Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  8 Dhu al-Hijjah 1436 Na: 1436/18 H
M.  Jumanne, 22 Septemba 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Linalo Hitajika ni Kuachana na Mfumo Dhalimu wa Kirasilimali

Serikali ya Kenya imezifunga rasmi shule za msingi na upili kufuatia mgomo wa walimu ambao sasa umeingia wiki yake ya nne. Mgomo huu ni kutafuta ongezeko la mshahara la kati ya asilimia 50 na 60 kama ilivyo elekezwa na Mahakama Kuu. Serikali upande wake imejitokeza waziwazi ikisema kuwa haina pesa za kufikia matakwa ya walimu hao.

Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki ingependa kuangazia nukta zifuatazo:

Kwanza tangu 1997 mpaka leo, hiyo ni miaka 18 kamili bado kadhia hii ya sekta ya elimu ingali haija tatuliwa! Ni aibu iliyoje kwa serikali inayodai kuwatawala watu huku ikishindwa kutatua kadhia muhimu zinazo gusa maslahi ya walimu wao. Inajulikana hadharani kuwa sio tu walimu pekee walio na matatizo bali pia madaktari na wamiliki wa magari ya abiria wanafuata nyayo za walimu. Hili laidhihirisha Kenya kama nchi ya migomo ambapo wafanyikazi wanabadilishana zamu!

Pili ni dhahiri shahiri kuwa viongozi wa kidemokrasia wana ubinafsi na hawatambui maslahi ya umma. Dalili ya hilo ni kuwa Kenya kamwe haijawahi kuona mgomo wa Wabunge, ambao wakati wowote hupendekeza na kuidhinisha ongezeko la marupurupu kwa matamanio yao licha ya rai jumla kukemea! Inathibitika kuwa elimu nzuri, afya nzuri na mazingira mazuri katika nchi za kidemokrasia sio wote wenye kuyamudu kama inavyodaiwa bali; hupatikana kwa matajiri. Kinyume na hilo, masikini ambao ndio wengi katika nchi hizi za kiimla hawapati huduma nzuri zozote na wao ndio wanao teseka zaidi na migomo ya aina hii.  Huo ni urongo wa wazi unaothibitisha Demokrasia kama nidhamu ya kisiasa isiyojali kuhusu maslahi ya umma badala yake inajali tu maslahi ya kundi fulani la watu.

Tatu katika mataifa ya kirasilimali, waajiri wao na tume zao huwahadaa waajiriwa kwa haki za kushiriki katika migomo ili wao watambue misingi miovu ya mfumo wa kirasilimali wenyewe. Uhalisia ni kuwa migomo haitatui matatizo yoyote ya waajiriwa; ni kama mfano wa kumnyima mgonjwa dawa ili kutibu ugonjwa wake lakini; badala yake kumpa dawa ya kupunguza tu maumivu! Linalo hitajika kwa waajiriwa hawa na watu wote kwa jumla ni wao kuukataa mfumo wa kirasilimali unao wahangaisha. Mfumo ambao umesimamishwa pekee kulinda maslahi ya kiuchumi ya watu fulani wanao wakamua raia hadi mwisho kwa kuwalenga kupitia aina tofauti tofauti za ushuru unaoyafanya maisha yao kuwa ya dhiki hata kwa wale wanaofanya kazi. Kwa hali kama hizi, vilio sio tu kuhusu mishahara bali juu ya gharama ya juu ya maisha ambayo serikali za kirasilimali zimeshindwa kuwasaidia raia wao ikiwemo walimu.   

Nne Uislamu unaeleza kinaganaga kuwa elimu ni miongoni mwa mahitaji msingi ya umma ambayo Dola inapaswa kutoa elimu kwa watoto wote bila la kujali asili zao za kijamii na kiuchumi. Uislamu pia, umeelekeza kuwa mishahara ya walimu ilipwe kutoka katika Hazina ya Dola (Bait ul-Mal). Mbali na hayo, Uislamu pia umepiga marufuku utozaji ushuru juu ya mshahara wa mwajiriwa ili kuwawezesha kukimu mahitaji yao msingi. Kwa msingi huo, tunaeleza kinaganaga kuwa ndani ya Khilafah kwa njia ya Utume, kamwe hutaona migomo ya walimu na wafanyikazi wote kwa sababu Uislamu unahifadhi haki zao.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu