Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Rabi' I 1443 Na: 1443 H / 013
M.  Jumatatu, 25 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Syria: Maiti na Viungo vya Miili!

Nani Atawasaidia na Kuzuia Ukandamizaji wa Mtawala Dhalimu Bashar na Maadui juu yao?
(Imetafsiriwa)

Asubuhi ya Jumatano tarehe 20/10/2021, vikosi vya al-Assad vililenga vitongoji kadhaa vya Ariha, mji wenye wakaazi wengi raia, na kurusha makombora zaidi ya tisa mfululizo ambayo yalipiga shule kadhaa, na kuacha mashahidi kadhaa, akiwemo mwalimu wa lugha ya Kiarabu ambaye alikuwa akielekea shuleni na mtoto aliyekuwa akielekea shuleni, akiwa amebeba mkoba wake mgongoni, pamoja na watoto na raia wengine katika vitongoji kadhaa vya mji huo. Wengine takriban 30 walijeruhiwa. (Sham Network).

Haya ni mauaji mapya yaliyofanywa na utawala katili wa Assad na vikosi vya makruseda vya Urusi dhidi ya watu wetu katika mji wa Ariha, kusini mwa Idlib. Vikosi hivi havizingatii jukumu lolote kuhusu watoto na wanawake wasio na hatia na vinalenga kwa makusudi miji mikuu, haswa mji wa Ariha, ambao unashuhudia msongamano wa watu na msongamano mkubwa wa raia zaidi ya elfu 50 (jamii kubwa zaidi ya wakaazi katika kiunga cha kusini mwa Idlib kwa sasa). Kwa hivyo inaelekeza mashambulizi yake kwenye shabaha hizi, kutokana na kiu ya kulipiza kisasi, na kuwalazimisha raia kukimbia.

Ni mauaji yanayofichua uongo wa madai ya upinzani kwamba umefanya mazungumzo na serikali - chini ya usimamizi wa kimataifa - kutafuta suluhu. Ni mauaji yanayofichua ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa na utawala wa jinai wa Bashar na Urusi dhidi ya watu wa Ariha na Syria kwa ujumla, hivyo hakuna uwajibikaji au mashtaka ya kisheria kwa uhalifu na mauaji yaliyofanywa dhidi ya raia. Ni mfumo wa kimataifa usiojali miito na dhiki ya watoto wasio na hatia ilhali wao ni miongoni mwa vifusi na mito ya damu; mfumo wa kimataifa ambao uko kimya kuhusu yale yanayofanywa na watu hawa. Hauoni wala hausikii wala haunyoshi kidole kwa yale yanayowatokea vijana na mabinti wa Kiislamu nchini Syria, na hili si jambo geni. Yanayofanywa dhidi ya watoto wa kiume na wa kike wa Kiislamu huko Kashmir na Afrika ya Kati na maeneo mengine ya mauaji na uchinjaji ni ushahidi wa wazi kabisa wa sera yake ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ni mfumo wa kimataifa ambao haujawapa Waislamu na wanadamu chochote ila dhiki na taabu na kushindwa kuyapatia ufumbuzi na suluhisho matatizo na migogoro inayoikabili!

Enyi Watu wetu mjini Ariha:

Je, kile wale wanaodai mazungumzo na suluhu si ni kupoteza muda na kuzidisha idadi ya mashahidi na mauaji ya raia? Je, jani la mtini lingali halijaanguka ili kukudhihirishieni ubaya wa watu hawa na ufisadi wa juhudi zao? Je, mnatarajia suluhu kutoka kwao ilhali wao ni wafungwa wa maamuzi ya kimataifa ambayo hawawezi kuyakengeusha, na kutoka kwenye mduara wa kile kinacholazimishwa na mfumo wa kiulimwengu unaowaongoza? Mnasubiri suluhu kutoka kwa wale ambao pingu zao zimekazwa?!

Enyi Ndugu zetu na Watoto wetu mjini Idlib:

Mumetambua wazi uungaji mkono wa Urusi kwa utawala wa Assad, hata ikihitajika kufanya mauaji ya moto na halaiki ili kulinda maslahi yake ambayo imeyapata kupitia uingiliaji kati wake wa moja kwa moja, kwa kudhibiti maliasili na kwa kuweka kambi za kijeshi ardhini, baharini na angani. Hili lingewezesha kuweka uwepo wa muda mrefu katika Bahari ya Mediterania, ambayo kwa kudumisha utawala wa Assad watapata sababu halali ambayo inahalalisha uwepo wake, kwani sio maslahi yake kupata suluhu ya kisiasa ili isije kupoteza marupurupu iliyopata kutokana na uingiliaji kati wake nchini Syria. Kwa hiyo, mnatazamia nini kutoka kwa wale wanaomwaga damu, wanaomiliki mbinu za kuua watoto wasio na hatia, na kufuata sera ya kuunguza ardhi?

Enyi Watu wetu nchini Syria:

Miaka imepita tangu mapinduzi yenu yaliobarakiwa na mumejaribu suluhu na makubaliano mengi... lakini je, hali yenu imebadilika? Je, mfumo umebadilika?

Mulisimama kubadili hali yenu. Je, malengo ya mapinduzi yenu yamefikiwa? Mulipaza kauli mbiu ya mapinduzi yenu, "Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Je, yalikuwa hivyo? Yamegeuzwa kutoka kwenye njia, basi yarudisheni katika njia hiyo na muyafanyeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na fanyeni hima kuulingania Mfumo wa Mola wenu Mlezi na mtabikishe vipengee vyake ili muwe watangulizi katika kuinusuru Dini Yake, kurudisha utawala Wake, na kung'oa mizizi ya mfumo fisidifu wa kirasilimali wa kisekula uliosababisha uharibifu mkubwa duniani.

Enyi Vijana Wanyofu wa Ummah… Enyi Watu wenye Nguvu na Ulinzi:

Je, hakuna muongofu miongoni mwenu atakayeinuka kuitikia mwito wa watoto dhaifu na wasio na hatia? Je, hakuna mtu miongoni mwenu atakayeweka mkono wake pamoja na wafanyikazi wenye ikhlasi kuinusuru dini hii na kulinyanyua juu zaidi neno lake?!

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfaal: 24].

Ummah wa Uislamu uko hai na haufi, na hautakosa watoto wake wenye ikhlasi na ulinzi. Hivyo basi, Ewe Mwenyezi Mungu tujaalie tulitekeleze hili haraka iwezekanavyo: wale watakaorudisha heshima yake na kuwahami watoto wake.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu