Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  7 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 021
M.  Jumanne, 10 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto wa Palestina Watakuwa Mahasimu wa Ummah na Majeshi Yake Siku ya Kiyama iwapo Hawatasonga Kuwanusuru
(Imetafsiriwa)

Msichana mwenye umri wa miaka 13, Bana Amjad Bakr, aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi kifuani na wanajeshi wavamizi jioni ya Ijumaa, Septemba 6, 2024, wakati wa shambulizi la walowezi, wakisaidiwa na vikosi vya uvamizi, kwa kijiji cha Qaryut, kusini mwa Nablus katika Ukingo wa Magharibi. Baba ya shahidi huyo alisema kwamba binti yake alipigwa risasi akiwa ndani ya chumba chake nyumbani na dada zake. Kwa kuuawa shahidi Bana Bakr, idadi ya mashahidi katika Ukingo wa Magharibi tangu tarehe 7 Oktoba imeongezeka hadi 692, wakiwemo watoto 159, kulingana na data kutoka Wizara ya Afya ya Palestina.

Umbile la Kiyahudi na walowezi wake wanaendelea na ghasia zao, wakitekeleza mauaji na mashambulizi ya kikatili dhidi ya watu wa ardhi iliyobarikiwa huko Gaza na Ukingo wa Magharibi, bila kuwasaza wazee wala vijana, wanaume au wanawake. Hakuna anayejisikia salama tena, si ndani ya nyumba zao wala nje. Msichana huyu mdogo alipigwa na risasi za uvamizi akiwa ndani ya chumba chake. Hili halishangazi kutoka kwa umbile hili halifu, ambalo limevunja majumba juu ya vichwa vya wanawake na watoto huko Gaza.

Umbile hili halifu na makundi yake ya walowezi wameendelea katika dhulma na jeuri yao kwa sababu Umma wa Kiislamu umetulia tuli, hauinuki kukomboa Masrah ya Mtume (saw), kukomesha mauaji ya halaiki huko Gaza, na kuondoa dhulma kutoka kwa watu wa ardhi iliyobarikiwa. Umma wa Kiislamu unaendelea kutazama jinai hizo za kinyama bila ya kuchukua hatua za kuondoa vikwazo vinavyowazuia kuwanusuru ndugu zao wanaodhulumiwa. Vikwazo hivi ni pamoja na watawala vibaraka, hasa wale wa Misri na Jordan, ambao wamekula njama na umbile hili halifu, wakailinda mipaka yake, na kuufunga pingu Ummah na majeshi yake wasiinuke kuwanusuru kaka na dada zao. Ummah lazima usonge mara moja kuwaondoa watawala hao na kufungua mipaka bandia iliyowekwa na wakoloni na mabwana wao ili kuugawanya na kuukata Umma wa Kiislamu. Baada ya yote, Mtume (saw) aliusifu Ummah huu kuwa kama mwili mmoja, na inapotokea kiungo chake chochote kinashtakia maumivu, mwili mzima hujibu kwa kukosa usingizi na homa.

Wameendelea na dhulma na jeuri zao kwa sababu majeshi ya Waislamu hayajawaasi watawala wasaliti na kujifungamanisha na Ummah wao, hivyo kupata radhi za Mwenyezi Mungu, kuwanusuru ndugu zao na dada zao, na kuliondoa umbile hili halifu. Ikiwa sio sasa, ni lini wanyoofu katika majeshi haya watanyanyuka? Wanawezaje kuishi kwa amani huku ndugu na dada zao wakiteseka, wakijua fika wao wana uwezo wa kuwanusuru na kuondoa ukandamizaji kutoka kwao?

Enyi Umma wa Uislamu, na hasa wale wenye nguvu na uwezo: Kama hamtavipindua viti hivi vya enzi na kuyahamisha majeshi haya, basi mtoto huyu, pamoja na watoto wengine wote ambao ni wahanga wa ukatili wa umbile hili halifu, watasimama kama watuhumu wenu katika Yawm Al-Qiyamah (Siku ya Kiyama). Watalia, “Ya Rabb, Umma wa Uislamu na majeshi yake watutelekeza.” Siku hiyo hapatakuwa na pa kukimbilia wala kuepushwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Basi jiokoeni, na timizeni wajibu wenu wa Kishari’ah, na mpate heshima ya maisha haya na Akhera. Kwa mikono yenu, ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ukhalifa na tamkini itatimia, pamoja na bishara njema ya Mtume (saw) kwamba Mayahudi watapigwa vita, na Ardhi Iliyobarikiwa itakombolewa.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu