Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  13 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 037
M.  Jumatano, 16 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji Mapya na Msimamo wa Majeshi yetu ni Ule Ule!

Je, hakuna Mwenye Hekima Miongoni mwenu Awezaye Kurudisha Izza Tena?!
(Imetafsiriwa)

Moto mkubwa na miili iliyoungua, matukio ya umwagaji damu yanayosifiwa kuwa ya kikatili zaidi tangu kuanza kwa vita kwenye Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba mwaka jana. Katika kipindi chote cha mwaka mzima wa vita vya ardhini na angani vilivyoanzishwa na Uvamizi kwenye Ukanda wa Gaza uliozingirwa, mauaji haya yalikuwa ya umwagaji damu mbaya zaidi, kama ilivyoelezwa na wanaharakati, madaktari na waandishi wa habari.

Vikosi vya Uvamizi vililenga mahema ya watu waliokimbia makaazi yao katika Hospitali ya Al-Aqsa Martyrs huko Deir al-Balah, ambayo yalitengenezwa kwa nailoni, na kusababisha moto mkubwa ulioenea na kujumuisha mahema 30 yaliyo na wakaazi wake usiku wa manane, ambapo watoto na wanawake walikuwa wamelala, kujaribu kukamata kipindi cha usalama katika mwaka ambao haujaacha kujazwa na vitisho na hofu. Moto huo ulidumu kwa zaidi ya dakika 45 kabla ya maafisa wa ulinzi wa raia kuweza kuudhibiti, na kusababisha, kwa mujibu wa Al Jazeera, mashahidi wanne, akiwemo mwanamke na watoto, na zaidi ya majeruhi 45 ya kuungua kwa digrii ya pili na ya tatu. Ushuhuda wa moja kwa moja ulioshuhudia uchomaji huo ulisema kuwa waliouawa shahidi waliungua hadi kufa bila mtu yeyote kuweza kuwaokoa kutokana na nguvu ya moto huo.

Masaa tu yalitenganisha moto huu mbaya na mauaji yaliyotangulia mnamo Oktoba 13, 2024 kwa shambulizi la bomu lililolenga Shule ya Mufti katika kambi ya Nuseirat, ambapo watu wasiopungua 22 waliuawa, wakiwemo watoto 15 na mwanamke mmoja, pamoja na majeruhi 80, kulingana na afisi ya vyombo vya habari vya serikali katika Ukanda huo. Matukio yanaongezeka kwa kasi, na mwaka mzima umepita na Waislamu katika eneo dogo lililozingirwa wanaangamizwa kwa kimpangilio, na kurudisha kwenye historia hadithi za Watu wa Handaki. Mwaka mzima na Waislamu hawa, ambao ni sehemu ya Waislamu bilioni mbili, wanaungwa mkono katika hali bora zaidi kwa dua! Hivi kweli sisi ni Ummah wanyonge?! Hivi kweli Umma wa Kiislamu hauwezi kukata mikono ya Mayahudi na kuwazuia wasichezee Gaza, Msikiti wa Al-Aqsa na Palestina yote?!

Hapana, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitufahamisha kuwa sisi ni Umma wa kheri na jihad, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitupa bishara njema ya kwamba tutaifungua Roma, kwa hivyo Al-Quds iko karibu na ukombozi, Mwenyezi Mungu akipenda, kuwa mji mkuu wa dola inayokuja ya Khilafah, na historia kwa mapana yake yote inathibitisha kwamba sisi ni Ummah ambao hata tukilala kwa muda gani, tutaamka na kuwaondoa maadui zetu kwa pigo kubwa ambalo baada ya hapo hawana pa kukimbilia. Hivi ndivyo ilivyotokea kwa maadui zetu wote, kutoka kuanzia kwa Makruseda, Wamongoli, Warumi, Wafursi na wengineo, basi vipi kuhusu Mayahudi ambao sio watu wa kupigana na hawana maisha ya baadaye, kama wao wenyewe wanavyokiri kwa ndimi zao, kama tulivyoona mwaka mzima huko Gaza?!

Enyi majeshi ya Waislamu, wako wapi miongoni mwenu waliouza nafsi zao kwa Mwenyezi Mungu ili wapate kheri hii? Je, kushindwa kwenu kutadumu kwa muda mrefu mnapotazama chuki ya Mayahudi inavyozidi kuenea kadiri mnavyoendelea kukaa kimya, na mnaona jinsi gharama ya kimya chenu ilivyo nzito huku watu wa Palestina wakilipia kwa damu yao?

[إِنَّ اللهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْداً عَلَيْهِ حَقّاً فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” [At-Tawbah 9:111]

[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ]

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbya 21:106]

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu