Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  3 Rabi' I 1443 Na: 1443 H / 011
M.  Jumapili, 10 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Janga la Njaa nchini Afghanistan: Sakata Mpya ya Mfumo wa Kiulimwengu
(Imetafsiriwa)

Watoto milioni moja wa Afghanistan wako katika hatari ya kufa kutokana na njaa; wavulana na wasichana milioni kumi wanategemea misaada ya kimataifa kuishi. Huku watu wa nchi hiyo wakikabiliwa na janga hili, Umoja wa Mataifa unazungumzia juu ya Taliban na kuingia kwake mamlakani na kudai kuwa janga hili ni matokeo ya mwezi mmoja baada ya Taliban kuchukua mamlaka! Katika taarifa moja ya Anthony Guterres, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa tangu Taliban ilipoingia mamlakani mwezi uliopita, kiwango cha umaskini kimepanda na huduma msingi za umma zinakaribia kuporomoka. Hakika hii ni aibu sana! Afisa aliye na uzito wa Guterres anapaswa kuwa mkweli. Je! Nchi hiyo ilikuwa ikitegemea usalama na ustawi hapo mwanzo kabla ya ujio wa Taliban?! Je! Ripoti za UN na wasiwasi wa jamii ya kimataifa ni za kweli?

Afghanistan imekumbwa na majanga chini ya mnyororo wa uvamizi wa Amerika kwa miaka ishirini. Ilikumbwa na mauaji, uharibifu wa miundombinu, ukaushaji rasilimali, ukame na umaskini, bila ya Amerika (ambayo iliikali kwa kisingizio cha maendeleo yake) kutoa msaada wowote kufanikisha kujitosheleza yenyewe au uhuru wa maamuzi mbali na misaada ya kimataifa.

Umoja wa Mataifa unajigamba nia yake ya kutoa mamilioni ili kukidhi njaa ya Waafghan, katika onyesho la ovu la hadhara ya kirasilimali. Mfumo wa Kiulimwengu iliowaua vijana wa Kiislamu, kukiuka matukufu yao na kuwapora utajiri wao, leo inawapa misaada, wakijua fika kuwa kujitoa kwake Afghanistan ilikuwa baada ya kutimiza misheni yake na kuimaliza kikamilifu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika alitangaza kuwa nchi yake iliondoka Afghanistan akijua kuwa haiwezi kufikia hali ya kujitegemea. Kwa hivyo kwa nini wanaangazia utendaji wa Taliban, ambayo inachukuliwa kuwa serikali changa kulingana na kanuni za kisiasa za kimataifa?! Je! Mfumo wa kiulimwengu ungalitenda kwa sauti ile ile ikiwa serikali ingekuwa mikononi mwa wanajeshi wa Afghanistan wanaounga mkono Magharibi? Sote tumeona jinsi Umoja wa Mataifa unavyotoa msaada wake wa kifedha kwa zile zinazoitwa nchi za Ulimwengu wa Tatu kwa badali ya kufungwa na makubaliano yenye sumu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo yanalazimisha mfumo wa Magharibi juu yao kama njia ya maisha. Makubaliano ya CEDAW na Beijing yalilazimishwa juu ya nchi za Kiislamu kwa nguvu kwa badali ya msaada wa kifedha.

Hivi ndivyo Amerika inavyoongoza ulimwengu: na mawazo ya kijambazi, kukausha vyanzo vya nguvu za dola, kufuja utajiri wao, na uvamizi unaowachosha, kisha kuwapa uhuru wa mamlaka wa masharti na wa kivipande ulionyakuliwa kutoka kwao! Halafu mwizi huyo hutuangalia kutupa makombo ya utajiri wetu ulioporwa kama msaada! Ni mwizi mkarimu alioje huyu! Na ukarimu wake hauna mwisho, kwani hataki kutuokoa na njaa, bali anaupiga vita Uislamu tunaoubeba, na anataka kutupa nuru za hadhara ya Kimagharibi ili tuweze kuwa waovu kama yeye! Mwenyezi Mungu (swt), Mola wa walimwengu, ni Mkweli aliposema:

[وَدُّواْ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَاءً]

“Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyo kufuru wao, ili muwe sawa sawa.” [An-Nisa: 89].

Fedha ambazo Umoja wa Mataifa inadai kutoa kwa Afghanistan sio safi. Tumeona kile amacho pesa za kisiasa zimefanya nchini Syria na jinsi gani ziilivyokuwa ala ya kumaliza harakati za jihad na kuwaua wale wenye ikhlasi. Mwenyezi Mungu (swt) daima ametuonya dhidi ya udanganyifu wa makafiri, na akatuelezea vipi:

[إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُواْ بِهَا وَإِن تَصْبِرُواْ وَتَتَّقُواْ لاَ يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا إِنَّ اللّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ]

“Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo.” [Aal-i-Imran: 120]. Na njia yao:

[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللّهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Al-Baqara: 120].

Mtume (saw) ametukataza kuwafuata. (saw) amesema:

«لَا تَسْتَضِيئُوا بِنَارِ الْمُشْرِكِينَ»

“Msitafute nusra kwa moto wa washirikina.”

Enyi watu wa utawala nchini Afghanistan, mmeona jinsi Amerika na Mfumo wa Kiulimwengu ni watu wa hila, waliwasaliti watu wa Palestina, Syria na Iraq kabla ... Leo, wanashuhudia uhalifu wa utawala wa India karibu na nanyi dhidi ya Waislamu huko, na wamebaki kimya. Hawaheshimu makubaliano wa ujamaa na waumini. Je! Watakutunzeni baada ya hili? Chuki imedhihiri vinywani mwao na wanakulaumuni kwa janga walilolisababisha wao wenyewe miongo kadhaa iliyopita kwa sababu tu nyinyi ni harakati ya Kiislamu.

Msipanue kamba za mapenzi kwa adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu, kateni barabara kwao, na jilindeni pamoja na familia zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Kuokoka na makucha ya njaa, umaskini na kuanguka kwa uchumi kumetajwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ambacho kinaelezea kila kitu na kina tiba kwa walimwengu wote. Qur’an sio kitabu cha ruqyah tu, bali kwa nidamu zake ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na masuluhisho, kitaweza, ikiwa mtashikamana nacho vizuri na kukitabikisha, kuiokoa Afghanistan na nchi zote za Kiislamu. Kuokoka ni kwa kupitia tu kuungana na Ummah wenu. 

[وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya: 92]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu