Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  10 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444/12 H
M.  Jumatano, 28 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tunawapa Salamu za Idd ul-Adha

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya inapenda kutoa salamu za dhati za Idd ul-Adha iliyobarikiwa kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa jumla. Tunatoa pongezi zetu kwa watoto wa kiume na wa kike wanaofanya kazi bila kuchoka kuelekea kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Pia tungependa kufikisha salamu zetu za dhati kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah na kwa Waislamu wote katika Idd hii yenye baraka.

Idd imeregea na damu zetu hazijaacha kutiririka kama mito! Imeregea, huku vilio vya Waislamu vikisikika kila mahali! Wanawake wetu wamepaza sauti zao zilizojaza anga Ewe Mu’tasim!! Bila majibu isipokuwa kejeli kutoka kwa wakoloni pamoja na vibaraka wao katika Ardhi za Kiislamu! Nchini Kenya, kama sehemu nyingine yoyote ya ulimwengu Idd inakuja huku gharama ya maisha ikiwa imepanda ilhali maumivu zaidi ya ushuru yanawekwa kwa Wakenya wa kawaida kama inavyodhihirika katika sheria mpya katili ya fedha!

Idd hii iliyobarikiwa inapaswa kutukumbusha mtihani mkubwa kwa Ibrahim (as) na utayari wake mkubwa wa kujitolea. Leo watetezi wa Khilafah wanakabiliwa na mateso ya moja kwa moja kutoka kwa utawala dhalimu kote duniani. Hakika tuko katika msimu wa sadaka; ni lazima tuulinganie Uislamu kama badali ya mfumo uliofeli wa Ubepari na hivyo suluhisho pekee la masaibu ya ulimwengu litakalotoa matokeo makubwa.

Hatimaye, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie matendo yetu mema na atuongoze kwenye Idd ya mwakani tukiwa chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, chini ya bendera ya 'Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah'.

Twawaombeeni kila mwaka na muwe karibu na Mwenyezi Mungu (swt).

Twawaombeeni kila mwaka muwe katika kheri.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu