Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 9 Rabi' I 1446 | Na: H 1446 / 022 |
M. Alhamisi, 12 Septemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaka Mpya wa Shule bila Shule au Wanafunzi!
(Imetafsiriwa)
Mwaka mpya wa shule umeanza katika Ukingo wa Magharibi na Al-Quds inayokaliwa kwa mabavu huku Ukanda wa Gaza ukiendelea kukabiliwa na vita vya mauaji ya halaiki bila ya shule wala elimu, ikiwa ni pamoja na kuharibiwa idadi kubwa ya shule na kuzigeuza shule zilizosalia kuwa makaazi.
Umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu linaendelea na vita vyake dhidi ya elimu huko Gaza kwa mwaka wa pili mfululizo, kwani mwaka uliopita wa shule ulimalizika kwa siku za kwanza za vita vya uharibifu kwenye Ukanda wa Gaza. Kwa muda wa miezi 11, uvamizi huo umekuwa ukilenga shule ambazo makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makaazi yao wamekimbilia, baada ya nyumba zao kuharibiwa kabisa. Shule na vyuo vikuu vingi vimeharibiwa; Shule na vyuo vikuu 122 viliharibiwa kabisa, na shule na vyuo vikuu 334 viliharibiwa kwa kiasi. Ripoti zinaonyesha kuwa watoto 625,000 wenye umri wa kwenda shule na takriban wanafunzi 80,000 wa vyuo vikuu wamenyimwa mwaka mzima wa masomo. Wanafunzi 39,000 pia walinyimwa kufanya mtihani wa shule ya upili (Tawjeehi), na watoto 58,000 walinyimwa furaha ya kuingia darasa la kwanza.
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu ya Palestina, wakati wa vita hivi vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, vikosi vya Mayahudi viliua zaidi ya wanafunzi 10,000 wa kiume na wa kike, huku zaidi ya wanafunzi 15,000 wakijeruhiwa, na takriban wanafunzi 19,000 walilazimika kuondoka Ukanda wa Gaza. Wizara hiyo pia ilionyesha kuwa zaidi ya walimu 400 wa shule, wanaume na wanawake, na maprofesa na watafiti zaidi ya 110 wa vyuo vikuu waliuawa shahidi.
Vita hivyo vimebadilisha maisha ya wanafunzi hao kutoka kwa madawati na vitabu hadi kutafuta kuni za kuwasha moto kwa ajili ya kupikia, au kutafuta chakula, maji na kusaidia familia zao, baada ya vikosi vya uvamizi kufukia vitabu na madawati yao chini ya vifusi. Badala ya kubeba vitabu na vifaa vya shule katika mifuko yao ya shule, wao huijaza kwa mabaki ya vitu vyao muhimu, kwa ajili ya maandalizi ya uhamisho mpya, na kujaribu kuokoa maisha yao kutokana na hofu ya mauaji ya halaiki, baada ya mara kwa mara kuonja uchungu wa kupoteza nyumba na familia zao.
Haya yote yanatokea mbele ya ulimwengu mnafiki na mzembe, ikiwemo UNICEF na mashirika ya kutetea haki za watoto ambao wanaendelea kuimba kuhusu haki za watoto, ambazo kwao zimefungika kwa uasi dhidi ya dini, familia na wazazi. Kinachotokea Gaza hakiko ndani ya maslahi yao au kazi zao!
Enyi Umma wa Kiislamu, na Enyi Watu wa Palestina: Ingawa sera na mitaala ya elimu iko chini ya maagizo ya nchi za Magharibi, na haina dori thabiti, Mayahudi hawataki hata vipengee msingi kabisa vya elimu kwa watu wa Palestina. Mauaji ya halaiki na ujinga havitakoma kwa sababu tu vita hivi viishe au mashini za uharibifu, mauaji na watu kuyahama makaazi yao visimame kwa muda, bali yatakuwa ni kupitia ukombozi wa Gaza, al-Quds na maeneo mengine ya Palestina. Hili halitatokea isipokuwa kwa jeshi la Waislamu linaloongozwa na Imamu kiongozi anayetawala kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu pekee na hukmu na maamrisho Yake. Elimu itaegemezwa juu ya ́Aqida ya Kiislamu hivyo itaregesha thamani na nafasi yake katika mwamko wa kweli, na mwalimu na shule vitaregea katika nafasi yao stahiki, kama ambavyo dori ya Al-Kisa’i na Al-Shaibani ili kuwa katika dola ya Kiislamu, ambayo itaregea chini ya dola ya pili ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya utume” ambayo itatenda miongoni mwa watu kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (saw).
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |