Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  29 Ramadan 1445 Na: 1445/12 H
M.  Jumatatu, 08 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Tunawapongeza kwa Munasaba wa Siku Kuu ya Idd ul Fitr

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kutoa salamu za dhati za Idd ul-Fitr kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa ujumla. Tunatoa pongezi zetu kwa wabebaji wa Da’wah wa Ummah wanyoofu wanaofanya kazi bila kuchoka kuelekea kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Pia tungependa kutoa salamu zetu njema kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah na kwa Waislamu wote katika Idd hii yenye baraka.

Umbile la mauaji la Kiyahudi linalopata uungwaji mkono wa Marekani na Ulaya linatekeleza mauaji huko Gaza. Kwa hiyo, Idd imerejea huku damu za wanawake wetu, watoto na wazee hazijaacha kutiririka kama mito katika mitaa ya Gaza. Wanawake wetu wanapaza sauti zao ambazo zimejaza anga Ewe Mu’tasim!! Bila majibu isipokuwa kejeli kutoka kwa wakoloni pamoja na vibaraka wao katika Ardhi za Kiislamu!

Suluhisho la Kiislamu juu ya kadhia ya Palestina kama suala jengine lolote linaloshuhudiwa duniani kamwe halitopatikana kwa kufanya ‘mikutano ya dharura’ ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au kauli tupu za Riyadh, Tehran, Islamabad au Istanbul. Tunahitaji Khilafah ambayo itakusukumeni na kupeleka  majeshi ya Kiislamu ili kuling’oa umbile la Kiyahudi la mauaji yanayokomboa sio tu Palestina inayokaliwa kimabavu bali ardhi zote za Waislamu. Khilafah pia itasuluhisha matatizo yote ya kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani kwa suluhisho la kudumu na la kina Bi’idhnillah.

Kullu Aami Wa antum aqrab ilaa lllah

Kullu aamiy wa antum bikheir

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir

Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu