Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445/15 H
M.  Ijumaa, 31 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir / Kenya Yafanya Visimamo vya Kushutumu Kitendo cha Kikatili cha Umbile la Mauaji la Kiyahudi cha Kulipua Mabomu Rafah

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kitendo cha kinyama na cha kusikitisha cha umbile la Kiyahudi cha kulipua mabomu katika Kambi za Wakimbizi huko Rafah, usiku wa tarehe 26 Mei 2024, Hizb ut Tahrir / Kenya ilifanya visimamo vya kulaani baada ya swala za Ijumaa katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi, Mombasa, Malindi, Kilifi na Kwale. Katika visimamo hivyo, Hizb ilitoa wito kwa majeshi ya Waislamu kusonga mara moja ili kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa katika Ardhi Iliyobarikiwa – Qibla cha Kwanza, Ardhi ya Isra’ wal Miraj na kuikomboa kutokana na makucha ya umbile halifu la Kiyahudi.

Hizb ut Tahrir / Kenya ilishutumu mauaji hayo yaliyofanywa hata baada ya amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa 'Israel' kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi huko Rafah. Pia ilikariri kwamba majeshi ya Waislamu na watu wenye nguvu wana jukumu kubwa la kuwanusuru wana wa Ardhi Iliyobarikiwa.

Ummah ulikumbushwa juu ya kazi yao adhimu ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itayakusanya majeshi ya Kiislamu dhidi ya umbile la Kiyahudi linaloungwa mkono na Magharibi.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu