Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  13 Jumada I 1444 Na: 1444/04 H
M.  Jumatano, 07 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hazina ya ‘Hustler’: Tungo Nyengine Mpya ya Mfumo wa Kibepari Ulioshindwa Kusimamia watu Kiuchumi

(Imetafsiriwa)

Katika hatua ya kuwapa mikopo wafanya biashara wadogo wadogo ambao wamekuwa wakitaabika kuchukua mikopo katika benki kubwa, serikali imezindua mfuko wa fedha unaojulikana maarufu Hustler Fund ambapo baada tu ya uzinduzi huo takriban Wakenya milioni 17 tayari wamechukua mkopo huo kwa muda tu wa saa moja kwenye siku ya kwanza ya uzinduzi huo. Kipindi cha uregeshaji wa mikopo kitapunguzwa hadi siku 14 katika mpango unaoonekana kufungua dirisha kwa wafanyi biashara wadogo kupata mkopo wa bei nafuu. Mfuko huo uliozinduliwa, utaona wakopaji wa kiwango cha chini wakipata Sh 500 huku kiasi kikubwa zaidi cha nyongeza kitakuwa Sh 50,000 kwa riba ya asilimia nane.

Harakati ya Hizb ut Tahrir Kenya ingependa kubaini yafuatayo:-

Ukweli kwamba kumekuwa na benki zinazotoa mikopo hiyo hiyo ya riba na ambayo imezidisha ugumu zaidi kwa raia wa kawaida na hatimaye kuwanufaisha wale wakopeshaji (wadai), inathibitisha kufilisika kisera kwa siasa na uchumi wa mfumo wa Kibepari. Kwa hivyo hazina hii ya mikopo inayotolewa na serikali ya sasa si lolote ila ubadilishwaji majina mapya ya mikakati ile ile ya zamani hivyo katu haitotatua kimsingi matatizo ya kiuchumi ambayo yamekita mizizi ndani ya taasisi za kifedha za kibepari.

Chini ya mfumo unaotegemea pesa za makaratasi (Fiat-Monetary), ambazo kiasili hazina thamani ya kidhati ila tu kupitia kanuni za kiserikali, pesa imefanywa ni bidhaa inayouzwa kwa bei ya riba ambayo inatumiwa na mabepari kunyonya na kuzuia raia wa kawaida kujikomboa kiuchumi. Mienendo ya mfumo wa kiuchumi wa kibepari, Riba hubadilisha sura yake mbaya mara kwa mara kwa kubadilisha kauli mbiu kama hii ya sasa ‘Hustler Fund’.

Matatizo ya kiuchumi ya raia hayatatatuliwa kwa kutegemea mfumo wa mikopo ya Riba bali ni kwa kupita utekelezwaji wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu na hapo ndio matatizo hayo yatatatuka kwani umeharamisha vikali riba kwenye miamala yote ya kifedha. Fauka ya haya, kwa kuwa Uislamu unaangalia tatizo la kiuchumi ambalo linapaswa kushughulikiwa ni ugawaji/usambazaji wa rasilimali. Kwa maana hii Khilafah kama serikali huwajibishwa kuchukua sera za kiuchumi zinazolenga kudhaminia kila raia waweze kukimu mahitaji yao msingi sambamba na kuwawezesha kufikia kukimu mahitaji ya ziada.

Tamati tungependa, kunasihi kwa dhati jamii yote kujiweka mbali na miamala yote ya kifedha ya riba kwani Mwenyezi Mungu (swt) ameukemea kwa ukali uovu huu pale aliposema:

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لاَ يَقُومُونَ إِلاَّ كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُواْ إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىَ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿

“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.” [Al-Baqara: 275]

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu