Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  7 Rabi' I 1445 Na: 1445 H / 004
M.  Ijumaa, 22 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Marufuku ya Niqab kama Kushikamana na Mila na Udhalimu
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Elimu na Elimu ya Kiufundi nchini Misri imetoa uamuzi kuhusu sare ya kawaida ya shule, ambao unajumuisha marufuku ya niqab. Uamuzi huu unasadifiana na kuanza kwa mwaka wa sasa wa masomo mwishoni mwa Septemba. Wizara imesambaza ilani kwa wakurugenzi wa elimu katika majimbo yote. Ilani hiyo inaruhusu hijab katika aina zake zote, ikisema kwamba "kuvaa hijab kwa wanafunzi wa kike ni hiari, mradi haifiniki uso, na haijumuishi mitindo yoyote au vielelezo ambavyo vinawakilisha kifiniko cha kichwa, kinyume na hivyo."

Wizara ya Elimu na Elimu ya Kiufundi nchini Misri inakataza kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiruhusu kwa kupiga marufuku niqab, na inaruhusu kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiharamisha pindi inaposema kwamba hijab zinakubalika mashuleni za aina yoyote bila vizuizi maalum, pamoja na turban, mitandio, na Mitindo mengine maarufu inayovaliwa chini ya jina la hijab. Mitindo hii haitimizi masharti ya hijab ya Kiislamu, ambayo ni kifiniko kwa kichwa na shingo, hadi eneo la kifua. Kama yeye, Mwenyezi, alivyosema:

[وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ]

“Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao” [Surat An-Nur: 31].

Je! Wizara inakusudia kufikia nini kwa kukataza Niqab, ambayo ni nembo ya kidini na vazi la Kiislamu lililovaliwa na wanawake wa Kiislamu kuwaiga Mama wa Waumini, wakitafuta thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Je! Ni ipi motisha nyuma ya kupiga marufuku niqab wakati aina mbali mbali za hijab zikiruhusiwa? Je! Kuna juhudi ya kimakusudi ya kuzihujumu hukmu za Shar'a na kuunda mazingira ya kupuuza vazi la Sharia katika akili za kizazi kipya, kimakusudi kuwavunja moyo kutokana na kufuata elimu?

Je! Wanawake wanaovaa niqab na wale wanaoiunga mkono wanawatotora maafisa katika wizara hiyo kutoa marufuku kama hii? Au je! Hii ni sehemu ya sera ya bunge inayolenga kupambana na Dini ya Mwenyezi Mungu nyoyoni mwa watu wa Misri? Je! Inaambatana na ajenda za utetezi wa wanawake na kwa kuafikiana na ruwaza mapya ya Umoja wa Mataifa, ambayo inapigia debe uasherati na muozo na inatafuta kulazimisha vifungu vya makubaliano ya Cedaw na Beijing nchini Misri kupitia njia yoyote inayowezekana?

Kwa kweli ni mtazamo wa kawaida kwamba sheria na kanuni katika jamii mara nyingi huakisi mifumo iliyopo na mwelekeo wa mamlaka zinazotawala. Maamuzi kama marufuku ya niqab yanaweza kuonekana kama ishara ya msimamo wa watawala wa Misri kuelekea matendo ya Kiislamu na kutokubali kwao kwa utekelezaji fulani wa kidini. Hali hii inaweza kukumbusha muktadha wa kihistoria wa jamii zengine, kama ilivyotajwa katika Quran, ambapo watu wa kitabu (Ahl al-Kitab) walikabiliwa na changamoto zinazohusiana na imani na matendo yao.

[يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَؤُلَاءِ أَهْدَى مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلاً]

“Wanaamini masanamu na Shet'ani! Na wanawasema walio kufuru, kuwa hao wameongoka zaidi katika njia kuliko Walio amini.” [Surat An-Nisaa: 51]

Watu wa Misri ni sehemu ya Ummah ya mwema, na licha ya mipango na njama dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu katika nchi yao, wanaendelea kushikamana nayo. Wanabaki thabiti katika matendo yao ya Dini. Majaribio haya yote machungu ni ushahidi kwamba aqida iko hai nyoyoni mwao, na imani ni thabiti katika nyoyo zao. Kama ilivyo mwili huu mzima, wanangojea kwa hamu siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakirimu watiifu na kuwanyenyekesha wanaoasi.

Kwa hivyo twamuomba Mwenyezi Mungu atumakinishe sisi na wao katika utiifu wake, na kuharakisha ushindi wake kwa ajili yetu, ili tuweze kutawala kwa Sharia yake na kupata utulivu katika utukufu wa uongofo wake. Kwa hakika, yeye ndiye Msimamizi wa hilo na Mwenye uweza zaidi juu yake.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً]

“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Surat Al-Isra: 51]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu