Ijumaa, 13 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  21 Rabi' II 1445 Na: 1445 H / 013
M.  Jumapili, 05 Novemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hakuna Maeneo Salama na Hakuna Mistari Mekundu katika Kamusi ya Umbile Halifu la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Angalau watu watano wameuawa shahidi na kadhaa kujeruhiwa, kutokana na ndege za umbile halifu la Kiyahudi kulenga, mnamo Alhamisi asubuhi, 2/11/2023, Shule ya Abu Assi kwa mabomu ya fosforasi nyeupe yaliyopigwa marufuku kimataifa. Ni mojawapo ya shule za Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA). Ilikuwa ikiwahifadhi maelfu ya watu waliokimbia makaazi yao katika Kambi ya Shati katika Ukanda wa Gaza. Video zilizochukuliwa na wanaharakati zilionyesha matukio ya kutisha ya shambulizi hilo la bomu, ikionyesha hali ya hofu na uoga iliyowakumba kina mama na baba kwa maisha ya watoto wao baada ya shambulizi hilo la bomu kuanza. Kina mama hao walikimbia bila viatu nje ya shule wakiwa wamewabeba watoto wao, na wanaume hao wakaharakisha kufukia mabomu yaliyoanguka kwenye uwanja wa shule na mchanga, ili kuzuia kuzuka kwa moshi mweupe.

Uhalifu wa umbile la Kiyahudi umevuka mipaka. Linafanya mauaji moja baada ya mengine, likizidisha uhalifu na ukatili dhidi ya raia wasio na ulinzi, haswa wanawake na watoto, likivuka mistari yote mekundu, kwa kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zenye athari kubwa kama fosforasi, kukiuka sheria na desturi zote zinazotambuliwa katika vita, na kulenga maeneo ambayo watu walidhani kuwa ni salama, kama vile shule, hospitali, na misikiti, lakini hakuna mahali salama kwa kuzingatia uhalifu na ushenzi huu.

Ulengaji shule hii haukuwa wa kwanza na hautakuwa wa mwisho. Ndege ya uvamizi ililenga Shule ya Osama bin Zaid, katika eneo la Al-Saftawi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa jioni, tarehe 3/11/2023, ambayo ilikuwa na makumi ya watu waliokimbia makaazi yao katika mandhari ya kutisha ya majeruhi na mashahidi, nyingi yao ikiwa ni viungo vya mwili. Mauaji ya kinyama pia yalifanywa kwa kulenga lango la Hospitali ya Al-Shifa na magari ya wagonjwa yaliyokuwa yakisafirisha majeruhi kwa ajili ya matibabu nchini Misri, huku hospitali nyingine zikilengwa kwa wakati huo huo.

Umbile hili halifu linajiona liko salama kutokana na kuadhibiwa na hivyo limepitiliza katika uhalifu wake. Watawala wa Waarabu na Waislamu, hasa nchi jirani, ni walaghai wanaotumikia maslahi ya Mayahudi na Marekani. Hawanyanyui hata mguu. Bali wanachukua hatua waziwazi dhidi ya watu wa Gaza na kuwawekea mzingiro. Jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na Marekani mtetezi mkuu wa umbile hili halifu, ni mlaji njama na mshirika katika uhalifu, na kadhalika taasisi zake zikiongozwa na Umoja wa Mataifa zilizotupa maumivu ya vichwa kwa haki na makubaliano, lakini linapokuja suala la Waislamu, ni kiziwi bubu na kipofu.

Mandhari za uharibifu, viungo vya mwili, na damu, zinazoa wito wa msaada, vilio vya watoto na wanawake, na kilio cha mwanamume kutokana na utisho wa mandhari yanatosha kulainisha jiwe, basi nyoyo za watu wenye nguvu katika majeshi ya Kiislamu zina nini kwamba hazijalainika kwa matukio kama haya?

ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللهِ وَمَا اللهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya. [Al-Baqarah: 74].

Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mnasubiri nini kuchukua hatua?! Kitu kama hiki huyeyusha moyo kutokana na huzuni, ikiwa kuna imani na Uislamu ndani ya moyo huo! Naapa kwa Mwenyezi Mungu mtaulizwa, lakini wakati huo itakuwa ni kuchelewa, basi jiokoeni na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu kabla haijafika siku hiyo.

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu