Afisi ya Habari
Kenya
H. 27 Jumada II 1444 | Na: 1444/05 H |
M. Ijumaa, 20 Januari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nidhamu Mbovu ya Kijamii ya Kibepari ndio Kiini cha Machafu ya Kijamii
(Imetafsiriwa)
Utafiti wa serikali wa hivi karibuni umefichua kusheheni pakubwa mahusiano ya nje ya ndoa ambapo inatajwa kuwa wanaume walioko kwenye ndoa wanatoka nje ya ndoa zao kwa kuwa na wapenzi saba huku wanawake nao wakiwa na wapenzi wawili. Aidha, utafiti huu ukadokeza majimbo yanayoongoza katika visa vya kwenda nje ya ndoa.
Kwa haya, sisi katika Hizb ut-Tahrir Kenya tungependa kubaini yafuatayo:
Chini ya mfumo wa Kisekula na fikra za Kiliberali, uzinzi, uasherati na ukahaba na mengine mengi machafu huwa ni yenye kukubalika kijamii, kitamaduni na hata kikanuni. Usekula hubeba fikra finyo za uhuru wa kibinafsi na uhuru wa kujumuika ambao huwa ndio nishati inayosukuma watu kujihusisha na mahusiano ya nje ya ndoa zao pasina na kuwa na hata chembe ya haya. Kwa maana hii, ndani ya mazingira haya machafu, mahusiano ya nje ya ndoa ni mojawapo ya majanga ya kifamilia.
Mfumo wa Kijamii wa Kirasilimali umeharibu ndoa kwa utaratibu, umeharibu uzazi, na kuchochea kuvunjika kwa utengamano wa Familia. Katiba za kilimwengu pia zimeshindwa kutangaza waziwazi uhalifu wa uzinzi na ukahaba ambao ni biashara inayofanywa peupe ndani ya tawala za kisekula. Zaidi ya hayo, sheria ya Kimataifa ya haki za binadamu inawapa wanaharakati kama vile wanaharakati wanaotetea haki za wanawake mfumo dhahania wa kutetea kikamilifu maovu haya hivyo kuushambulia Uislamu ambao umeharamisha zinaa na kuutaja kuwa ni njia mbovu.
Nidhamu ya Kijamii ya Kiislamu imeweka misingi inayolenga kuunda jamii yenye mtazamo sahihi wa mahusiano baina ya wanaume na wanawake unaolenga matangamano mema baina ya jinsia hizo mbili ukiwaongoza katika kulinda heshima yake. Kwa hiyo, pamoja na utekelezaji wa kidhati na utekelezwaji wa maadili na sheria za taratibu ya kijamii ya Kiislamu, mtazamo wa jamii kuhusu uhusiano kati ya wanaume na wanawake uko mbali na kushinikizwa na kipengele cha maingiliano tu ya kimwili na starehe. Zaidi ya hayo Uislamu umeharamisha uzinzi na matendo yote machafu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
﴾وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا﴿
“Wala msikaribie Zina. Hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa.” [Al-Isra: 32]
Uislamu ndio mfumo uliofanya uchajimungu uwe ndio nishati ya mtu inayompelekea kujizuia sio tu na uzinifu bali machafu yote kwa ujumla. Sheria ya Kiislamu imewajibisha wanaume na wanawake kujipamba na sifa ya haya inayowafanya wajiepushe na kila ovu bali wajifunge kikamilifu na sheria za Mwenyezi Mungu zinazoambatana na maisha yao ya kijamii. Katika Uislamu, ndoa hufungwa kwa lengo la kutafuta stara, kukidhi hisia za kimwili ili kuwe na utulivu huku ikiangaliwa zaidi kama njia itakayoletea mafanikio makubwa ya kijamii.
Kuzuia na maovu haya ya kijamii, jamii inapaswa kukataa hulka na mawazo finyo ya kiliberali yanayolinganiwa na Urasilimali na siasa yake ya Kidemokrasia. Wanapaswa pia kufanya kazi ya kuusimamisha Uislamu na mfumo wake wa utawala nao ni Khilafah kwa njia ya Utume.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |