Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  4 Ramadan 1436 Na: 1436/13 H
M.  Jumapili, 21 Juni 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki Inatoa Mwito Kabla ya Mwisho… kwa Ummah wa Mafanikio Makubwa Kabisa

Wanachama wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki, Ijumaa iliyopita, kwa kuingia Ramadhan (2 Ramadhan 1436 H / 19 Juni 2015) walikuwa na wasaa mzuri wa kukutana na wanachama wengine wa Hizb kote ulimwenguni kufikisha ujumbe maalumu kutoka kwa Amiri wa Hizb unaojulikana kama "Mwito Kabla ya Mwisho… kutoka kwa Hizb ut Tahrir" ambao uliwalenga Waislamu haswa na hususan wale wanao shikilia udhibiti na mamlaka miongoni mwao ambayo yanaweza kutumiwa kutoa nusra katika nchi zenye nguvu za Kiislamu. Mwito huo pia uliwalenga Waislamu wote walio salia popote walipo.   

Katika sehemu ya Afrika Mashariki, Hizb ilifikisha mwito huu mbele ya wasikilizaji wengi katika miji mikuu mitatu ya Kiislamu iliyo eneo la Afrika Mashariki. Jijini Mombasa, Kenya mwito huu ulifikishwa ndani ya Msikiti wa Taqwa, na Ustadh Shabani Mwalimu, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki. Jijini Dar es Salaam, Tanzania, mwito huu ulifikishwa ndani ya Msikiti wa Simba Mbali na Masoud Msellem, Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki. Ama sehemu ya Zanzibar, mwito huu ulifikishwa ndani ya Msikiti wa Mianzini kupitia Ali Amour, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki. Katika miji yote hiyo, mwito huu ulisikizwa kwa makini na Waislamu punde tu baada ya swala ya Ijumaa.  

Lengo kuu la mwito huo wa kimataifa, lilikuwa ni kuwakumbusha Waislamu walio katika mamlaka na kumiliki nguvu na ushawishi katika nchi zenye nguvu za Kiislamu kuhusu kazi na jukumu zito, juu ya shingo zao kupitia kujitolea mhanga kuulinda Uislamu kupitia kutoa NUSRA kwa lengo la kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah katika mojawapo na nchi yoyote ya Kiislamu yenye nguvu. Katika jaribio la kuwasaidia Waislamu kunyanyuka kutoka katika hali yao ya sasa ya mateso, matatizo na majanga mengi yasiyosemeka wanayopitia tangu kuvunjwa kwa Dola ya mwisho ya Kiislamu ya Khiafah Uthmaniya; na kubeba jukumu tukufu la kuhukumu na kutawala kwa Uislamu. Katika upande wa Waislamu wote, mwito huu uliwakumbusha ufaradhi wa kuungana mikono na Hizb ut Tahrir katika kufanya kazi kwa bidii ya kurejesha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Kwani hii ndiyo mama wa faradhi zote nyingine za Kiislamu. Mwito huu uliwaonya na kuwasihi Waislamu wasiwe watazamaji tu; badala yake wanapaswa kuunga bogi la safari hii bila ya kuchelewa, kwani wao ni sehemu ya Ummah huu.   

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mwanzo wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, kuufanya mwito huu usikike, ukubaliwe na kuzilainisha nyoyo za wale waliokatika mamlaka katika nchi za Kiislamu na kuwafanya watoe Nusra katika mojawapo ya ardhi za Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu na kisha kuenea hadi ulimwengu mzima.

Mwisho, wa maneno yetu, sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu