Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  22 Muharram 1446 Na: H 1446/01
M.  Jumapili, 28 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Mageuzi ya Baraza la Mawaziri: Mkakati wa zamani Nyuso mpya

(Imetafsiriwa)

Rais William Ruto amewateua wanachama wanne wa chama kikuu cha upinzani kama sehemu ya baraza jipya la mawaziri huku maandamano yakiendelea kulitikisa taifa hili la kanda ya Afrika Mashariki. Rais alikuwa ameahidi kuteua baraza jipya la mawaziri ili kukabiliana na maandamano ya G-z yaliyoshuhudiwa mwezi mmoja uliopita. Hatua hiyo ‘inalenga’ kuwezesha upatikanaji wa ajira, usimamizi thabiti wa madeni, kuimarishwa kwa uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya pesa za umma.

Tungependa kueleza yafuatayo:-

Masuala yaliyoibuliwa na kizazi cha G-z yamekuwa ni yale yale ambayo yamekuwa yakiibuliwa na jamii kwa ujumla katika historia ya Kenya. Tukiangazia kwa makini matatizo haya, tunaona kwamba bado hayajapata suluhu ya kikweli bali wanasiasa wamekuwa wakiyapatiliza na kuyazungusha kwa mzunguko wao muovu wa kisiasa hatimaye kuyatokomeza kwenye giza totoro. Uhalisia wa hali hii ya kutamausha kamwe wanasiasa hawatoibadili kwa ajili ya maslahi ya umma, bali tabaka la kisiasa na hata wale wanaoitwa G-z wamefunga mwito wa mabadiliko kwa dhana kwamba mabadiliko yako kwenye marekebisho ya kikatiba na kubadilisha wanasiasa.

Tunasema mfumo wa kibepari, zana ya kikoloni inayotumika kunyanyasa ‘nchi za ulimwengu wa tatu’ ndio suala linalohitaji kujadiliwa hapa. Ingawa tunathamini maandamano ya sauti ya G-z dhidi ya IMF na Benki ya Dunia kama zana za kifedha za kikoloni, hata hivyo, kuna haja ya kuendeleza hisia hizi za kisiasa ili kuelewa uhalisia ulioko wa mfumo huu wa Kibepari unaotawalishwa kote duniani na Kenya ni miongoni mwa muhanga wa mfumo huu.

Mfumo wa Kibepari umetengeza urongo juu ya mabadiliko kwa kuyafunga na chaguzi za mara kwa mara, marekebisho ya katiba na haki ya kuandamana licha kwa yote hayo hakujashuhudiwa mabadiliko yoyote yale ya kimsingi. Kwa fika hii ya kina na ufahamu huu ulio wazi tunasema bayana kwamba watu wapya na wale wa zamani kwenye baraza la mawaziri ni mkakati ule ule wa zamani matokeo yake ikiwa ni yale yale wala hakuna mapya.

Tunasema mabadiliko makubwa ni wito kwa Uislamu kama mfumo pekee unaompendeza Mola wa wanadamu… Mfumo ambao unalazimika kurudisha utu wa mwanadamu kama kipaumbele cha kisiasa. Juu ya utekelezaji wake chini ya mfumo wa utawala Khilafah unahakikishia watu maisha mazuri. Uislamu ndio chaguo pekee la kumkomboa mwanadamu kutokana na kufeli huku kwa mara kwa mara kwa mfumo wa kirasilimali, kwani unahakikisha ustawi wa kiuchumi na Kisiasa. Kihistoria, kwa utekelezaji wake, Uislamu uliwanyanyua wanadamu kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa kiuchumi na unafiki wa kisiasa.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya wa Habari Hizb ut Tahrir

Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu