Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 29 Rajab 1446 | Na: H 1446 / 078 |
M. Jumatano, 29 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wauyghur Pia Ni Sehemu ya Umma Bora, Musiwasahau
(Imetafsiriwa)
Tunapokaribia kumbukumbu ya mwaka wa 104 wa kuvunjwa kwa Khilafah, Umma wa Kiislamu unaendelea kupokea habari za ukandamizaji kutoka kwa maadui wake kila mahali, kuanzia Palestina hadi Syria, Sudan, Misri na China, ambako Waislamu wa Uyghur wanavumilia mateso na vikwazo vikali katika kila nyanja ya maisha yao.
Licha ya vyombo vya habari vya China kuficha ukatili wake huko Turkestan Mashariki, baadhi ya habari za mateso ya Wauyghur bado zinatufikia. Taarifa hizi zinatilia nguvu uhakika wetu, siku baada ya siku, wa haja ya dharura ya Khilafah ambayo itarudisha heshima ya Waislamu na kuwalinda dhidi ya aina zote za uvamizi.
Mnamo tarehe 20 mwezi huu, BBC ilichapisha ripoti iliyopewa kichwa “'Jahannam duniani': China inakaribia kuwafukuza Wauyghur wanaoshikiliwa nchini Thailand” Ripoti hiyo inabainisha wanaume 47 wa Kiislamu wa Uyghur waliozuiliwa na Thailand mwaka wa 2014 baada ya kukimbia mateso katika nchi yao. Mmoja wa waliotoroka, mwanamke Muislamu anayeishi Uturuki tangu 2015, aliruhusiwa kuondoka Thailand na watoto wake watatu lakini bila mumewe. Sasa, anahofia kwamba ikiwa atafukuzwa nchini China, hatamwona tena.
Inafaa kukumbuka kuwa mnamo 2015, Thailand iliwafukuza kwa nguvu kundi la wakimbizi wa Uyghur kurudi China. Walirekodiwa wakiwa wamevaa kofia, wamefungwa pingu na kuzungukwa na idadi kubwa ya maafisa wa polisi wa China. Hatima yao bado haijajulikana, huku ripoti zikionyesha kuwa walikabiliwa na kesi za siri na vifungo virefu gerezani.
Kifungo cha muda mrefu ni mojawapo ya mbinu za China za kuwakandamiza Waislamu, kuzua mashtaka kama vile “kusoma au kufundisha Quran” na “kujifunza hukmu za Kiislamu.” Waislamu wa Uyghur wananyimwa haki zao nchini China, na wanawake wa Kiislamu hawapati ulinzi kutoka kwa yale yanayoitwa mashirika ya wanawake au mikataba kama CEDAW. Mwezi Juni mwaka jana, China ilimkamata Selihan Rozi, mwanamke wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 49, kwa kuwafundisha watoto wake na majirani zake aya za Qur'an kwa ajili ya swala. Alihukumiwa miaka kumi na saba jela! Afisa wa ndani wa Chama cha Kikomunisti aliiambia Radio Free Asia kwamba alifungwa kwa ajili ya “shughuli haramu za kidini.”
Wanawake nchini China wamefungwa kwa miaka mingi kwa ajili tu ya kusoma aya za Quran, licha ya kuwa ni haki ya kimaumbile ya binadamu iliyoainishwa katika sheria za kimataifa, sheria ambazo zinaonekana kutekelezwa pale tu zinapolenga Uislamu na Waislamu. Wakati huo huo, wanaume wa Kiislamu wanakamatwa na kuhamishwa kwa nguvu na kurudi kwenye jahanamu ile ile waliyowahi kutoroka, yote haya yakifanywa mbele ya macho ya ulimwengu, lakini hakuna anayepinga ukiukaji huu wa wazi wa haki yao ya kimsingi ya kutekeleza dini yao kwa uhuru.
Wakati huo huo, tumeona jinsi serikali za Magharibi zilivyoharakisha kuyakusanya kwa njia kujihami makabila madogo nchini Syria pindi mujahidina walipofanikiwa kuuangusha utawala uliokuwa ukiwatesa watu wake kwa miongo kadhaa.
Imedhihirika kwa mtu yeyote mwenye macho kuona kwamba mashambulizi ya kimataifa dhidi ya Waislamu yamefikia kilele chake, na kwamba kauli mbiu za haki za binadamu na haki za walio wachache si chochote ila masanamu wanayoyaabudu yanaposhughulikia maslahi yao, na kuyakanyaga chini ya miguu yao pindi haki hizo hizo zikenda kinyume na ajenda zao.
Lakini vipi kuhusu sisi Waislamu? Baada ya kushuhudia uadui wao, unafiki, na kutojali haki na utu wetu, je, mtu yeyote mwenye akili timamu bado anaweza kutarajia haki kutoka kwao?
Waislamu wa Uyghur, sawa na Ummah wote uliosalia, wanabakia kudhurika bila kuwepo dola inayowatetea na kiongozi anayewalinda. Maneno “Ahad! Ahad!” ambayo Bilal (ra) aliyatamka hayakumkinga na viboko vya Umayyah ibn Khalaf, kilichomkomboa ni Kiapo cha Pili cha Aqabah, Takbira za Badr, na panga za Mujahidina waliobeba bendera ya Uislamu chini ya ulinzi wa dola.
Mateso yanayovumiliwa na Ummah na jinai zinazotendwa na madhalimu dhidi yake hatimaye yatatoa njia ya kusimamishwa kwa muundo mkuu wa Uislamu Khilafah Rashida, nuru inayowaongoza wanaodhulumiwa na moto unaoteketeza madhalimu, ukitoa laana juu yao mpaka Siku ya Kiyama.
[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً] “na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Surat Al-Isra:51]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |