Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  8 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445/16
M.  Ijumaa, 14 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

[لَبَّيْكَ ٱللَّٰهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ ٱلْحَمْدَ وَٱلنِّعْمَةَ لَكَ وَٱلْمُلْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ]
Enyi Majeshi ya Waislamu! Je, Talbiya inayotamkwa wakati wa Hajj itakufanyeni Muitikie Wito wa Mwenyezi Mungu na Muanze Kutembea Kuikomboa Gaza?

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kutoa salamu za dhati za Idd ul-Adha iliyobarikiwa kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa jumla. Tunaposherehekea Idd hii yenye baraka, tujikumbushe matendo ya Mtume (saw) baada ya hijja yake ya kuaga; uteuzi wake wa Usama ibn Zayd kama kamanda wa kikosi cha msafara ambacho kilitumwa Syria. Tunapohitimisha hijja, Jeshi la Waislamu linapaswa kufuata Sunnah ya Mtume (saw) kuandamana kupigana na jeshi la jeshi la mauaji Mayahudi katika Gaza inayokaliwa kwa mabavu.

Hakika Talbiya (Labaika Allahuma Labaik, labaika laa shareeka laka labaika...) inapaswa kuyaamsha majeshi ya Waislamu kuvuka mipaka bandia ya Sykes Picot ili kuwanusuru wana wa Gaza ambao wamelitikisa jeshi la Mayahudi. Enyi viongozi wa Waislamu: Baadhi yenu huenda mlitamka maneno haya matukufu ya ibada ambayo yana maana kwamba kadhia ya Palestina kama kadhia nyengine yoyote ile itatatuliwa kwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu, yaani Uislamu. Kwa nini basi mnafanya ‘mikutano ya dharura’ ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au munatoa kauli tupu ambazo si lolote zaidi ya kuimarisha mkono wa uhalifu wa kuikalia Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina, ardhi ya Isra’ wal Mi’raj??

Idd hii inapaswa kuwakumbusha Waislamu mtihani mkubwa kwa Baba wa Imani Ibrahim (as) na utayari wake mkubwa wa kujitolea. Hakika tuko katika msimu wa kujitolea mhanga; ni lazima tulinganie Uislamu kama badali ya mfumo uliofeli wa Ubepari na hivyo suluhisho pekee la mateso ya ulimwengu litakuwa na matokeo makubwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie amali zetu njema na atuongoze kwenye Idd ya mwakani tukiwa chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaziunganisha nchi zote za Kiislamu duniani chini ya bendera ya 'Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah'.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu