Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445/18
M.  Jumamosi, 29 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi nchini Kenya

(Imetafsiriwa)

(إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Hakika Sisi Ni Wa MwenyeziMungu Na Hakiki Sisi Kwake Yeye ni Wenye Kurejea”

Kwa imani thabiti na kujisalimisha kikamilifu kwa Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir/Kenya inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla, na haswa watu wa Kenya;

Seif Omari Mwaruwa

(Mwenyezi Mungu Amrehemu) aliyefariki dunia siku ya Ijumaa Juni 28, 2024. 

Licha ya kuwa mzee, Ndugu Seif alijiunga na Hizb ut Tahrir – harakati ya Kiislamu ya kilimwengu ya Kimfumo inayobeba wito adhimu wa kuhuisha maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume (saw). Pamoja na hali yake ya maradhi mzee alikuwa bado anatimiza ahadi yake na kutangamana na watu wa umri wake juu ya suala muhimu la Khilafah na wala hatumsifii yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Hakika nyoyo zetu zinahuzunika, macho yetu yanatokwa na machozi kwa msiba huu mkubwa wa baba na ndugu yetu. Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu na umsamehe. Ewe Mwenyezi Mungu, kirimu mashukio yake na ukunjue makaazi yake.

Mwisho tungependa kutuma rambirambi zetu za dhati kwa familia yake huku tukimuomba Mwenyezi Mungu (swt) awalipe ujira awape subra, ujasiri na faraja. Twamuomba Mwenyezi Mungu aidha, ambadilishie nyumba yake kwa makaazi bora, na familia yake kwa familia bora zaidi na akatukutanishe pamoja naye chini ya bendera ya Mtume (saw) Siku ya Kiyamah.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu