Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  13 Safar 1439 Na: 1439/003
M.  Alhamisi, 02 Novemba 2017

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Wito wa Wakaazi wa Mashariki Mwa Ghouta kwa Vikao vya Kimataifa ni Mithili ya Kutafuta Hifadhi ya Joto Ndani ya Moto!
(Imetafsiriwa)

Jumapili iliyopita, serikali ya kikatili ilililenga soko maarufu na shule ya watoto eneo la Mashariki mwa Ghouta kwa silaha za mabomu, ikiwaua na kuwajeruhi maelfu ya raia, wakiwemo watoto na wanawake.

Hii hapa Mashariki mwa Ghouta, kama mikoa mengine ya Syria, ikilipa gharama kubwa, takwimu zikionesha kuwa zaidi ya watu 18,000, wakiwemo takriban watoto na wanawake 6,000, waliuwawa, kando na kukabiliwa na mauaji ya kinyama kupitia silaha za kemikali mnamo 21 Agosti 2013. Picha za mifupa ya watoto zinaendelea kusambazwa katika vyombo vya habari na mtandaoni kudhihirisha mateso ya watu wapatao 400,000.

Wale waliokwama eneo la Mashariki mwa Ghouta wanaishi katika mizozo huku wakikabiliwa na njaa na maradhi, ambapo misaada ya kibinadamu ni haba, na chakula na madawa ni haba mno, na hawana uwezo wa kununua kile ambacho chapatikana kwa nadra sana kwao, huku, msafara wa mwisho wa misaada wa UM ukiingia mnamo 23 Septemba mwaka jana na msaada wa takriban watu 25,000 waliokwama katika miji ya Harasta Mashariki, Misraba na Madeira, licha ya azimio la Baraza la Usalama nambari 2254 juu ya kuifanya upya leseni ya kuingia Syria kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Iweje Baraza la Usalama, ambalo liliasisiwa ili kufaulisha maslahi ya nchi za kilafi za kikoloni katika biladi za Waislamu… iweje iondoe dhulma za serikali hii ya kikatili na kuyaondoa mashaka haya kwa Waislamu!!! Lakini la kushangaza ni pindi tuonapo serikali hizi katika biladi za Waislamu zikikimbilia kuomba usaidizi, misaada na kuchunguza uhalifu huu, kana kwamba wanajali sana ushindi kwa wanaonyanyaswa au kupatikana kwa haki!

Hili likiongezewa na takwimu za mashirika na jumuia, mpya katika takwimu hizi ni ripoti ya Hazina ya Watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF) kuwa zaidi ya watoto elfu moja wa Mashariki mwa Ghouta wanateseka kutokana na ukosefu wa lishe bora, ambayo imetuacha vinywa wazi. Ni nini kilichopelekea ripoti kama hizi, ambazo zimezoeleka, zenye kuhesabu maiti, wenye njaa na majeruhi miongoni mwa Waislamu wanaoteseka kila mahali? Je, ripoti hizi zimekomesha muungano wa mashambulizi ya anga na serikali kutokana na kutekeleza mauaji!! Je, dola zilizoko leo katika ulimwengu wa Kiislamu zilitaharuki pindi ziliposoma ripoti hizi au hata zilipoona picha za kuogofya za mifupa ya watoto?! Au je, habari hizi za kuhuzunisha na uovu wa janga la kibinadamu eneo la Mashariki mwa Ghouta yamegeuka kuwa mambo ya kimaumbile ya kawaida, yanayotarajiwa kuendelea, na hata kuzidi, mithili ya majanga mengine yaliyouzonga Ummah wa Kiislamu?!  

Kanuni ya kimataifa imeuorodhesha uhalifu unaofanywa nchini Syria kama mbaya zaidi, tangu Machi 2011. Mwishoni mwa 2017, hali ya maafa ya kibinadamu na uhalifu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha imeendelea kuwa mbaya kutokana na kudumu kumwagwa kwa mabomu, uvamizi wa kudumu na kufuata sera ya kimakusudi ya kuwanyima chakula raia katika maeneo ya uasi, ambayo inakadiriwa kuwa mojawapo ya mbinu za vita hivi vya kinyama. Yote haya yanathibitisha kuhusika kwa kila mmoja katika khiyana dhidi ya mapinduzi haya tangu kuzuka kwake. Vile vile inathibitisha udhaifu wa watawala wa Waislamu, wakiongozwa na Erdogan aliyeharakisha kuingia Idlib, kutekeleza mapendekezo ya walio jadiliana mjini Astana pasi na kusitasita, huku maelfu wakiteseka na kulia kutokana na njaa na maradhi, wakikosa mtu wa kuwaokoa na kuwasaidia isipokuwa Allah Ta’ala, ambaye tunamuomba awape Waislamu jumla faraja ya karibuni, na haswa watu wa Syria, walio na bishara njema kutoka kwa Hadith ya Mtume wa Allah (saw):

«إِنَّ فُسْطَاطَ الْمُسْلِمِينَ يَوْمَ الْمَلْحَمَةِ بِالْغُوطَةِ، إِلَى جَانِبِ مَدِينَةٍ يُقَالُ لَهَا: دِمَشْقُ، مِنْ خَيْرِ مَدَائِنِ الشَّامِ»

“Hakika ngome ya Waislamu siku ya vita itakuwa eneo la Ghouta karibu na mji unaoitwa: Dimishqi, ambao ni miongoni mwa miji bora ya Sham.”

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu