika bendera zake, kuitukuza mipaka yake, na kuwatukuza watawala wake vibaraka, au kusimama pamoja nao, na kwa hivyo kuwa mtu anayewasaidia wasaliti wakandamizi. Huu ni uzalendo ambao watawala vibaraka, pamoja na wataalamu wa vyombo vya habari, wasomi, mawaziri, na mabingwa wabunge, na ambao misingi yao imeasisiwa na kafiri Magharibi ili kuendeleza msambaratiko na mgawanyiko wa Ummah na kuzitetea serikali hizi ambazo ndizo njia za kubomoa nchi za Waislamu, kulinda na kulipa tamkini umbile la Kiyahudi, nyuma yake Marekani na Ulaya, na kushindwa kuwanusuru watu wa Palestina, na hata kushindwa kuifurusha Marekani, washirika wake na kambi zao kutoka nchi za Waislamu.

Enyi watu ... Enyi watu wetu nchini Jordan:

Kutafuta masuluhisho yanayotokana na uhalisia fisadi na mchungu, ambao ni udhibiti wa wakoloni makafiri na umbile la Kiyahudi, na kujisalimisha kitumwa kwao ambako watawala wenu wamekumakinisha, uaminifu wao katika kulinda umbile la Kiyahudi, uporaji wa utajiri wenu, kukosa kuwanusuru watu wa Palestina, na masuluhisho yanayotokana na msingi wa uzalendo wa kitaifa ambao hugawanya na kutawanya, kuisalimisha nchi yenu kupitia kuanzisha kambi za wakoloni na mwaliko wa watawala wenu na ridhaa yao, yote haya yataongeza tu udhalilifu na utumwa wenu.

Kurudi kwenu kwa Dini yenu, Uislamu, na utabikishaji wa sheria zake kupitia kusimamisha dola yake, ndio itakayofikia maadili matukufu ya Uislamu. Ndani ya dola ya Kiisilamu imo fahari yenu na hadhi yenu, na kupitia kwayo mutaachwa huru kutokana na utumwa wa watawala wenu vikaragosi, na kupitia kwayo majeshi yenu yataongozwa ili kuzikomboa ardhi za Waislamu zilizokaliwa kimabavu nchini Palestina na kwengineko. Umbile la Kiyahudi litang’olewa milele na wakoloni makafiri watafurushwa, na mutapata radhi za Bwana wa Walimwengu, na ulimwengu utabarikiwa kwa rehma na uadilifu baada ya dhulma na uovu kuenea ndani yake.

[مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعاً إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَكْرُ أُولَئِكَ هُوَ يَبُورُ]

“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na a'mali njema Yeye huitukuza. Na wanao panga vitimbi vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya hao vitaondokea patupu.” [Fatir: 10]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu