Afisi ya Habari
Kenya
H. 18 Dhu al-Qi'dah 1442 | Na: 1442/13 H |
M. Jumanne, 29 Juni 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maisha Chini ya Urasilimali ni Mateso na Yamekuwa ni Mfano Kamili ya Jahannam Ardhini
Hizb ut Tahrir / Kenya inashtushwa na kiwango cha watu waliotekwa nyara kote nchini. Visa vilivyorekodiwa na maafisa wa usalama wa Kenya vimefichua kwamba wahalifu wamejitokeza kuwateka nyara wasichana na watoto na kisha kuitisha pesa kwa familia zao. Video zimezuka mitandaoni zikionyesha wahasiriwa wakiteswa, kunyanyaswa na kuacha sio hai wala maiti. Katika suala hili tungependa kusema yafuatayo:
Hata kama visa hivi vinaenea sana na kwa kweli vinasababisha hofu, hata hivyo tungewaonya umma kwa jumla kwamba sio lazima kuongeza hofu kwa kueneza habari bila ya uchunguzi barabara wa kutegemewa kwake. Hili ni mojawapo ya mafundisho ya kina ya Uislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ)
“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.” [Al-Hujuraat 49:6].
Mtindo huu wa kusikitisha wa kupotea, kuuawa kwa watoto, wasichana na watu binafsi kwa kweli umesababisha hofu na wasiwasi kwa Wakenya. Kwa familia za Waislamu nchini, hili ni janga la nyongeza kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipitia mauaji, ya kuenea, na yaliyopangwa kwa uangalifu kinyume na sheria yanayofanywa mara kwa mara na polisi wa Kenya chini ya 'Vita dhidi ya Ugaidi'. Hii ni dalili kwamba maisha chini ya Urasilimali ni mateso na yamekuwa ni mfano kamili ya Jahannam ardhini.
Ugumu wa maisha unaohusishwa na Urasilimali umechochea uwepo wa visa hivi katika jamii kwani kila mtu amepoteza mwelekeo na hutumia njia yoyote ovu kutafuta "maisha bora". Wazazi pia hawana muda wa kutosha wa kukaa na watoto wao kwani wanajikuta wakifuatilia maisha. Tungependa hata hivyo kuwakumbusha wazazi kwamba watoto wana haki ya kuwa salama, kuamiliwa kwa mapenzi na kulindwa dhidi ya ukatili na unyanyasaji.
Hatimaye, tunasema kinaganaga kuwa visa hivi havitokei tu nchini Kenya pekee lakini ulimwenguni kwa jumla. Katika suala hili, Waislamu wanapaswa kuregelea jukumu lao zito la kufanya kazi kwa lengo moja tu la kusimamisha tena Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume katika moja ya nchi nyingi za Waislamu, hiyo ndiyo nidhamu pekee ya utawala yenye nguvu ya kulinda raia dhidi ya aina yoyote ya ukatili.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |