Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 20 Muharram 1439 | Na: 1439/002 |
M. Jumanne, 10 Oktoba 2017 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gharama Kubwa Inayolipwa na Raia Eneo la Deir al-Zour
Na Watawala wa Waislamu katika Meza ya Majadiliano kwa Kuketi na Kukutana na Muuwaji
(Imetafsiriwa)
Ndege za kivita za Urusi, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kimaeneo kutoka Deir al-Zour, zimefanya mashambulizi ya msururu wa mabomu juu ya feri za mtoni zilizokuwa zimebeba maelfu ya raia wanaokimbia eneo la Deir al-Zour kuelekea maeneo mengine, yakisababisha zaidi ya vifo hamsini na maelfu kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.
Uwezekano wa kupona unakaribia kuwa hakuna, hata kwa raia waliolazimika kutoroka kutokana na mashambulizi makali ya angani yaliyowaacha wengi wao maiti katika idadi ambazo hazihesabiki ambazo zinatarajiwa kuongezeka kutokana na ukosefu wa takwimu juu ya watu waliotoweka ambao bado wangali chini ya vifusi. Kwa mujibu wa wanaharakati mjini humo, zaidi ya mashambulizi ya angani 1,000 na kumwagwa kwa idadi kubwa ya mabomu aina ya makombora, na mabomu ya madini ya ‘phosphorus’ pamoja na mizinga ya angani, imenakiliwa katika siku chache zilizopita.
Tangu Machi 2011, Syria imekuwa katika kitovu cha vita dhalimu na mapigano makali vikiwalazimu zaidi ya nusu ya wakaazi kuhama majumbani mwao; huku milioni 5 wakitathminiwa kutoroka nchi hiyo na zaidi ya milioni sita wakiwa wakimbizi wa ndani kwa ndani. Mgogoro wa Syria, ambao umetajwa kuwa janga baya zaidi la kibinadamu la zama hizi, umesababisha mateso yasiyoelezeka kwa wanawake, watoto na wanaume katika maeneo yote, hususan yale yalioasi dhidi ya unyanyasaji katili wa serikali ya Kibaathi ambayo umetumia zana zake za kijeshi na miungano yake ya kisiasa na kijeshi kutibua mapinduzi na kuyapotoa njia yake, ili kutatua kadhia hii kupitia muungano wa kimataifa uliokusanyika kuupiga vita Uislamu katika ardhi ya Ash-Sham.
Kwa miaka, Amerika imefanya kazi kuwagandamiza watu wa Ash-Sham kwa mbinu na njia zote, ikiwemo mikataba ya makubaliano ya kusitisha vita iliyoanza mnamo 30 Disemba 2016 kufuatia makubaliano ya vyama vilivyokusanyika wakati huo jijini Ankara, ambayo hayakulazimishwa juu ya serikali na miungano yake. Kufuatia matukio ya kijeshi uwanjani, mauaji yaliendelea kutekelezwa na udondoshaji mabomu kiholela umebakia kuwa hali kuu ya maeneo ambayo hayakujumuishwa ndani ya azimio hilo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Na huu ndio upinzani wa ng’ambo, ambao ungali unaendelea kukutana kuanzia Geneva 1 mpaka Geneva 8 na kisha Astana 1 hadi Astana 6, ambapo taarifa zote zaashiria kuanza kwa utekelezaji wa mpango wa Amerika na suluhisho lao jipya lililolazimishwa kutokana na ukakamavu wa watu Ash-Sham, nalo ni, kuikalia Syria kijeshi kwa kutafiti uwezekano wa kutuma majeshi ya kuweka amani katika maeneo tete, hususan mkoa wa Idlib. Na ili kutekeleza malengo yake ya kikoloni, imezidisha mashambulizi yake makali ya kijeshi juu ya maeneo hayo, ikilenga raia na miundo msingi na kutekeleza mauaji baada ya mauaji, ambapo kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu, siku chache zilizopita, ilitajwa kuwa ghasia nchini Syria zimekuwa mbaya zaidi tangu kuanguka kwa Aleppo.
Na hawa hapa watawala wa Waislamu ambao wamejazana kwa makundi kwa maadui wa Uislamu. Ufalme wa ukoo wa Saud unafanya mikataba ya kiuchumi na kuweka ruwaza za mbeleni za ushirikiano kamili na muuwaji wa watoto wa Syria wakati wa mapokezi yake mwanana katika ziara yake nyumbani kwa muuwaji huyo! Na huyu hapa mtawala wa Pakistan, akifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Urusi huku ikirusha roketi kutoka katika nyambizi zake na ndege zake kuvunja majumba ndani mukiwa na wakaazi wake!! Na kuna misimamo mengine ya aibu ambayo uovu wake hauelezeki, huku ulimwengu ukiviona vipande vya watoto wetu na kusikia vilio vya mama zetu. Hata kukemea na kushutumu kumepitwa na wakati sasa na hakuko sambamba na kiwango cha usaidizi wao kwa makafiri wa Kimagharibi.
Hakuna jengine lililo wazi zaidi kuliko uvamizi huu na taarifa hizo zinazofichua lengo la kikoloni la Amerika na washirika wake, ambao, licha ya uhalifu wao wote dhidi ya Waislamu, wamefeli, bali wamewaamsha Waislamu zaidi juu ya Uislamu wao na kuwafanya kutambua kwamba wale wanaonyooshea mkono Amerika na washirika wake ndio vizingiti katika njia ya kurudi Uislamu katika utawala, hususan, katika njia ya kurudi kwa Khilafah Rashida ya pili.
Tunawaambia hao kwamba Khilafah Rashida kwa njia ya Utume yaja, kwa idhini ya Allah, kwa sababu ni ahadi ya Allah (swt) na bishara ya Mtume wake (saw). Na tunawakumbusha Waislamu maneno ya Allah (swt):
[وَلا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَبَقُوا إِنَّهُمْ لا يُعجِزُونَ]
“Na wala wasidhani wale waliokufuru wametangulia mbele [wameokoka na dhabu]. Hakika wao hawajashinda [mbele ya Allah].” [Al-Anfal: 59].
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |