Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  4 Ramadan 1445 Na: 1445/11 H
M.  Alhamisi, 14 Machi 2024

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Kenya

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara 2: 156]

(Imetafsiriwa)

Kwa imani thabiti na kujisalimisha kikamilifu kwa kudra ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir / Kenya inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla na watu wa Kenya hasa;

Ustadh Said Salim Ali

(Mwenyezi Mungu amrehemu) aliyefariki mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 14 Machi 2024, baada ya kushambuliwa na majambazi.

Akiwa kama Ustadh na Imam, Ustadh Said alijiunga na Hizb ut Tahrir - chama cha Kiislamu cha kimfumo cha kilimwengu ambacho kinabeba ulinganizi adhimu wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume (saw). Ingawa, na sisi hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), tunashuhudia kwamba alikuwa akitekeleza kujitolea kwake kwa Da’awa.

Hakika nyoyo zetu zinahuzunika, macho yetu yanabubujika machozi kwa msiba huu mkubwa wa baba na ndugu yetu, Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu na umsamehe. Ewe Mwenyezi Mungu, yakirimu mapokezi yake, na upanue muingio wake.

Mwisho, tunapenda kutuma rambirambi zetu za dhati kwa familia yake tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu (swt) awalipe malipo makubwa, na awape subira, ujasiri na faraja. Tunamuomba Mwenyezi Mungu abadilishe makaazi yake kwa makaazi bora, na familia yake kwa familia bora, na atukusanye sisi na yeye chini ya bendera ya Mtume (saw) Siku ya Kiyama.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu