Afisi ya Habari
Kenya
H. 4 Safar 1441 | Na: 1441 H / 02 |
M. Jumatano, 02 Oktoba 2019 |
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Mkasa wa Feri: Kufeli kwa Urasilimali katika Kuhudumukia Watu Wake
Imepita saa 72 (kuanzia Jumapili, 29/09/2019 Saa 18:15 PM) miili ya Mariam Kigenda mwenye umri wa miaka 35 na binti yake hadi sasa haijatolewa kutoka majini. Bi Mariam alikufa maji baada ya gari lake kurudi nyuma na kuingia kwenye bahari ya Hindi siku ya Jumapili tarehe 29 Septemba 2019. Twapenda kutoa rambirambi zetu kwa marafiki na familia ya bi Mariam Kigenda.
Licha ya kuwepo kwa wapiga mbizi wa Jeshi la Wanamaji na wale wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya, hadi sasa miili ya wenda zao haijatolewa! Hali hii ya kusikitisha imelazimu familia ya Mariam kukodisha wapiga mbizi wa kibinafsi kusaka miili hiyo. La kutamausha zaidi, kwa miaka yote ya kuhudumu kwake, Kenya Feri hadi sasa haina hata mpiga mbizi mmoja. Suala msingi linaloibuka ni; je kweli maafisaa wa kijeshi wako tayari kukabaliana na majanga ama nikuwa tu tayari kufanya gwaride katika siku kuu za kitaifa pekee?
Mkasa huu kwa mara nyingine unaonesha ukosefu wa usimamizi bora pamoja na kuweko kwa mikakati miovu sio tu katika shirika la huduma za Feri bali katika wazira yote ya uchukuzi na usafiri. Ni utepetevu wa kiwango cha juu sana kuona Serikali na Wizara yake ya Uchukuzi wakisuburia majanga kutokea kisha ikijivuta katika kuchangamkia masuala ya usalama wa umma. Tunatangaza wazi kwamba yote haya ni ishara ya kufeli kwa mfumo wa kibepari katika kuhudumikia vyema raia wake. Mfumo huu kikawaida hupuuza na kudharau masuala ya huduma zote kwa umma ikiwemo suala la usalama wa umma. Kwa uhalisia huu, ndio tunalingania watu wote kuungana nasi katika kazi tukufu ya kuisimamisha tena Khilafah itakayotilia maanani suala la usalama wa umma ikiwemo usafiri wa abiria kwa kukagua vyombo vyote vya usafiri na kuweka jopo maalumu la uokozi wa dharura kabla ya kuanza safari ili kuepuka ajali za kiholela.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |