Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  1 Sha'aban 1430 Na:
M.  Jumatano, 22 Julai 2009

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ufahamu wa Kimakosa Kuhusu Hizb ut Tahrir kuwa ni 'Chama cha Kisiasa'

Mara tu baada ya kumalizika kwa Kongamano la Kimataifa la Khilafah lililo andaliwa na Hizb ut tahrir Afrika Mashariki mnamo 27 Rajab 1430 H (19 Julai 2009) katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni, Dar es Salaam, kongamano la kipekee lililo faulu lililo hudhuriwa na maelfu ya watu wa jinsia zote mbili, hisia mchanganyiko ziliibuka hususan kuhusiana na ufahamu wa kimakosa kuhusu maana ya Hizb ut Tahrir kuwa ni chama cha kisiasa.

Kutokana na ufahamu huu wa kimakosa tungependa kubainisha na kufafanua yafuatayo:

1. Neno 'Siyasah' asili ni neno la Kiarabu na halikutokana na lugha za kibantu (lugha zenye asili ya Kiafrika). Kwa mujibu wa Uislamu, neno hili lamaanisha 'kusimamia na kuchunga mambo yao ikiwemo kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu pamoja na kuowaongoza juu ya lile wanalo paswa kufanya na kutofanya kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu. Vilevile 'Siyasah' hii ni wajibu wa Kiislamu unaomfunga kila Muislamu kwani hutiririka kimaumbile kutokana na itikadi ya Kiislamu. Bali kihakika kuikataa fahamu hii ya siasa katika Uislamu ni sawa na kuikataa hukmu nyengine yoyote ya Kiislamu kama kuswali na kufunga. 

Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa fahamu ya siasa katika Uislamu kimsingi ni tofauti kutokana na siasa zinazo tekelezwa na vyama vya kisekula/kidemokrasia kwani itikadi ambayo kwayo Uislamu umejengwa juu yake ni tofauti kabisa kutokana na itikadi ya kisekula ya kidemokrasia. Hivyo basi ufahamu wao wa siasa ni tofauti kabisa

1. Siyasah ambayo ni kuangalia mambo ya watu hutabikishwa katika njia mbili kwa mujibu wa Uislamu. Kwanza, hufanywa kivitendo na Dola kupitia kulazimisha sera maalumu juu ya watu, na pili hufanywa kifikra na watendaji wengine wasiokuwa Dola ambao wamefungika na kuamrisha mema na kukataza maovu na kuihisabu Dola, upande ambao waweza kutekelezwa na mtu yeyote, kundi au chama. Hizb ut Tahrir huzifunga siasa zake katika upande huo wapili pekee. 

Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu na fikra zake zote huvuliwa kutokana na machimbuko ya Kiislamu kwa mujibu wa dalili zake kutoka katika Qur'an na Sunnah. Dalili hizo za Kiislamu zinaharamisha kushiriki katika siasa zilizo jengwa juu ya nidhamu ya kidemokrasia ambayo imejengwa juu ya usekula, fikra ambayo inagongana na Uislamu moja kwa moja.

Ni muhimu mno ifahamike waziwazi kuwa Hizb ut Tahrir kamwe haitumii ghasia wala amali zozote za kisilaha katika njia yake ya mabadiliko. Zaidi ya hayo hailengi kuasisi Dola ya Kiislamu eneo la Afrika Mashariki wala hailengi kujihusisha na mvutano wa kisiasa dhidi ya serikali. Imejifunga kikamilifu na kulingania Uislamu kupitia mvutano wa kifikra katika mujtamaa. Kutokana na msingi huu ni dhahiri kuwa hakuna sababu ya kuwepo vita kati yake na serikali.

Baada ya kusema hayo na baada ya ufafanuzi wa juu, sasa tunapo sema kuwa Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa hatumaanishi 'chama cha kisiasa' kuwa ni 'chama kisiasa cha kidemokrasia' kinacho wakilishwa na wanasiasa wa kidemokrasia na kusimamiwa na sheria inayo husiana na usajili wa vyama vya kisiasa. Kihakika siasa kwa mtazamo wetu ni kitu tofauti kabisa. Hivyo basi Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa kwa mujibu wa Uislamu kinacho lenga kuangalia mambo ya watu kifikra nje ya upeo wa Bunge la kidemokrasia.

Fauka ya hayo, kitakuwa ni kioja chenye dosari hatari endapo upande mmoja tutaikashifu demokrasia na ilhali, upande mwengine, tunataka kuwa washika dau wanaoshiriki katika demokrasia! Ufisadi wazi na usio shaka wa demokrasia umefichuliwa pakubwa katika fasihi nyingi za Hizb ut Tahrir ikiwemo kijitabu chetu: "Demokrasia ni Nidhamu ya Kikafiri" ambayo iliuzwa kwa mamia siku ya kongamano hilo lililo tangulia kutajwa.

Kwa ufupi, siasa katika ufahamu wa Hizb ut Tahrir ni tofauti na ufahamu wa kidemokrasia inayompa mwanadamu 'haki' ya kutunga sheria badala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kutokana na msingi huu, na huu ndio mtazamo wa Kiislamu, kamwe haturuhusiwi ima kushiriki katika chaguzi za kidemokrasia au kujiunga na chama chochote cha kidemokrasia.

Kuhusu taarifa, za kipuuzi, duni na za kiuadui zinazo tolewa na baadhi ya viongozi wa Kikristo kama zilivyo nukuliwa na baadhi ya magazeti ya kila siku: Mmoja wao ni Mchungaji Christopher Mtikila aliye nukuliwa na (gazeti la) 'Uhuru' la Jumanne 21 Julai, 2009 katika ukurasa wa 3 akisema kuwa: "Wote wale waliojitokeza kukitambulisha chama hiki cha kisiasa wanastahili kukamatwa na kushtakiwa." Mwengine ni Askofu Mkuu Kilaini wa Dar es Salaam aliye nukuliwa na 'Habari leo' la tarehe hiyo hiyo katika ukurasa wa 2 akiichochea serikali kuchukua hatua kali hasa juu ya kadhia hii.

Tumetambua kuwa 'viongozi' hawa wa kanisa, kwa masikitiko makubwa, wanazungumza upuuzi kutokana na ujinga wa kutojua kwa lengo la kuichochea serikali kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki pasi na msingi wowote wa kisheria.

Pasi na shaka, taarifa hizi ni dhihirisho wazi la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na zinatukumbusha maneno ya kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

قَدْ بَدَتْ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمْ الآياتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ

"Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini." [Al-Imran:118]

'Viongozi' hawa wa kanisa wanaipatiliza kadhia hii iliyoko sasa ili kunali maslahi yao duni kinyume na haki za Waislamu za kulingania dini yao ya Uislamu, ilhali ni dhahiri Waislamu ndio idadi kubwa ya raia wa Tanzania! 

Kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, na kama sehemu ya kutekeleza mvutano wa kifikra, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki inasubutu waziwazi kuwataka viongozi hawa wa Kikristo kushiriki nasi katika mdahalo wa wazi wa kiakili hadharani ndani ya wiki mbili zijazo, katika siku na wakati watakao chagua wao maadamu utakuwa katika mahali wazi na pazuri kwa ajili ya uhudhuriaji wa umma. Mdahalo huu utafichua, hadharani, fikra ipi ni ya kweli kati ya rai zao na itikadi yetu ya Kiislamu.

Ni matarajio yetu kuwa viongozi hawa hawatasita kuitikia mwito huu wa mdahalo kwani utategemea dalili za kiakili pekee na utanufaisha mujtamaa mzima.

Masoud Msellem

Mwakilishi Rasmi kwa Vyombo vya Habari wa Kongamano la Kimataifa la Khilafah

Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu