Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 038
M.  Alhamisi, 17 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Heshima ya Wanawake wa Kiislamu ni ya Khiyari katika Demokrasia za Kiliberali

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 3 Oktoba, CBS News iliripoti kwamba mwanamke mmoja Muislamu alizuiliwa na polisi wa Philadelphia ambao walimvua hijabu yake. Wakati wa saa 20 ya kukamatwa kwake, aliachwa wazi na hakupewa njia ya kubadilisha nguo zake. Kwa sasa ameajiri mshauri wa kisheria kutoka Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani (CAIR) na anataka haki kwa unyanyasaji wake. Dada huyo alikamatwa kufuatia tukio katika Chuo Kikuu cha Temple mwezi Septemba, ambako alikuwa akipinga ukandamizaji wa Waislamu huko Gaza. Dada huyo alisema afisa mmoja alimvua hijabu yake na kofia yake ndogo. Adam Attia, mkurugenzi wa sheria wa CAIR Philadelphia, aliuita “unajisi mkubwa wa imani na desturi zake za kidini. Tunataka kufanyia kazi mabadiliko katika sera hizi ili kuanzia sasa wanawake wa Kiislamu wasiyapitie haya. Na sisi tuko tayari zaidi kushirikiana na kufanya kazi na shirika lolote, idara ya polisi, chuo kikuu ambacho kiko tayari kutusikiliza kwa sababu hilo ni jambo ambalo linakiuka pakubwa imani zetu za kidini.”

Idara ya Polisi ya Philadelphia (PDD) ilisema yafuatayo: “Tunatambua kwamba sera zetu zinahitaji kubadilika ili kuheshimu vyema na kuzingatia desturi za kidini… PPD inajitahidi kusasisha sera zetu ili kuruhusu uvaaji wa mitandio ya kidini wakati wa mchakato wa kusajiliwa na wakiwa kizuizini, mradi haiathiri itifaki za usalama au usalama.”

Kinachopaswa kueleweka katika tukio hilo ni kwamba uhangaishaji na unyanyasaji wa wanawake wa Kiislamu unafanywa kuwa jambo la kawaida duniani na ndani ya nchi na vyombo vile vile vinavyodai kuwa vinara wa dunia katika uwezeshaji wa wanawake na haki za wanawake. Mgongano wa wazi haungeweza kuwa wazi zaidi ya hivi. Walakini, bado kuna wawakilishi wa Waislamu ambao hawathamini kabisa namna Demokrasia ya Kiliberali ilivyopotea njia.

Huku Vita vya Gaza vikienea katika maeneo mengine ya Ash-Sham, ulipuaji wa mabomu ya moto na mauaji yanaenea zaidi, yakiwakumba wanawake na watoto wa Ummah huu kwa njia ambayo haijawahi kutokea katika historia ya hivi karibuni. Tunaweza kuona kwamba maisha na heshima ya kina mama wa Ummah huu hayana umuhimu kwa wale ambao wameuza damu zetu kwa wazabuni wa juu kabisa katika soko la madaraka na ufisadi: watawala na tawala za ardhi za Waislamu. Hakuna hata mmoja wa watawala wa Waislamu mwenye nia ya kutumikia maslahi ya umma huu na huo ni ukweli ambao kila mamlaka isiyokuwa ya Kiislamu inaujua vyema. Kwa hivyo, ni msimu wa wazi wa kwenda kuwinda mali na miili ya Ummah huu ili kukusanya kama tuzo za kuonyesha ulimwengu.

Tunahitaji mamlaka ya Kiislamu kuregea katika mfumo wa Khilafah kwa njia ya Utume ili kurekebisha ukosefu wa usawa huu wa uadilifu. Mashirika tuliyo nayo yanaweza tu kupanua bakuli za kuomba ili kujaza mabadiliko ya sera ambayo kamwe hayatawapa wanawake wa Kiislamu nafasi yao halali kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyoamuru. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَنِّي لاَ أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ]

“Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi.” [Aali-Imran:195]

Hadhi ya juu ambayo Uislamu unailinda heshima ya mwanamke wa Kiislamu inaonekana katika matendo ya kipenzi chetu Mtume (saw) ambaye alilifukuza kabila zima la Kiyahudi, Banu Qaynuqa kutoka katika dola yake ya Madina Al-Munawwara kutokana na kumnyanyasa mwanamke mmoja wa Kiislamu na kukiuka mavazi yake ya Kiislamu. Na bado leo, utu wa wanawake wa Kiislamu unavunjwa katika ardhi kote ulimwenguni bila serikali ya kutetea heshima yao. Tumechelewa kwa muda mrefu kwa kipimo sahihi cha jinsi maisha na utu wa wanawake wa Kiislamu lazima usimamiwe. Uongozi katika namna ya ruwaza sahihi ya Quran na Sunnah: Khilafah, ndiyo inayokosekana, sio idadi ya waumini, pesa au khairati. Kadiri sisi kama Umma wa Kiislamu tunavyotambua hili, ndivyo hali yetu itakavyobadilika haraka tusipokengeushwa na chenga za mkate wa mabadiliko.

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu