Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  28 Shawwal 1444 Na: 1444/11 H
M.  Alhamisi, 18 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utozaji Ushuru Sura ya Kikatili ya Ubepari

(Imetafsiriwa)

Wakenya wanapambana na nyakati ngumu zaidi juu ya mapendekezo ya Sheria ya Fedha ya 2023. Mswada wa fedha uliowasilishwa bungeni unaregesha asilimia 16 ya ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa za petroli pamoja na kuanzisha ushuru wa nyumba wa asilimia 3. Bei za takriban bidhaa na huduma zote zimepanda katika miezi ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na gharama ya umeme, mafuta na unga wa mahindi.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Kenya tungependa kufafanua yafuatayo:

Mswada huo umefichua unafiki wa wanasiasa ambao hawana ikhlasi huku maafisa wakuu wa serikali wa sasa wakikataa Mswada wa Marekebisho wa Bidhaa za Petroli (Ushuru na Kodi) wa 2021 katika utawala uliopita. Huku Serikali ya Jubilee ikiwa nje ya afisi, waliokuwa wapinzani wa wakati huo wa ushuru wa juu ndio sasa wanaouunga mkono zaidi.

Kwa mtazamo wa harakaharaka wa utozaji ushuru mkubwa kwa Wakenya wa kawaida wakati wa kabla na baada ya uhuru haujawahi kutatua matatizo yoyote ya kiuchumi na kifedha bali kuitumbukiza nchi katika mgogoro wa kudumu wa kiuchumi na kifedha. Inavyoonekana, utozaji ushuru kama pato kuu katika mfumo wa kibepari haujakuwa na kamwe hautakuwa suluhisho kwa uchumi ambao tayari unaugua.

Imedhihirika wazi kuwa serikali za kibepari hazijitwiki jukumu katika kusimamia mambo na maslahi ya mwananchi wa kawaida. Badala yake, kinacho maanishwa na kuboresha maisha ya watu wake ni kuongeza kodi ambayo hatimaye huathiri kupanda kwa bei za bidhaa na huduma na kusababisha umaskini uliokithiri. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, tawala za kibepari zinategemea sana ukopaji fedha. Kuchukua mikopo mingi kwa kodi za wananchi kama dhamana ya kufadhili miradi ‘hewa’ kisha baada ya hapo fedha hizo zinaporwa na viongozi walafi wa juu serikalini.

Tunasisitiza tena kwamba Dola ya Khilafah inayotabikisha mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ulio huru kutokana na  utozaji kodi zote za kikatili kama vile VAT na Kodi ya Mapato. Mtume Muhammad (saw), amesema;

«لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ صَاحِبُ مَكْسٍ» “Mtoza ushuru hataingia peponi.” (Ahmad). Uislamu una mfumo wake wa kipekee wa ukusanyaji mapato, ikiwa ni pamoja na mapato kutoka kwa mali ya umma (kama vile gesi) na uzalishaji wa kilimo (kama vile kharaj), ambayo huingiza mapato bila kunyonga shughuli za kiuchumi. Na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unaorodhesha rasilimali kama vile nishati, ardhi ya malisho na maji kama mali ya umma. Dola wala watu binafsi hawawezi kujinyakulia manufaa yake peke yao, badala yake manufaa kutoka nazo ni kwa ajili ya watu wote. Mtume Muhammad (saw), amesema:

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّار» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto” (Ahmad, ibn Majah)

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu